Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na hofu na wasiwasi katika uhusiano na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na hofu na wasiwasi katika uhusiano na mpenzi wako

Hofu na wasiwasi ni hisia za kawaida katika uhusiano wowote, na ni muhimu kujifunza jinsi ya kuziele... Read More
Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha ushirikiano wa kifedha na kuweka malengo ya pamoja katika familia ni muhimu sana kati... Read More

Jinsi ya Kuwa Msaada katika Safari ya Kiroho ya mke wako

Jinsi ya Kuwa Msaada katika Safari ya Kiroho ya mke wako

Kuwa msaada katika safari ya kiroho ya mke wako ni jambo muhimu katika kujenga uhusiano wa kiroho na... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali wanyama

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali wanyama

Kama mpenzi wa wanyama, tunajua jinsi inavyokuwa muhimu kuwasaidia na kuwajali. Lakini, kuna nyak... Read More

Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii katika Familia: Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki

Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii katika Familia: Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki

Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii katika Familia: Kuweka Muda kwa Ajili ya Marafiki

Famili... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kudumisha afya na ustawi wa akili

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kudumisha afya na ustawi wa akili

Kusaidiana na mpenzi wako katika kudumisha afya na ustawi wa akili ni muhimu katika kujenga uhusiano... Read More
Kufanya Mapenzi ya Kufurahisha na Mazoezi ya Kujiboresha: Jinsi ya Kufurahia Vyote

Kufanya Mapenzi ya Kufurahisha na Mazoezi ya Kujiboresha: Jinsi ya Kufurahia Vyote

  1. Kufanya mapenzi ni jambo muhimu katika uhusiano, lakini ni muhimu pia kujiboresha kiafy... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kuweka Mipango ya Elimu katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kuweka Mipango ya Elimu katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kuweka Mipango ya Elimu katika Familia

Elimu ni muhi... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Maana na Wazee katika Familia: Kusikiliza na Kujifunza

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Maana na Wazee katika Familia: Kusikiliza na Kujifunza

Leo tunazungumzia jinsi ya kuwa na Mazungumzo ya Maana na Wazee katika Familia: Kusikiliza na Kuj... Read More

Dalili za mahusiano feki, mahusiano ya kichina

Dalili za mahusiano feki, mahusiano ya kichina

Ukitaka kujua Simu ya Kichina utajua tu jinsi ilivyo na makelele mengiiiii sana wakati wa kuitaβ€... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Uaminifu na Watoto Kuhusu Afya ya Akili na Vizazi

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Uaminifu na Watoto Kuhusu Afya ya Akili na Vizazi

  1. Kuanza kuzungumza na watoto wako mapema: Ni muhimu kuanza kuzungumza na watoto wako map... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Mawasiliano ya Upendo katika Mahusiano yako

Kuweka Kipaumbele cha Mawasiliano ya Upendo katika Mahusiano yako

Mahusiano ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Kila mtu anataka kuwa na mtu wa kumpenda na kuwa na uh... Read More