Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Featured Image

Ishara hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda, wasichana wanatofautiana ila wengi wao wana-share ishara tofauti. Mwanamke anayekupenda hatakosa kati ya hizi

Siyo kwamba ishara hizi zote anaweza kuwanazo msichana mmoja, ila kila mmoja kwa ishara zake.

Ishara hizo ni kama ifuatavyo

1. Mnapokutana na kuongea

Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea, ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu. Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia. Sikiliza sauti yake, kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.

2. Ajali za kijitakia

Anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike. Anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia, au anakukumbatia.

3. Anaibia kukuchunguza

Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia, ukigeuka anajifanya yuko bize na mambo yake kumbe anakuchunguza taratibu.

4. Anapenda mgusane

Mwanamke anayevutiwa na wewe mnapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako, au unapokutana naye anaweza kukukumbatia.

5. Anatafuta ukaribu

Mwanamke aliyevutiwa na wewe anapenda kuwa karibu na wewe muda wote. Mfano akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta, ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake kuhusu wewe. Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga, hata kama mmeenda out pamoja na marafiki
zake utakuta yupo karibu na wewe.

6. Anapenda umjali

Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie, mfano mmeenda mahali kukawa na baridi hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako, hata kama kuna watu hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.

7. Hawezi kuzuia tabasamu

Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee, hata kama kuna kitu kimemwudhi atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.

8. Ishara za mwili

Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini. Kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani, utamwona anashtuka gafla.

9. Anafurahishwa na vituko vyako

Mwanamke anayekupenda daima ni mwenye furaha mkiwa pamoja. Huwezi ukamboa, hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.

10. Anakujali

Anakuwa anakujali, mfano akiona umeumia labda umejigonga, yupo radhi akuhudumie. unapokuwa naye anaweza kuuliza "unahitaji chochote? unaweza ukasema "nina kiu ngoja ninunue maji" utamsikia "nina maji, kunywa haya yangu kwanza".basi ujue kwamba anakujali.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Usawa katika Mahusiano: Kujenga Umoja na Uwiano

Mahusiano ... Read More

Ushawishi wa Vyombo vya Habari katika Maoni yetu ya Kufanya Mapenzi: Kuchambua na Kuelimisha

Ushawishi wa Vyombo vya Habari katika Maoni yetu ya Kufanya Mapenzi: Kuchambua na Kuelimisha

Ushawishi wa vyombo vya habari katika maoni yetu ya kufanya mapenzi ni suala ambalo limekuwa liki... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya usalama na faragha katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya usalama na faragha katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya usalama na faragha katika ngono/kufanya mapenzi?

H... Read More

Kuunda Muda na Nafasi ya Ubunifu katika Mahusiano yako

Kuunda Muda na Nafasi ya Ubunifu katika Mahusiano yako

Mahusiano ni muhimu sana katika maisha ya binadamu. Kuunda muda na nafasi ya ubunifu katika mahus... Read More

Mbinu za Kupata Tarehe na Wasichana kwa Mafanikio

Mbinu za Kupata Tarehe na Wasichana kwa Mafanikio

Leo, tunazungumzia mbinu za kupata tarehe na wasichana kwa mafanikio. Kila mtu anataka kuwa na mp... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiimani na mafundisho ya kidini na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiimani na mafundisho ya kidini na mpenzi wako

Kama unapenda mtu wa imani tofauti na wewe, hapa kuna maoni kadhaa ambayo yanaweza kukusaidia kue... Read More

Jinsi ya kusaidiana na mke wako kwenye majukumu ya kifamilia

Jinsi ya kusaidiana na mke wako kwenye majukumu ya kifamilia

Kusaidiana na mke wako kwenye majukumu ya kifamilia ni muhimu katika kujenga usawa na kuimarisha uhu... Read More
Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

  1. Kujenga mahusiano mazuri ya familia ni jambo muhimu katika kuhakikisha kuwa kila mtu an... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha ushirikiano na majirani

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha ushirikiano na majirani

Habari yako mpenzi wangu? Hii leo, napenda kuzungumza nawe kuhusu jinsi ya kusaidiana na majirani... Read More

Njia za Kukuza Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Familia

Njia za Kukuza Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Familia

Njia za Kukuza Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Familia

Katika familia, ushirikian... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujifunza na Kuendeleza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujifunza na Kuendeleza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha ushirikiano wa kujifunza na kuendeleza maarifa katika familia ni muhimu sana kwa maen... Read More

Jinsi ya Kuwa na Muda wa Kutuliza na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Muda wa Kutuliza na Msichana

Kila mwanamume anataka kuwa na muda mzuri wa kutuliza na msichana wake. Lakini, wakati mwingine n... Read More