Ujumbe wa kimapenzi kumwambia mpenzi wako kuwa umelipata penzi ambalo ndio kutoka kwake tuu
Penzi, maisha yangu yote nimesoma juu ya neno hili,
nimeota juu yake, nimelilia, nimelihitaji. Sasa pamoja
nawe nimelipata.
Penzi, maisha yangu yote nimesoma juu ya neno hili,
nimeota juu yake, nimelilia, nimelihitaji. Sasa pamoja
nawe nimelipata.
Nakuomba usiondoke, bali ubaki nami
Kwani wewe ndiye kamilisho la maisha
Yangu kwa sasa na siku za usoni
Ama baada ya salamu, mimi ni mzima wa afya njema. Mie ni ndege nipo angani na nimetafuta mti wa kutua kila pembe ya dunia lakini sijaupata bado. Je naweza nikatua kwako?
mapenzi si pombe lkn yanalewesha, wala si kidonda lakini
yanatonesha,wala si maradhi lakini yanaumiza, wala si
njaa lakini yanakondesha ,mapenzi ni uvumilivu kwa
unaempenda
Fungua macho yako uone kopa za mahaba ninazokumwagia,
fungua mikono yako na upokee mapenzi yangu,
fungua simu yako uone ni jinsi gani ninavyokukumbuka japo
kwa kukutumia sms mpenzi wangu,
Nakutakia usiku mwema
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Umbo lako kama sayari, lizungukapo umbile la jua
ni kama upendo wa thamani usioweza kuuzika.
Unaweza usione kamwe ni kwa kiasi gani ninavyokujali.
Unaweza usisikie ni kwa kiasi gani nilivyokushiba, unaweza
usihisi namna gani ninavyokukumbuka. Sababu ni moyo wangu
tu uliyoyaficha hayo.
Naweza kuishiwa ujumbe wa kukutumia. Naweza kuishiwa utani
pia. Naweza kuishiwa chaji lakini moyo wangu hauwezi
kukosa nafasi ya kukuweka.
Kumjali mtu ni rahisi, lakini kumfanya mtu akujali ni
vigumu, nashangaa umewezaje kunifanya nikujali?
Recent Comments