Ujumbe mzuri wa SMS wa kumfariji mpenzi wako maisha yake yanapokuwa magumu
Updated at: 2024-05-25 15:36:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Furaha yangu kubwa ni kuliona tabasamu lako, kujua uko na furaha, na kuhisi upendo wako. Najua kuwa maisha mara nyingine huwa ni makatili, na hiyo ni sababu niko hapa kukuonyesha kuwa maisha yanaweza kuwa mazuri kama kuna mtu anayekujali.
Ujumbe wa meseji wa kumsihi mpenzi wako mdumishe mapenzi yenu
Updated at: 2024-05-25 15:25:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi inapopatika si busara kuichezea tudumishe penzi letu laazizi wangu.
Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka. Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika. Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka. Kitale katikati yake ukila utaridhika.
Updated at: 2024-05-25 15:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka. Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika. Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka. Kitale katikati yake ukila utaridhika. Matamu na maji yake hukata kiu haraka. Weupe watui lake lina ladha ukipika. Kupaka mafuta yake mwili hulainika. Na kwenye machicha yake kazi nying hufanyika. Hata na upepo wake uvumapo utacheka. Sikijui kitu chake kipi kisichotumika.usiku mwema
Ujumbe mzuri wa SMS wa usiku mwema kwa mpenzi wako umpendaye
Mungu akubariki uwe mwiz wa ujuzi na maarifa, mlafi wa kushauri, mroho wa busara, mchoyo wa matusi, mlevi wa upendo na kiherehere cha kuabudu.
Updated at: 2024-05-25 15:37:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mungu akubariki uwe mwiz wa ujuzi na maarifa, mlafi wa kushauri, mroho wa busara, mchoyo wa matusi, mlevi wa upendo na kiherehere cha kuabudu.say Amen! Ucku mwema mpenzi
SMS ya mapenzi ya mahaba kwa mpenzi wako aliyeko mbali
Updated at: 2024-05-25 15:25:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna bahari kati yetu. Misitu na milima inatutenganisha, mimi si ‘Supamani’ lakini nipe sekunde moja nitavuka nchi nyingi kukutumia mapenzi yangu. Umeipata hiyo? Pokea mapenzi yangu japo uko mbali.
SMS ya kumsisitiza mpenzi wako asiende kwa mwingine
Updated at: 2024-05-25 15:26:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
chekecho la huba ,toka uvunguni mwa moyo wangu navika moyo wako taji la upendo,na kupulizia marashi ya hubaa ,usimpe mwingine mi ndiye ninayejua kulea.