SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye
Updated at: 2024-05-25 15:36:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
SMS ya mapenzi kutakia maisha marefu siku ya kuzaliwa au birthday
Updated at: 2024-05-25 15:26:21 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi, pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi, nakupenda la azizi.
Updated at: 2024-05-25 15:36:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako Safarini nitajenga hekalu la pendo letu Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako Na mwanzo wa sherehe ya ndoa yetu
Ujumbe wa kumsifia mpenzi wako kumwambia kuwa hakuna anayemfikia yeye
Updated at: 2024-05-25 15:26:31 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Baadhi ya watu huzaliwa na vipaji. Huweza kufanya mambo mazuri kwa ujuzi wao, lakini hamna anayekufikia wewe, kwani ukinisogelea tu kila kitu huwa kizuri.
Updated at: 2024-05-25 15:36:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Katika maisha nimejifunza mambo mengi ikiwemo,. Kupendwa, kupenda, kusamehe, kuvumilia, lakini nimeshindwa kujifunza kukusahau wewe kwa sababu umekuwa ukinikumbuka sana.. nakutakia ASUBUHI NJEMA