Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS💌💕
AckyShine

Madhara ya kubana mkojo muda mrefu

Featured Image

Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature’s call.

Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini, akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili. Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo umenibana kweli, ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi ndivyo watu wengi wanafanya.

Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia, kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo, mkojo unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa. Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili (Receptors) vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia au kimejaa, baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo, ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kuikaza misuli maalumu (Sphincters) mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.

Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe yaani, automatic, kitendo cha mtu kupuuzia kwenda kukojoa husababisha Ubongo upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwa kuwa Ubongo nao hutuma taarifa katika kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi uwezo wa ubongo kutoa taarifa hizi na pia uwezo wa vigunduzi asili (Receptors) vilivyoko katika kibofu cha mkojo kupoteza uwezo wake tena wa kufanya kazi hizo au uwezo kuwa mdogo. Matokeo yake ni mtu siku kweli anahitajika kuvumilia kidogo ili afike sehemu inayostahihi kujisaidia, lakini hawezi tena na kujikuta muda mdogo tu….mtu tayari kaloanisha nguo yake.

Mpenzi msomaji, mtu kujibana na kupuuzia kwenda kukojoa husababisha uwezo wa kibofu cha mkojo kujitawala (control) upotee. Pia kama uwezo wa neva zinazopeleka taarifa kwenye ubongo kuhusu mabadiliko/ujazo wa kibofu cha mkojo zitaharibika, basi misuli maalumu ya kubana mkojo (sphincter) itashindwa kuachia na matokeo yake mtu ataendelea kukaa na mkojo katika kibofu chake kwa muda mwingi zaidi kitu ambacho ni hatari kwa afya yake. Endapo mkojo huu utashindwa kutoka, utatengeneza mazalia ya bakteria na kukusababishia magonjwa ya kibofu (bladder infection). Magonjwa ya kibofu cha mkojo ni pamoja na U.T.I (Urinary Tract Infections), pia huweza kusababisha magonjwa ya figo na mchafuko wa damu, bacteremia.

Kuna hali huwa inajitokeza kwa baadhi ya watu, yawezekana alikuwa kabanwa na mkojo au alikuwa hajahisi kwenda kukojoa, ila akinywa maji au akisikia sauti ya maji yanachuluzika mfano maji yakitoka bombani, basi atahisi kwenda kukojoa.

Mpenzi msomaji, ni vyema tukawa wasikivu pale mtu unapobanwa na mkojo, hii ni kwa ajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwa ajili ya afya yako kwa ujumla. Kama unalo tatizo, usisite kuonana na wataalamu wa afya.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Aina ya vyakula vinavyotakiwa kwa wajawazito

Aina ya vyakula vinavyotakiwa kwa wajawazito

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na ... Read More

UJUE NA UFAHAMU MFUMO WA MOYO (CARDIOVASCULAR SYSTEM)

UJUE NA UFAHAMU MFUMO WA MOYO (CARDIOVASCULAR SYSTEM)

Mfumo huu wa moyo una kazi zifuatazo:-

👉kupampu damu Mwilini pia kusafirisha gas, taka n... Read More

Madhara ya kunywa soda

Madhara ya kunywa soda

Tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dum... Read More

Faida 10 za kula tende kiafya

Faida 10 za kula tende kiafya

Kila wakati unashauriwa na watalam wa afya ya kwamba unatakiwa kula tende kwa wingi ili kupata fa... Read More

Faida za ulaji wa Peasi

Faida za ulaji wa Peasi

Peasi ni tunda ambalo limekuwa halithaminiwi licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binada... Read More

Madhara ya kutumia dawa za kuzuia mimba wakati wa hatari

Madhara ya kutumia dawa za kuzuia mimba wakati wa hatari

Watu wengi hasa vijana watakuwa wanafahamu dawa ambazo hutumiwa sana kuzuia ujauzito pale ambapo ... Read More

Faida za kiafya za Kula Matunda

Faida za kiafya za Kula Matunda

Matunda yote yana faida mwilini kiafya lakini matunda yanatofautiana kifaida. Zifuatazo ni faida ... Read More

Madhara ya dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu

Madhara ya dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu

Dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu zimetengenezwa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanao... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia mvuke

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia mvuke

Mvuke husaidia kusafisha ngozi. Ni rahisi sana kutumia mvuke kutibu chunusi.

Chemsha maji k... Read More

Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu w... Read More

Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*
*1.Usichelewe kwenda HAJA.* Kutunza... Read More

Faida za kula uyoga kiafya

Faida za kula uyoga kiafya

Uyoga una vitamini na aina nyingi na madini. Virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo kwenye uyoga n... Read More