Updated at: 2024-09-03 07:51:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ikiwa penzi langu kwako litakufa halitazikwa,ikiwa moyo wangu ni mwandiko hautafutika na kama dhati yangu ni machozi daima hayatokauka na wewe kwangu ni damu ngozini haitochuruzika ila mishipani… .
Updated at: 2024-05-25 15:27:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ama baada ya salamu, mimi ni mzima wa afya njema. Mie ni ndege nipo angani na nimetafuta mti wa kutua kila pembe ya dunia lakini sijaupata bado. Je naweza nikatua kwako?
SMS nzuri ya kumtumia mpenzi wako aliyekuacha kumuomba akurudie
Updated at: 2024-05-25 15:22:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
ni bora mnara ukitikisika kuliko kupata pengo lisilozibika moyoni umeniachia jeraha lisilotibika na ufa usiozibika.rudi mpenzi unautesa mtima wa moyo wangu.
Updated at: 2024-05-25 15:36:18 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje. Hodiiiiii, Hodiiiii, Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.
Updated at: 2024-05-25 15:24:52 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
nimetuma ndege wangu auzunguke ''moyo'' wako kwa '' upendo '' auguse ''uso'' wako kwa ''faraja'' na mwisho akunong'oneze sikioni taratibu kuwa nakupenda.