Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS💌💕
AckyShine

Angalia jinsi maamuzi yako ya jana na ya leo yanavyoweza kukuathiri

Featured Image

By Malisa GJ,
Nimeitoa kwa Comrade Markus Mpangala na kuitafsiri kwa Kiswahili (kisicho rasmi sana).
Mwaka 1998 "Google" walitaka kuiuza kampuni yao kwa "Yahoo" kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.

Mwaka 2002 Yahoo wakagundua kwamba walifanya makosa kuikataa Google kwahiyo wakarudi na kutaka kuinunua kwa dola Bilioni 3 (sawa na Trilioni 6). Lakini Google wakataka wapewe Dola Bilioni 5 (sawa na Trilioni 10). Yahoo wakagoma.

Mwaka 2008 kampuni ya Microsoft ikataka kuinunua Yahoo kwa Dola Bilioni 40 (sawa na Trilioni 80) lakini Yahoo wakakataa offer hiyo. Wakaona ni "ndogo"

Lakini Yahoo ikazidi kuporomoka kwenye soko na ilipofika mwaka 2016 hatimaye ikauzwa kwa dola Bilioni 4.6 (sawa na Trilioni 9) kwa kampuni ya Verizon.

#MyTake:

Unajifunza nini kupitia kisa hiki cha Yahoo? Binafsi nimejifunza mambo kadhaa:

#Mosi ni kuhusu fursa. Ukipata fursa leo itumie huwezi kujua kesho itakuaje. Yahoo wamechezea fursa nyingi sana. Kama wangekua makini huenda wao ndio wangekua wamiliki wa Google leo. Au wangeuzwa kwa bei kubwa (Trilioni 80) kwa Microsoft mwaka 2008. Lakini maringo yao yamewafanya kuja kuiishia kuuzwa bei ya "mbwa" (trilioni 9). Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Pili ni kuhusu Thamani. Ukiwa kwenye nafasi leo usijione una thamani kuliko asiye na nafasi hiyo. Huwezi kujua kesho itakuaje. Maisha ni kupanda na kushuka. Unaweza kumnyanyasa mtu leo kwa sababu una nafasi fulani, kesho ukaenda kuomba kazi ukakuta ndio "boss" anayeajiri. Unayemuona leo yupo chini kesho aweza kuwa juu, na aliye juu akawa chini. Yahoo ilikua juu sana miaka ya 1990's lakini kwa sasa imebaki "skrepa". Hata sijui kama kuna watu wanaitumia siku hizi zaidi ya wale wabibi waliofungua email kipindi kile cha zama za kale za mawe.

Yahoo ilijiona juu kuliko wengine kwahiyo ikadharau kampuni zingine. Hata Google ilipotaka kuuzwa kwa Yahoo mwaka 1998, Yahoo iliona kama vile kuinunua Google ni kupoteza fedha. Leo inatamani kuwa hata "department" ya Google lakini haiwezekani. Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Tatu nimejifunza majuto ni mjukuu. Wamiliki wa Yahoo huenda wanajuta sana kwa kupoteza fursa zote zilizokuja mbele yao. Vivyo hivyo katika maisha kuna maamuzi unaweza kufanya leo kesho ukayajutia. Mwanadada anaweza kukataa kuchumbiwa na kijana kwa sababu hana kazi, hana nyumba wala gari. Lakini baada ya miaka kadhaa anamuona yule kijana amefanikiwa kuliko alivyofikiri. Anatamani awe hata mchepuko wake lakini haiwezekani.
Usifanye makosa ya Yahoo.!

#Nne nimejifunza kuwa ukichagua sana nazi utapata koroma. Yahoo walijifanya kuchagua sana. Kila aliyekuja na "Offer" walikataa. Matokeo yake wakaja kuuzwa bei ya kuku za kienyeji kutoka Singida. Mwaka 2008 Microsoft walitaka kuinunua Yahoo kwa Dola bilioni 40 wakagoma. Lakini miaka 8 baadae (2016) wamekuja kuuzwa Dola bilioni 4.6 (yani 10% ya kile walichokua wapewe mwaka 2008).

Vivyo hivyo na binadamu ndivyo tulivyo. Ngoja nitumie mfano wa akina dada ili unielewe vzr. Kuna kina dada kuringa kwao ni fahari. Sisemi kina dada wasiringe. Ni vizuri kuringa lakini isiwe "too much". Sasa wewe unaringa wanaume zaidi ya 10 waliokuja kukuposa, wote unawakataa unataka uolewe na nani?

Mwenye elimu umemkataa, mwenye gari umemkataa, mwenye nyumba umekataa, mwenye biashara umekataa. Umewakataa wote. Ukija kuhamaki umekuwa kama "Yahoo"… una miaka 35 na huna hata mchumba wa kusingiziwa. Unaanza kwenda kwenye mikesha ya maombi ili upate muujiza. Miaka mitatu inaisha hakuna muujiza wala mazingaombwe.

Unaamua kuweka tangazo gazetini "natafuta mchumba mwenye miaka 40 na kuendelea. Hata kama hana kazi mimi nina kazi tutasaidiana". Miaka miwili inapita hupati. Unagundua ulikosea kama Yahoo. Hakuna mwanaumwe wa miaka 40 ambaye yupo single. Unarekebisha na kusema kuanzia miaka 25, wakati wewe una 40.

Unaamua kujilipua kama Jackline Wolper na Harmonizer. Au Zari na Diamond. Au Wema na Idris. Hujui wakati Wema anachukua taji la Miss Tanzania Idriss alikua form one?? Lakini leo wanamitana mababy?? Kwahiyo unaona miaka 25 kwa 40 sio issue. Na wewe unaamua kuingia kwenye kundi la "akina bibi wanaolea wajukuu zao"

Lakini hupati "husband material". Unawapata "maplay boy" wa mjini. Wanakuja wanakuta ni bibi wa miaka 40 wanakuuliza "umemaliza eddah" wakidhani ni mjane umefiwa na mume unataka kuolewa tena. Kumbe hujawahi kutolewa mahari hata mara moja. Wanakuambia ngoja tufikirie, halafu haoooo wanapotea kama Microsoft ilivyopotea mbele ya uso wa Yahoo. Hawarudi ng'o.

Baadae baba yako anaamua kuondoa tangazo la "Jihadhari mbwa mkali" lililokuwa getini anaweka tangazo jipya "tunauza barafu" Na hapo ndipo utakapogundua kuwa vifusi vya mchanga wa mgodini vinaweza kutumika kupiga "plasta" nyumba yenu.

My dear Life is too short to be complicated. Live your life. Enjoy every moment of your life. Tumia fursa zote muhimu unazozipata. Usiringe. Usimdharau mtu. Heshimu kila mtu. Mche Mungu. Usifanye makosa ya "Yahoo".!

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

FUNZO: Maisha ni kuchagua

FUNZO: Maisha ni kuchagua

Siku hizi kuna tangazo moja la kampuni ya simu za mikononi, Tigo, likimuonesha mama akiwa _busy_ ... Read More

Elimu ya biashara

Elimu ya biashara

Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo... Read More

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..

-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa k... Read More

Angalia jinsi muda wako unavyopotea

Angalia jinsi muda wako unavyopotea

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa mie... Read More

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo

MAHITAJI:

1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.Read More

Kushindwa au vikwazo sio sababu ya kutofanikiwa

Kushindwa au vikwazo sio sababu ya kutofanikiwa

"Nilibakwa nikiwa na miaka 9 lakini leo mimi ni mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani"... Read More

Umasikini isiwe sababu wala utajiri isiwe sababu ya kuwa mchafu au kutokuwa na usafi

Umasikini isiwe sababu wala utajiri isiwe sababu ya kuwa mchafu au kutokuwa na usafi

Katika maisha, umasikini siyo sababu ya mtu kuwa mchafu au kutokuwa na usaf... Read More

Njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha

Njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejenga GHOROFA na yule anayejenga Read More

Mambo ya kufanya mwezi Disemba

Mambo ya kufanya mwezi Disemba

Ikiwa leo ni tarehe **1/12 huwezi amini kuwa hakuna t... Read More

Usiyoyajua kuhusu pesa haya hapa

Usiyoyajua kuhusu pesa haya hapa

Habari za Leo Rafiki yangu wa Muhimu sana. Ni furaha yangu kujua unaendelea vyema sana na majukum... Read More

Kuwa na kawaida ya kujiwekea Akiba ni njia na Siri ya kuwa tajiri

Kuwa na kawaida ya kujiwekea Akiba ni njia na Siri ya kuwa tajiri

Watu wengi wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?” Je ni mbinu gani zin... Read More

Nia yako isishindwe

Nia yako isishindwe

Nimejifunza jambo kubwa sana ambalo sote tuna lijua nalo ni "NIA".
Nimemtazama mwendesha pik... Read More