Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kufurahia Safari ya Kipekee ya Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kufurahia Safari ya Kipekee ya Ndoa na mke wako

Kufurahia safari ya kipekee ya ndoa na mke wako ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wenu na kujenga... Read More
Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Mahusiano ni s... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kusawazisha Majukumu na Kupanga Ratiba katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Kusawazisha Majukumu na Kupanga Ratiba katika Familia Yako

Hakuna jambo bora kuliko kuwa na familia yenye maadili, mshikamano, na usawa. Kuweka kipaumbele c... Read More

Jinsi ya Kupenda na Kuthamini Ndugu: Kuonyesha Upendo katika Neno na Matendo

Jinsi ya Kupenda na Kuthamini Ndugu: Kuonyesha Upendo katika Neno na Matendo

Upendo na heshima ni muhimu katika familia, na ndugu zetu ni watu muhimu sana kwetu. Kupenda na k... Read More

Jinsi ya Kuishi kwa Furaha katika Familia: Kupenda, Kusamehe, na Kuwa na Shukrani

Jinsi ya Kuishi kwa Furaha katika Familia: Kupenda, Kusamehe, na Kuwa na Shukrani

Karibu katika makala hii kuhusu jinsi ya kuishi kwa furaha katika familia. Familia ni kila kitu k... Read More

Jinsi ya Kuimarisha Maisha ya Kiroho katika Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuimarisha Maisha ya Kiroho katika Ndoa na mke wako

Kuimarisha maisha ya kiroho katika ndoa na mke wako ni muhimu katika kukuza uhusiano wenu na kuweka ... Read More
Jinsi ya Kusimamia Majukumu ya Kazi na Familia: Kujenga Usawa na Ufanisi

Jinsi ya Kusimamia Majukumu ya Kazi na Familia: Kujenga Usawa na Ufanisi

Jinsi ya Kusimamia Majukumu ya Kazi na Familia: Kujenga Usawa na Ufanisi

Hivi karibuni, ma... Read More

Njia za Kujenga Heshima na Usawa katika Kufanya Mapenzi: Kupigania Mahusiano ya Kijinsia yenye Afya

Njia za Kujenga Heshima na Usawa katika Kufanya Mapenzi: Kupigania Mahusiano ya Kijinsia yenye Afya

Mapenzi ni sehemu muhimu sana ya maisha yetu, lakini wakati mwingine yanaweza kuwa magumu kuyashu... Read More

Je, kuna umuhimu wa ngono/kufanya mapenzi unabadilika wakati wa mzunguko wa maisha?

Je, kuna umuhimu wa ngono/kufanya mapenzi unabadilika wakati wa mzunguko wa maisha?

Habari za leo wapenzi wangu! Nami nina furaha sana kuwa hapa leo kuongelea kuhusu swala la ngono ... Read More

Jinsi ya Kukuza Ushirikiano na Mazungumzo ya Kina katika Familia

Jinsi ya Kukuza Ushirikiano na Mazungumzo ya Kina katika Familia

Karibu kwenye makala hii ya Jinsi ya Kukuza Ushirikiano na Mazungumzo ya Kina katika Familia. Fam... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kufanya maamuzi muhimu kuhusu mipango ya maisha ya baadaye

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kufanya maamuzi muhimu kuhusu mipango ya maisha ya baadaye

Jinsi ya Kusaidiana na Mpenzi wako katika Kufanya Maamuzi Muhimu Kuhusu Mipango ya Maisha ya Baad... Read More

Kuhamasisha Kujitambua na Kujielewa katika Mahusiano

Kuhamasisha Kujitambua na Kujielewa katika Mahusiano

  1. Kujitambua na Kujielewa ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Kujitambua kunamaanisha ... Read More