Updated at: 2024-05-25 15:26:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nakutakia kila la kheri katika maisha yako ya ndoa,wengi watakuambia maneno kila kukicha,lakini nakuambia wapo ambao kwa hakika watakaokuwa wamelenga kutia doa ndoa yako ,rafiki yangu kipenzi kwani wengi waitamani ndoa lakini hawajapata wa kuwaowa
Updated at: 2024-05-25 15:22:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mapenzi ni matamu napia yana raha, wewe hauni ishi hamu, siku zote wanipa raha, wewe kwangu ni mtu muhimu, unaeng'aa moyoni mwangu kama nyota ya jaha. "NAKUOMBA USINIACHE MPENZI WANGU"
SMS ya kumtumia mpenzi wako kumuahidi kuendelea kumpenda daima
Updated at: 2024-05-25 15:22:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo! "NAKUPENDA MALAIKA WANGU"
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako
Safarini nitajenga hekalu la pendo letu
Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako
Updated at: 2024-05-25 15:37:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako Safarini nitajenga hekalu la pendo letu Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako Na mwanzo wa sherehe ya ndoa yetu
Updated at: 2024-05-25 15:26:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Salamu yako ni nusu ya uhai wangu, kuikosa nisawa na kuidhulumu nafsi yangu, kuipata nisawa na ua ridi machoni mwangu, nakila ninapoipata huwa najisikia faraja moyoni mwangu, Nakupenda sana Muhibu wangu.
Updated at: 2024-05-25 15:27:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi
Updated at: 2024-05-25 15:25:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nakupenda sana mwandani wangu ndiyo maana moyo wangu hupatwa kidonda ninaokuona na mwingine hasa anapokuwa hana sifa, nahisi kama anakutumia wewe kama mdori wake wa kumfurahisha. Uwe makini ua la moyo wangu.
Ujumbe mzuri wa kumwambia mpenzi wako kuwa yeye tuu mdiye kakutawala
Updated at: 2024-05-25 15:36:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.