Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kufurahia Kila Siku katika Familia Yako

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kufurahia Kila Siku katika Familia Yako

Kuwa na familia yenye ushirikiano na furaha ni jambo muhimu sana katika maisha. Kwa kufanya hivyo... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za tabia na mienendo ya watoto wenu na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za tabia na mienendo ya watoto wenu na mpenzi wako

Kama wazazi na wenzi, tunajua kuwa kuna tofauti katika tabia na mienendo yetu. Lakini pia, inawez... Read More

Jinsi ya Kusaidiana katika kushughulikia matatizo ya afya na magonjwa na mpenzi wako

Jinsi ya Kusaidiana katika kushughulikia matatizo ya afya na magonjwa na mpenzi wako

Kusaidiana katika kushughulikia matatizo ya afya na magonjwa ni muhimu katika kujenga uhusiano wenye... Read More
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu hisia na mahitaji yako

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu hisia na mahitaji yako

Kuwasiliana kwa ufanisi kuhusu hisia na mahitaji yako ni muhimu sana katika uhusiano. Hapa kuna mwon... Read More
Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Mahusiano ... Read More

Njia za Kupunguza Mizozo ya Kijinsia katika Mahusiano

Njia za Kupunguza Mizozo ya Kijinsia katika Mahusiano

Mahusiano yanaweza kuwa magumu kwa sababu ya mizozo ya kijinsia. Mizozo hii inaweza kutokea kati ... Read More

Jinsi ya Kuunga mkono mpenzi wako katika masuala ya kazi

Jinsi ya Kuunga mkono mpenzi wako katika masuala ya kazi

Kuunga mkono mpenzi wako katika masuala ya kazi ni muhimu katika kujenga uhusiano wenye nguvu na kuo... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kitamaduni na desturi za kikabila na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kitamaduni na desturi za kikabila na mpenzi wako

Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuwa tofauti kati ya wewe na mpenzi wako. Hii inaweza kuwa kitam... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya historia na utamaduni wa jamii yenu

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya historia na utamaduni wa jamii yenu

Siku zote ni muhimu kuwa na mawasiliano mazuri na mpenzi wako, na moja ya mambo muhimu ni kuwasil... Read More

Kuimarisha Ushawishi wa Mwenzi katika Kufanya Mapenzi: Kuelewa na Kujibu Mahitaji yao

Kuimarisha Ushawishi wa Mwenzi katika Kufanya Mapenzi: Kuelewa na Kujibu Mahitaji yao

Mapenzi ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu, na kila mtu anapenda kufanya mapenzi yenye ubor... Read More

Mbinu za kumfanya mwanamke akukubali

Mbinu za kumfanya mwanamke akukubali

Njia za kumfanya akukubali ni kama ifuatavyo

Uwe na muonekano mzuri

Wanawake wana... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kuishi kwa Nia na Dhati katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Kuishi kwa Nia na Dhati katika Familia Yako

Kuishi kwa nia na dhati katika familia yako ni muhimu sana kwa afya ya kiroho na kiakili ya kila ... Read More