Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS💌💕
AckyShine

Nifanye nini ili kuepuka kubakwa na mpenzi/ rafiki?

Featured Image
Kuna baadhi ya vidokezo ambavyo vinaweza kukusaidia:
1. Usikae faragha na mwenzi wako kabla hujawa tayari na kumwamini. Ongozana na marafiki wengine hasa mwanzoni mwa urafiki wenu. Msitoke tu nyie wawili hadi hapo utakapojisikia kuwa umemjua kiasi cha kumwelewa na kumwamini. Pia jiepushe kukaa sehemu za faragha naye.

2. Kama utatoka naye, hakikisha kuwa kuna mtu anayejua mnakokwenda na ni muda gani unakusudia kurudi nyumbani. Ikiwezekana kuwa na namba ya simu ya mmoja kati ya rafiki zako. Hii itakusaidia kama ikijitokeza hali ya kutaka msaada.
3. Usikubali yeye alipe gharama zote. Ni vizuri kugawa gharama hizo kati yenu. Kama mtakwenda kwenye tamasha au kupata kinywaji hakikisha kulipia nusu ya hizo gharama. Ukifanya hivyo utamzuia mwenzio mawazo ya kukufikiria “kuwa anakudai ngono“ kama malipo ya pesa yake aliyotumia.
4. Ni vizuri kutafakari na kuweka kichwani kabla ya kwenda naye popote juu ya nini unachotaka na kile usichotaka kitokee.
5. Onyesha wazi kuwa unaposema “hapana“ unamaanisha “hapana“ usimpe nafasi ya kuchukulia hiyo “hapana“ kuwa ndiyo.
6. Amini hisia zako. Kama unaona unalazimishwa usisite kueleza maoni yako / unavyojisikia. Ikibidi ondoka sehemu hiyo.
AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Ninaweza kupata mimba wakati nipo kwenye hedhi?

Ninaweza kupata mimba wakati nipo kwenye hedhi?

Ili mwanamke aweze kushika mimba, i inabidi yai lililopevuka likutane na mbegu za kiume. Yai pevu... Read More

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Mwili wa mwanaume unatengeneza aina mbili za mbegu. Kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kiume na k... Read More

Je, watu wanasemaje kuhusu kutumia manjonjo na manukato wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanasemaje kuhusu kutumia manjonjo na manukato wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Kutumia manjonjo na manukato wakati wa ngono/kufanya mapenzi ni mada ambayo ina debate kubwa. Wap... Read More

Je, nini imani ya watu katika kuelewa na kuheshimu mchakato wa uponyaji wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, nini imani ya watu katika kuelewa na kuheshimu mchakato wa uponyaji wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, umewahi kufikiria jinsi watu wanavyoelewa na kuheshimu mchakato wa uponyaji wakati wa ngono a... Read More

Je , vipimo vya Virusi vya UKIMWI vinasema ukweli?

Je , vipimo vya Virusi vya UKIMWI vinasema ukweli?

Uwezekano wa kupata majibu ya uwongo ni mdogo sana, isipokuwa tu kama vipimo vitafanyika kipindi ... Read More

Umri wa kuanza kutumia njia za uzazi wa mpango

Umri wa kuanza kutumia njia za uzazi wa mpango

Muda unaofaa kutumia njia ya kupanga uzazi ni wakati unapojamiiana kwa mara ya kwanza. Huu ni wak... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Heshima kwa Msichana Wako

Wanawake ni vipenzi vya thamani sana katika m... Read More

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya kawaida au ngono/kufanya mapenzi ya kufanya mazoezi ya kimwili?

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya kawaida au ngono/kufanya mapenzi ya kufanya mazoezi ya kimwili?

Habari rafiki! Karibu katika makala hii ambayo itakupa mwanga kuhusu kile watu wanapendelea kati ... Read More

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Mwili wa mwanaume unatengeneza aina mbili za mbegu. Kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kiume na k... Read More

Je, ni matatizo yapi yanayotokana na ujauzito katika umri mkubwa?

Je, ni matatizo yapi yanayotokana na ujauzito katika umri mkubwa?

Kwa wanawake wenye miaka zaidi ya 35 uwezekano wa kupata matatizo ya kiafya wakati wa ujauzito au... Read More

Watu wanaoua Albino wanapata faida gani?

Watu wanaoua Albino wanapata faida gani?

Hakuna uchunguzi wa kisayansi ambao umeonyesha faida
yoyote inayopatikana kwa kuua Albino.Read More

Je, ni madhara gani atapata mama mjamzito endapo atajamiiana na mwenzi wake?

Je, ni madhara gani atapata mama mjamzito endapo atajamiiana na mwenzi wake?

Kama kati ya mwanamke na mwanaume hakuna mwenye magonjwa ya zinaa, hakuna madhara yoyote kwa mwan... Read More