Ujumbe mzuri wa kimapenzi wa kumwambia mpenzi mapenzi huanza na wewe na yeye
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo! “NAKUPENDA MALAIKA WANGU”
Uamkapo nitakupa langu tabasamu
Ukweli wa moyo utawale roho yako
Kwani macho yako ndo uzuri kwangu
Nakupenda sasa na milele kipenzi changu
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
pongezi kwako mpenzi kuwa wangu mtetezi kwenye jahazi la
mapenzi,ufundi na ujuzi unao hasa tuwapo wawili
chumbani.penzi lako halichakai daima huzaliwa upya.
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako,
naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Pokea sms yangu iliyojaa utamu, nimeipamba kwa maneno laini yenye ladha adimu, utamu wake ni kama apple haufanani na ndimu, nimeituma kwako sms hii ikuletee salamu “UHALI GANI MPENZI?”
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Mwanamke ni yule amfanyaye mwanamme auhisi uanaume wake,
wewe ni mwanamke mwenye sifa hizo.
Penzi langu kwako ni la milele, nitakuhifadhi moyoni
mwangu siku zote za maisha yangu, uwe wangu nami niwe wako
daima, nakupenda dearโฆ
Recent Comments