Ujumbe wa kumwambia umpendaye kuwa ni pengo lisilozibika milele kwa hiyo asikuache
nikipoteza kitu cha thamani nitauzunika nitasahau ila
nikikupoteza wewe ni pengo lisilozibika kamwe.
nikipoteza kitu cha thamani nitauzunika nitasahau ila
nikikupoteza wewe ni pengo lisilozibika kamwe.
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu “SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO”
moyo wangu saafi kama upole wa tausi wingi wa baridi kama maji ya mtungi ,yote ni kutokana na mapenzi unayonipatia. ASANTE KWA KUNIPENDA MPENZI
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi
nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu,
kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi
Penzi, maisha yangu yote nimesoma juu ya neno hili,
nimeota juu yake, nimelilia, nimelihitaji. Sasa pamoja
nawe nimelipata.
tazama, nimezama
ndani ya bahari
la penzi lako
siwezi
kusonga mbele
kurudi nyuma
sijielewi
haya mapenzi ya fujo hayafai
kama wanipenda
jaribu kunipa raha
Kukusahau wewe ni ngumu lakini kunisahau mimi ni juu yako.
Usinisahau kamwe, unaweza kuisahau meseji hii, lakini si
mtumaji.
Kuna miezi 12 katika mwaka…siku 30 katika mwezi…siku 7
katika wiki, masaa 24 katika siku…dakika 60 katika saa……
lakini wewe ni mmoja tu maishani mwangu.
Ningependa siku moja utamani sana kuwa na mimi, na
uhangaike sana kunitafuta, ili ujue ni kwa kiasi
ninavyotamani kuwa nawe sasa.
Recent Comments