Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ndoa sio utani. Soma stori hii

Featured Image

"Mkeo amefariki. Rudi nyumbani kwako haraka sana" Hezron alimwambia Daniel katika simu.

"Mke wangu amekufa? Nini kimetokea? Amekufaje?" Daniel aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa vibaya.

"Daktari amesema ni shinikizo la moyo lililosababishwa na stress kali. Daktari na polisi wapo hapa nyumbani kwako. Njoo haraka" Hezron akaongea kidogo na akakata simu.

Muda anapigiwa simu na Hezron, Daniel alikuwa mtoko na mwanamke mwingine mrembo katika moja ya hoteli kubwa iliyoko maeneo ya Kunduchi. Alikuwa akifurahi nae huku wakinywa vinywaji ghali na chakula cha hadhi ya nyota tano. Lakini baada ya kupokea tu ile simu ya taarifa ya kifo cha mkewe, Daniel alichanganyikiwa, uso wake ukabadilika.

Hezron ni rafiki yake wa karibu.

Daniel akainuka na kuondoka katika ile Hotel akimwacha yule mwanake Mrembo.

"Kuna tatizo gani?" Yule mrembo aliuliza.

"Siwezi kuzungumza" Daniel alijibu na kuondoka haraka.

Daniel akaenda alikopaki gari yake, akaingia, akaiwasha na kukanyaga mafuta, akaiondoa kwa kasi ya ajabu.

Akiwa anaendesha, Daniel akakumbuka jinsi yeye na mkewe anaeambiwa amefariki walivoenda pamoja Showroom ya magari na kununua hilo gari pamoja.

Akiwa anakata kona, akakumbuka jinsi alivyokuwa akimfundisha mkewe kuendesha gari. Hizo zilikua nyakati njema kabisa katika maisha yao ya ndoa.

"Mke wangu amekufa! Kweli mke wangu amekufa! Mungu wangu.." alilia sana huku akiendesha.

Akakumbuka siku ya ndoa yao. Agano waliloliweka pamoja. Akiwa anabadilisha gia, akaangalia vidole vyake asiione pete yake ya ndoa. Pete ya ndoa aliitoa ili kudanganya wanawake wengine kwamba hajaoa.

Daniel akakumbuka ni jinsi gani alivyokuwa akimjibu mkewe hovyo, kwamba anayo kila sababu ya kufurahia maisha na kuponda raha. Akakumbuka maneno ya kuchoma aliyokuwa akimwambia mkewe kwamba yeye amezaa na amezeeka!

"Mke wangu amefariki! Kwanini umefariki Lisa! Kwanini Mungu? Alijiuliza maswali lukuki.

Jibu likamjia. Akakumbuka ni nini Hezron alimwambia. Kwamba mkewe yawezekana amekufa kwa shinikizo la damu kutokana ma stress. Kwa hali hiyo Daniel nimemuua mke wangu.

"Nimemuua mke wangu mwenyewe. Mungu nisamehe…" alijutia huku akiendesha gari kwa kasi.

Daniel akakumbuka jinsi mambo yalivyoenda vibaya katika ndoa yake. Jinsi gani upendo ulikimbia katika ndoa yao. Jinsi gani walivyoanza mabishano na ugomvi. Takribani mara nne ameshampiga mkewe vibao. Alikuwa mtu mbaya kwa mkewe na kwa watoto wake wadogo wawili.

Alifikiri aache kuhudumia familia, hitaji lake likaja kuwa kutomheshimu mkewe, kutomheshimu mkewe kukaleta dharau na maneno ya kejeli kwa mkewe, maneno ya kejeli yakasababisha vidonda vya tumbo kwa mke mwema Lisa kutokana na mawazo na kutokula.

Naam, Lisa aliugua vidonda vya tumbo kutokana na maumivu ya mawazo aliyosababishiwa na mumewe. Afya yake ilikongoroka, umbo lake zuri namba nane lilipotea, Lisa alionekana kama mzee, wakati ni mwanamke wa miaka 29 tu. Ila Daniel hakujali, alimzarau. Alijibadili kutoka mume aliyempenda mkewe kuwa mtu msaliti, anayemuumiza mkewe. Lisa amefariki!!?

Akiwa bado anaendesha akakumbuka jinsi alivyomfuata Lisa na kumuomba wafunge ndoa, Lisa alikuwa mzuri, akijitegemea na mwenye furaha na maisha. Yeye kumuoa tu ndio ikawa kumharibu, kumuumiza na mwishowe kumuua kwa stress!

Atakufaje? Hawezi kujua kwa sababu hajarudi nyumbani wiki moja sasa imepita, hajui watoto wanakula nini, wanavaa nini. Mke wake alikuwa akimtumia texts na kumpigia akimsisitizia arudi nyumbani, ila kilio cha mkewe kilitua katika masikio yake ambayo hayasikii. Mkewe alikuwa akilia, akipiga kelele mumewe arudi nyumbani, yote hayo ni kwa ajili ya kuokoa ndoa yake. Lakini mimi Daniel sikusikia. Sasa amefariki!

"Mimi nitafanya nini na watoto wangu?" alifikiria nafsini kwake. Watoto wawili alionao ambao alikuwa hawajali kwa sababu ya kuwa busy na warembo wa jiji la Makonda. Akakubali kwamba kweli mke wake alikuwa na moyo wa ajabu, kuwatunza watoto wale wawili bila msaada wake.

"Nani atanisaidia kuwalea? " Wanawake ambao amekuwa akila nao bata hawawezi kumsaidia kulea watoto, sio wife material wale, wife material hawezi kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzake. Alifikiria nafsini mwake.

Wazazi wa mkewe watafikiri nini?
Watu watafikiri nini? Mungu ananifikiriaje?
Hii ndio inaishaje ishaje? Ndoa yangu ndio imeishia hivi? Mke wangu kafariki?

Daniel akapaki gari, akatoka na kukimbia ndani ya nyumba.

Akafungua geti, akafungua mlango. Akamuona Hezron, rafiki yake akiwa amesimama katika korido ya nyumba yake.

"Kimetokea nini? Haiwezekani kuwa amekufa. Hawezi kufa. Mimi nitafanya nini Hezron?" Daniel aliongea akiwa amekata tamaa.

Hezron akamkumbatia Daniel.

"Uko sawa Daniel?" Hezron aliuliza.

"Nitakuaje sawa wakati mke wangu amekufa? Mama wa watoto wangu! Uko wapi mwili wake?" Daniel aliuliza.

"Upo sebuleni" Hezron alijibu.

Daniel akakimbia kuelekea sebuleni.

Mshangao!!

Akamwona mkewe akiwa hai. Amekaa katika sofa akiwa na mke wa Hezron ambae ni daktari wa saikolojia pembeni.

"Haujafa?!" Daniel aliuliza akiwa na mshangao

"Ndio hajafariki. Ila kama ukiendelea na hii tabia atafariki siku moja. Mkeo hajawa sawa kabisa. Amekuwa akijaribu kukutafuta na kukurudisha nyumbani ila umempuuza. Taarifa za kifo chake zimekufanya ukimbie kama mwehu. Ulitakiwa ukimbie kwa ajili ya maisha yake na si kwa ajili ya kifo." Mke wa Hezron aliongea.

Daniel akakaa katika kochi mbele ya mkewe na akamshika uso wake. Mkewe akarudishwa kichwa nyuma.

"Natumaini kwamba safari yako ya uchungu kuja hapa ukifikiri mkeo amekufa itakukumbusha ni nini cha muhimu kinachotakiwa kufanywa. Usisubiri mpaka uchelewe ndio ufanye jambo jema. Unayo nafasi ya pili." Aliongea mke wa Hezron

Daniel akanyanyua mkono wa mkewe machozi yakimtiririka, asiamini juu ya kile anachoshuhudia.

"Ndoa sio lelemama nyie wawili. Acheni kucheza michezo ya kipumbavu na maisha. Kesho sio garantii" aliongeza mke wa Hezron.

"Nyie wawili mna matatizo. Mmeridhika na matatizo ya kuumizana hasa wewe shemeji yangu Daniel. Kesho haiwezi kuwa pale kwa ajili yako kwa ajili ya kuomba msamaha. Mkewe Hezron aliongea.

"Na siku ya kiama tutakapokutana na mwenyezi Mungu, Daniel kitu ambacho Mungu atauliza ulimtendaje mke wako ambae ni ubavu wako? Huyu ni binti wa Mungu. Unavomuumiza yeye na Mungu anaumia pia" Akaongezea Hezron.

Mke wa Daniel akamgeukia Hezron na mkewe akasema "Nashukuruni sana kwa kupanga hii idea ya kumuamsha mume wangu, sio siri nilitamani kufa hata leo. Ninampenda sana ila nimechoka na maumivu. Ninyi ni marafiki bora wa familia yetu.

Daniel akamkumbatia mkewe tightly na akasema "Nisamehe sana Lisa wangu, sitaki kukupoteza. Leo nimeshuhudia familia yangu ikivunjika vipande vipande. Nilikuwa kipofu tena katikati ya giza tororo ila sasa ninaona. Usife tafadhali. Nitafanya yale yaliyo bora kuanzia sasa.

Rafiki yangu Hezron na shemeji yangu Julieth ninyi ni marafiki bora kabisa, rafiki aliye bora hukuondoa katika kiza na kukuweka katika nuru. Mmedhihirisha hilo. Naomba niwaahidi tukio hili limekuwa funzo kubwa kwangu. Naanza sasa kuwa mume na baba bora wa familia. Ila siku nyingine msinitishie kifo, naweza kufa kwa pressure na mimi. Nawashukuruni sana. Mwenyezi Mungu awajazi.

"Hahaaa Okey yaishi maneno yako, Mke wangu na mimi tunawaacha, tuwaache mfanye yale ambayo wanandoa wawili wanaopendana kweli hufanya." Hezron aliongea.

Na wakaondoka!

Mpende mwanandoa mwenzako, waheshimu wazazi, wabariki watoto wako, wapende rafiki zako, wote wakiwa bado wako hai.

Kabla hujachelewa!

Busara yangu,.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kukabiliana na Mazoea ya Kutowajali katika Mahusiano: Kuweka Thamani ya Kuwasiliana na Kuonyesha Kujali

Kukabiliana na Mazoea ya Kutowajali katika Mahusiano: Kuweka Thamani ya Kuwasiliana na Kuonyesha Kujali

Kukabiliana na Mazoea ya Kutowajali katika Mahusiano: Kuweka Thamani ya Kuwasiliana na Kuonyesha ... Read More

Mbinu 6 za Kujenga Uhusiano wa Kimwili na Kihisia na mke wako

Mbinu 6 za Kujenga Uhusiano wa Kimwili na Kihisia na mke wako

Kujenga uhusiano wa kimwili na kihisia na mke wako ni muhimu katika kuimarisha ndoa na kuendeleza in... Read More
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya teknolojia na mawasiliano ya kisasa

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya teknolojia na mawasiliano ya kisasa

  1. Anza kwa kumwuliza mpenzi wako kuhusu teknolojia wanayoipenda Je, ni smartphones, table... Read More

Njia za Kuweka Mipango ya Pamoja na Malengo katika Mahusiano yako

Njia za Kuweka Mipango ya Pamoja na Malengo katika Mahusiano yako

Mahusiano ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Kama tunavyojua, ili kufanikiwa katika mahusiano yetu,... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano ya Wazi na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano ya Wazi na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano ya Wazi na Msichana Wako

Ndoa ni muunganiko wa wawili kuwa ki... Read More

Kujenga Furaha ya Kijinsia katika Ndoa: Mazoezi ya Kuimarisha Uhusiano

Kujenga Furaha ya Kijinsia katika Ndoa: Mazoezi ya Kuimarisha Uhusiano

Kujenga Furaha ya Kijinsia katika Ndoa: Mazoezi ya Kuimarisha Uhusiano

Ndoa ni muungano wa... Read More

Jinsi ya Kusimamia Fedha pamoja na Mke wako

Jinsi ya Kusimamia Fedha pamoja na Mke wako

Kusimamia fedha pamoja na mke wako ni muhimu katika kudumisha hali nzuri ya kifedha na kuepuka migog... Read More
Njia za Kuimarisha Umoja wa Kifamilia na Kuweka Maadili ya Pamoja

Njia za Kuimarisha Umoja wa Kifamilia na Kuweka Maadili ya Pamoja

Umoja wa kifamilia ni kitu muhimu katika maisha ya kila mmoja wetu. Familia ndiyo kitovu cha mais... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kujisahau katika Familia: Kuweka Thamani ya Kujali na Kuthamini

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kujisahau katika Familia: Kuweka Thamani ya Kujali na Kuthamini

Familia ni kitu kizuri sana kwa sababu hutoa faraja, upendo, na usalama kwa wanachama wake. Hata ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha uhusiano wa karibu na ndugu na jamaa

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha uhusiano wa karibu na ndugu na jamaa

Kuhusiana na mahusiano ya familia, hakuna chochote kinachoweza kuwa juu ya upendo wa karibu na nd... Read More

Kufanya Mapenzi ya Asubuhi au Jioni: Upendeleo Wa wengi ni Upi?

Kufanya Mapenzi ya Asubuhi au Jioni: Upendeleo Wa wengi ni Upi?

Kufanya mapenzi yako wakati gani hasa? Asubuhi au jioni? Hii ni swali ambalo wengi hujikuta wakij... Read More

Kukuza Mshikamano na Umoja katika Mahusiano ya Kifamilia

Kukuza Mshikamano na Umoja katika Mahusiano ya Kifamilia

Mahusiano ya kifamilia ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Ni muhimu sana kukuza mshi... Read More