Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ukeketaji ni nini?

Featured Image

Katika baadhi za jamii viungo vya uzazi vya nje vya msichana,
yaani kisimi au sehemu ya ndani na nje ya mashavu ya uke
yanakatwa na kuondolewa kabisa. Huu ndiyo ukeketaji au
kutahiriwa kwa mwanamke.
Wakati mwingine uekeketaji hufanyika katika umri wa miezi ya
mwanzo ya maisha ya mtoto wa kike. Mara kwa mara kutahiriwa
kwa wanawake hufanyika wakati msichana anapofikia utu uzima
au kuadhimisha na kuvuka kutoka utoto kuingia utu uzima.
Mara nyingine ukeketaji ni sehemu ya unyago na kuadhimia kwa
msichana kujifunza jinsi ya kuwa mtu mzima.
Kuna aina mbalimbali za ukeketaji:
1 Sehemu ya ngozi inayofunika kisimi huwa inaondolewa.
Mara nyingine kisimi au eneo lake hukatwa pia. Watu
wengi huita aina hii sunna.
2 Kisimi pamoja na sehemu za mashavu ya ndani
hutolewa.
3 Sehemu yote au baadhi ya viungo vya nje hutolewa na
uke hufungwa kwa kushona. Hii huacha sehemu ndogo
ya tundu ambapo mkojo na damu ya mwezi (hedhi)
hupita. Aina hii huitwa mfyato (Infibulation).
4 Aina yeyote ya kuchezea kwa lengo la kuharibu
sehemu yoyote ya viungo vya nje kama vile kutia vitu
vyenye madhara kwenye uke, kurefusha mashavu au
kisimi kwa kuvivuta au kutoboatoboa.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsia ya mtoto angali mimba

Jinsia ya mtoto angali mimba

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Mwili wa mwanaume unatengeneza aina mbili za... Read More

Je, sigara ni sumu kwa binadamu?

Je, sigara ni sumu kwa binadamu?

Ndiyo. Nikotini iliyo kwenye tumbaku ni sumu. Ukiwa na kiwango kikubwa cha nikotini katika damu utaj... Read More
Kwa nini watu wanakuwa na hulka ya kuua Albino?

Kwa nini watu wanakuwa na hulka ya kuua Albino?

Vitendo vya kuua Albino tunavyovishuhudia sasa ni mambo
mapya na kwa kila hali siyo njia sah... Read More

Ubikira ni nini?

Ubikira ni nini?

Maana halisi ya neno β€œbikira” ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kabisa kujamii ana. Kuj... Read More

Njia za Kujenga Uwezo wa Kusamehe na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Uwezo wa Kusamehe na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Uwezo wa Kusamehe na Msichana katika Uhusiano

Uhusiano ni kitu kizuri sana... Read More

Vidokezo vya Kufanya Msichana Ahisi Anapendwa na Kuthaminiwa

Vidokezo vya Kufanya Msichana Ahisi Anapendwa na Kuthaminiwa

Habari za asubuhi wapendwa! Leo, tutajadili vidokezo muhimu ambavyo vitamsaidia msichana ahisi an... Read More

Jinsi ya Kuvutia Wasichana: Vidokezo vya Kuchumbiana na Wasichana

Jinsi ya Kuvutia Wasichana: Vidokezo vya Kuchumbiana na Wasichana

Jambo rafiki yangu! Katika maisha ya kila siku, tunakutana na wasichana wengi ambao tunapenda kuw... Read More

Je, kwa nini unasema kwamba wasichana vijana hawapo tayari kubeba mimba?

Je, kwa nini unasema kwamba wasichana vijana hawapo tayari kubeba mimba?

Ni kweli kwamba kupata hedhi ni dalili ya mwili wa msichana kuwa tayari kwa kubeba mimba, lakini ... Read More

Kwa nini watu wanakunywa pombe?

Kwa nini watu wanakunywa pombe?

Unywaji wa pombe ni sehemu ya utamaduni wa Tanzania na nchi
nyinginezo duniani.

Watu h... Read More

Sheria kuhusu kufanya punyeto

Sheria kuhusu kufanya punyeto

Punyeto ni kupapasa au kusugua kiungo cha uzazi ili uweze kupata
starehe. Hakuna kosa kwa te... Read More

Je, ni matatizo yapi yanayotokana na ujauzito katika umri mkubwa?

Je, ni matatizo yapi yanayotokana na ujauzito katika umri mkubwa?

Kwa wanawake wenye miaka zaidi ya 35 uwezekano wa kupata matatizo ya kiafya wakati wa ujauzito au... Read More

Je, Ni Vipi naweza Kupata Msaada au Elimu kuhusu Ngono?

Je, Ni Vipi naweza Kupata Msaada au Elimu kuhusu Ngono?

Je, ni vipi naweza kupata msaada au elimu kuhusu ngono? πŸ€”πŸ“š

Wewe kama kijana mzuri na... Read More