Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Matatizo yanayotokana na ujauzito katika umri mdogo

Featured Image

Wataalamu wanashauri kwamba msichana anastahili kuanza kubeba mimba kuanzia umri wa miaka 18 hadi 20. Kabla ya umri huu, mwili wa msichana bado haujakomaa vizuri. Viungo vya uzazi bado ni vidogo na ngozi ni laini. Vilevile mfupa wa nyonga bado mwembamba kiasi cha kumwezesha mtoto kupitia wakati wa kuzaliwa.
Wasichana chini ya miaka 18 wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo, hasa wakati wa kujifungua. Matatizo hayo ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa juu, kuumwa uchungu kwa muda mrefu, kukwama kwa mtoto, kujifungua kwa njia ya operesheni, kujifungua kabla ya wakati na watoto kuzaliwa na uzito mdogo. Mwili huwa na mahitaji makubwa wakati wa ujauzito na kujifungua na mwili wa wasichana wenye umri chini ya miaka 18 huwa haujakomaa vya kutosha kwa kazi ya kubeba mimba.
Mbali ya shida za kiafya, kuna matatizo mengine yatokanayo na kupata mimba mapema. Mara nyingi msichana na mwenzie wanakuwa bado wanasoma shule, msichana hufukuzwa shule na hata hutengwa katika jamii . Vijana mara nyingi hawana mapato ya kumlea na kumtunza mtoto, na mahali pa kuishi huwa hawana. Vilevile mvulana mara nyingi hayuko tayari kuchukua jukumu la kuwa baba. Kwa sababu hizi zote, ni vizuri zaidi mimba zitungwe baada ya msichana kufikia umri wa miaka 18.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Watu husema bia hukufanya uwe mnene, je, ni kweli?

Watu husema bia hukufanya uwe mnene, je, ni kweli?

Ni kweli kwamba baadhi ya pombe, hasa bia, husababisha
ongezeko la uzito kwa baadhi ya watu ... Read More

Njia za Kumshtua Msichana kwa Tarehe ya Kwanza

Njia za Kumshtua Msichana kwa Tarehe ya Kwanza

Hakuna kitu kizuri kama kukutana na msichana unayempenda kwa tarehe ya kwanza. Lakini, unapotaman... Read More

Haki za ujinsia na afya ya uzazi zinamhusu pia mtu anayeishi na ualbino?

Haki za ujinsia na afya ya uzazi zinamhusu pia mtu anayeishi na ualbino?

Haki za msingi; hasa zile zinazohusiana na kuthaminiwa na
kuheshimiwa kama binadamu zinawahu... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Tarehe ya Kimapenzi na Msichana

Kama wewe ni miongoni mwa wanaume wanaotaka kuwa na tarehe ya kimapenzi na msichana, kuna vidokez... Read More

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aone Thamani Yako

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aone Thamani Yako

Vidokezo vya Kufanya Msichana Aone Thamani Yako

Mara nyingi, kama wanaume, tunataka kuonye... Read More

Njia za Kujenga Mazingira ya Kuaminika katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kujenga Mazingira ya Kuaminika katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kujenga Mazingira ya Kuaminika katika Uhusiano wako na Msichana

Kamwe hufai kuhisi... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Ukarimu kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Ukarimu kwa Msichana Wako

Habari za leo! Leo nataka kuzungumza juu ya jinsi ya kuonyesha ukarimu kwa msichana wako. Kama mw... Read More

Umri unaofaa kuoa

Umri unaofaa kuoa

Kuoana maana yake ni kuwajibika kwa maisha yako na mke au mume wako. Mara nyingi kuoana kunaambatana... Read More
Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Kuna sababu kuu mbili i kwa wana ndoa kupata maambukizi i ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Kw... Read More

Jinsi ya Kujikinga na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende

Jinsi ya Kujikinga na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende

Jinsi ya Kujikinga na Maambukizi ya Kisonono na Kaswende 🌟

Karibu sana kwenye makala hi... Read More

Ndoa ya kulazimishwa

Ndoa ya kulazimishwa

Ndoa ya kulazimishwa ni ile ambayo mwanamume au mwanamke
anaozwa bila yeye mwenyewe kukubali... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano Mazuri ya Simu na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano Mazuri ya Simu na Msichana

Kama una nia ya kuimarisha uhusiano wako na msichana, ni muhimu kuwa na mawasiliano mazuri ya sim... Read More