Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Je, Wewe unayesoma huu ujumbe una ndoto?

Featured Image

KILA mtu duniani ana ndoto ingawa haijalishi ni ndoto gani uliyonayo.
Ndoto uliyonayo ina thamani kubwa kuliko fedha wala kitu chochote kile. Ndoto uliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadilisha maisha yako na kukufikisha sehemu ambayo ulitaka ufike ama zaidi ya pale ulipotarajia kufika.





Ndoto yako inaweza kukupeleka sehemu mbalimbali duniani ukazunguka kufanya mambo yako si kwa sababu una fedha sana, bali ni kwa sababu una ndoto. Ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa kuliko fedha.





Ndoto inaweza kuzaa fedha kwa maana matunda yake yanaweza kuwa fedha, lakini katu fedha haiwezi kuzaa ndoto. Kwa hiyo bais, ndoto ni kubwa kuliko fedha.





Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, mtu maskini kuliko wote duniani ni yule asiyekuwa na ndoto!





Hivyo utakubaliana naye kuwa kila mwenye ndoto ni tajiri na si maskini, maana ana kitu cha thamani, cha pekee na cha tofauti ambacho hakuna mwenye nacho isipokua wewe mwenyewe.





Tatizo kubwa ni kwamba, watu wengi wameua ndoto zao kwa kisingizio cha kukosa fedha lakini wanashindwa kutambua kwamba hakuna fedha inayozidi ndoto isipokuwa ndoto inazidi fedha.





Tatizo lingine ni kwamba, watu wengi hawajui kuwa ndoto zao zina nguvu kubwa kufanikisha maisha yao kijamii, kiuchumi, kisiasa na kila nyanja.





Ndani ya ndoto zako kuna kila kitu unachokitaka ama unachokihitaji – iwe fedha, utajiri, umaarufu, familia nzuri, mume mzuri, mke mzuri, watoto wazuri, kazi nzuri, afya nzuri – hivyo ukiacha kutafuta fedha ukatafuta kutimiza ndoto zako utapata kila kitu ikiwemo utoshelevu na amani ya moyo.





Lakini tatizo lipo kwenye kufanya ndoto zako zitimie na zikuzalie mafanikio. Haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani, kama hutaitimiza ikaja kwenye uhalisia tambua kwamba utakufa maskini ukiwa na utajiri wa ndoto, jambo ambalo linaumiza na linatesa maisha ya watu wengi wanaoishi maisha ya chini tofauti na walivyopaswa wawe.





Ndoto yako ndiyo imebeba kusudi la maisha yako. Kama hutaishi katika ndoto yako maana yake utakuwa hujaishi maisha yako ambayo kwa kiasi kikubwa yapo kwenye ndoto zako.





Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, watu wengi duniani hawaishi, bali wapo tu. Kuna tofauti kati ya kuishi na kuwepo. Kuishi ni kutimiza ndoto zako na ndani ya kusudi la maisha yako, lakini kama hutimizi ndoto hizo uko nje ya kusudi la maisha yako. Wewe utakuwa hauishi bali upo upo tu.





Anaamka asubuhi kwa sababu watu wanaamka. Ukimuuliza kwanini umeamka anasema ni kwa sababu watu wameamka! Hana sababu za msingi. Kataa kuishi bila agenda, bila kuwa na ndoto ambayo kila siku unapiga hatua kuifikia ama uko ndani yake sasa katika kuitimiza na kuifanikisha kwa kiwango cha juu.





Kila kitu kipo kwenye ndoto zako, tafuta kutimiza ndoto zako kuliko kutafuta fedha kwa sababu fedha ni moja kati ya bidhaa iliyomo ndani ya ndoto zako.





Sisemi watu wasitafute fedha, la hasha. Wazitafute, tena kwa bidi, ila wasisahau kutafuta kutimiza ndoto zao na kutumia fedha kama moja kati ya nyenzo za kuwawezesha kutimiza ndoto zao.





Ukweli ni kwamba, fedha daima huwa hazitoshi, hata kama ni nyingi kiasi gani. Kama unabisha waulize matajiri kama wamewahi kuridhika. Lakini katika kutimiza ndoto zako kuna utoshelevu kiasi na kuridhika kiasi fulani (satisfaction) hata kama si kwa asilimia 100.





Mwandishi mashuhuri wa vitabu, Myles Munroe, aliwahi kusema kuwa β€œWatu wenye kusumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo ni wale ambao ndoto zao hazijatokea kwenye uhalisia, zinawasumbua.”





Inawezekana unasumbuka sana kwenye maisha yako kwa sababu hujatimiza ndoto zako, maana ndoto huwa haimwachi mtu akatulia, inampa mahangaiko, mfadhaiko wa kutaifuta.





Kila mtu anapaswa azae, ndoto yako izae, uwezo ulionao uzae. Unaweza kukuzalia mafanikio makubwa, hivyo usikubali kufa na kitu cha thamani kilichoko ndani yako.





Hakuna ndoto kubwa wala ndogo. Fikiria mtu aliyegundua lipstick, leo hii wanawake dunia nzima wanapaka lipstick, si jambo dogo tena.





Hukuja duniani kuwa mtu wa kuhangaikia fedha, inatakiwa fedha ikuhangaikie wewe, ikupende na ikutamani na si wewe utamani fedha.





Tengeneza miundombinu ya fedha na hiyo miundombinu iko kwenye ndoto zako, maono yako, kipaji


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake

BARUA YA BOSI ILIBADILI FIKRA ZANGU KUHUSU PESA KATIKA DAKIKA ZA MWISHO ZA MAISHA YANG... Read More

Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu

Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu

Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku a... Read More

Elimu ya biashara

Elimu ya biashara

Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo... Read More

Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

Tafuta fursa kila kona.
Tumia kipaji chako.
Kuwa na nidhamu katika fed... Read More

Jinsi Muda Unavyopotea, Jifunze kitu hapa

Jinsi Muda Unavyopotea, Jifunze kitu hapa

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa mie... Read More

Ushauri wangu kwa leo

Ushauri wangu kwa leo

Kuna watu wengi sana huwa wanani-challenge ninaposema kwamba ni muhimu sana mtu kuishi katika kus... Read More

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hu... Read More

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana... Read More

Ugumu wa maisha huanzia akilini mwako

Ugumu wa maisha huanzia akilini mwako

Ebu fikiria Dada anayechoma mahindi maeneo ya Manzese Darajani kuanzia saa 12 jioni mpaka SAA 2 u... Read More

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..

-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa k... Read More

Kwa nini watu wanapenda pesa

Kwa nini watu wanapenda pesa

Watu wengi tunapenda sana Pesa lakini hatuko tayari kuzifanyia Pesa kazi nikiwa na maana kutumia ... Read More

Kushindwa au vikwazo sio sababu ya kutofanikiwa

Kushindwa au vikwazo sio sababu ya kutofanikiwa

"Nilibakwa nikiwa na miaka 9 lakini leo mimi ni mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa duniani"... Read More