Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

ATHARI ZA ULEVI KATIKA JAMII

Featured Image
Watu wanokunywa kupitia kiasi huathiri jamii kwa njia
mbalimbali. Madhara mengine hutokea kwa kuwa wanafanya
vitu ambavyo wasingevifanya iwapo wasingekuwa wamelewa.

Watu wakilewa, huweza kuwa na hasira, wagomvi hivyo basi
huwadhuru wengi kiakili na kimwili. Isitoshe, ajali nyingi za
kazini na barabarani hutokea watu wakiwa wamelewa. Mara
nyingi watu wasiokuwa na hatia na vilema hupoteza maisha yao
kutokana na ajali zinazohusiana na ulevi.

Watu wanaokunywa
pombe kupita kiasi hupunguza uangalifu na hivyo basi kuchangia
katika kuenea kwa VVU kwenye jamii. Watu wanaokunywa pombe
wanaweza pia kufanya ujambazi katika jamii. Pia wanaokunywa
kupita kiasi si wafanyakazi wa kutegemewa kwani hutumia
muda mwingi nje ya sehemu zao za kazi.

Watu waliozoea kunywa pombe nyingi hupoteza pesa zao nyingi
kununua pombe na muda wao mwingi kufikiria jinsi ya kupata
pesa za kunywea pombe.

Kutokana na gharama za kununua
pombe familia zao hukosa pesa za vitu muhimu kama kodi ya
nyumba, ada na sare za shule na chakula.

Vijana wanaokunywa pombe huanza kuiba pesa nyumbani kwao
ili kununulia pombe. Matumizi mabaya ya pombe mara nyingi
husababisha matatizo au kuvunjika kwa familia, au urafiki.

Vilevile husababisha matokeo mabaya shuleni au kuacha kabisa
shule, hali ambayo inaweza kusababisha kukosa nafasi za kazi,
kujitegemea wewe mwenyewe na kusaidia famila yako na jamii.
AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna madhara gani kama mtu anakaa muda mrefu bila kujamiiana au kufanya mapenzi?

Je, kuna madhara gani kama mtu anakaa muda mrefu bila kujamiiana au kufanya mapenzi?

Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya iwapo utakaa muda mrefu bila ya kujamiiana. Viungo ... Read More
Jinsi ya Kuwa na Mvuto wa Kipekee kwa Msichana

Jinsi ya Kuwa na Mvuto wa Kipekee kwa Msichana

Kila mtu anataka kuwa na mvuto wa kipekee kwa msichana. Lakini je, unajua jinsi ya kuwa na mvuto ... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Kinga (Condom)

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Kinga (Condom)

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Kinga (Condom) 😊🌺

Karibu kweny... Read More

Je, watumiaji wa dawa za kulevya wanaweza kupata watoto?

Je, watumiaji wa dawa za kulevya wanaweza kupata watoto?

Ndiyo, hii i ii inawezekana. Lakini ujue kwamba watu wanaotumia dawa za kulevya huwa dhaifu kisai... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia muda mwingi katika mchezo wa hatua wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia muda mwingi katika mchezo wa hatua wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako rafiki, leo tutajadili kuhusu swali linaloulizwa sana kuhusu watu kwa nini wanapendel... Read More

Nina rafiki wa kike ambae ni Albino wa ngozi na tunapendana sana, lakini kwa nini anakataa kujamiiana na mimi?

Nina rafiki wa kike ambae ni Albino wa ngozi na tunapendana sana, lakini kwa nini anakataa kujamiiana na mimi?

Rafiki yako wa kike ana haki ya kukataa kujamiiana na wewe.
Labda hayuko tayari kujamiiana a... Read More

Vidokezo vya Kutafuta Tarehe ya Muda Mrefu na Msichana

Vidokezo vya Kutafuta Tarehe ya Muda Mrefu na Msichana

Leo hii tutazungumzia kuhusu masuala ya kutafuta tarehe ya muda mrefu na msichana. Inawezekana um... Read More

Je, nikitoa au kupata damu hospitalini, itakuwepo hatari ya kupata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Je, nikitoa au kupata damu hospitalini, itakuwepo hatari ya kupata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Katika swali hili lazima tutofautishe kati ya kutoa damu na kuwekewa damu. Kutoa damu hakuleti ha... Read More

Je, unaweza kupanga kuzaa aina ya watoto, yaani wa kiume au wa kike tu?

Je, unaweza kupanga kuzaa aina ya watoto, yaani wa kiume au wa kike tu?

Mimba i inatungwa wakati yai la kike linaporutubishwa na mbegu za kiume. Kama tulivyoona hapo juu... Read More

Utoaji wa zawadi kwa kubadilishana na kujamiiana

Utoaji wa zawadi kwa kubadilishana na kujamiiana

Kutoa zawadi kwa mtu kwa kubadilishana ili kujamiiana
ni unyanyasaji mbaya. Iwapo mpokeaji w... Read More

Ukubwa wa kondomu

Ukubwa wa kondomu

Kuna aina kondomu za ukubwa mbalimbali. Kwa wastani ukubwa wa kondomu unafaa kwa wanaume watu waz... Read More

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto bila matatizo?

Ulemavu wa watu wanaoishi na ualbino hauingiliani na uwezo
wa kuweza kuzaa. Tuelewe kwamba u... Read More