SMS ya kumuonyesha mpenzi wako jinsi anavyokupagawisha
Watu waliniambia ninaweza kufanya chochote kama tu nitaweka mawazo yangu juu ya hicho kitu. Lakini kila nikijitahidi unaipoteza akili yangu
Watu waliniambia ninaweza kufanya chochote kama tu nitaweka mawazo yangu juu ya hicho kitu. Lakini kila nikijitahidi unaipoteza akili yangu
Utamu wako ni zaidi ya asali, ni wa asili usiohitaji kuongezewa ladha ya sukari, nitaumiss endapo kama ukiwa mbali “NIACHE NIKUPENDE SWEET”
Natamani ningekuwa chozi jichoni mwako ambapo ningetelemka
na kuishia midomoni mwako, lakini kamwe sitamani uwe chozi
jichoni mwangu nitakupoteza kila muda niliapo.
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Nakupenda kwa kuwa umegundua thamani ya penzi langu
nakuahidi utafaidi utamu wa mapenzi yangu
penzi linaweza kuelezewa kwa namna nyingi. Namna moja
niijuayo nikumtumia mapenzi hayo mtu asomaye meseji hii
Weupe wa penzi lako ni kama mwezi angani.Ucheshi na mahaba
yako nifananishe na nini? Kupata mfano wako hatotokea
amini. Elewa mimiwako sikuachi asilani
Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu
usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee,
lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.
Recent Comments