Updated at: 2024-05-25 17:53:18 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.
Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!
Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsAppโฆ!
_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang'oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._
โ
_*Kisha nikaituma ile message*_
Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yakeโฆ Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.
*Akatuma message akiniulizaโฆ*
_Hao wanawake unawajuwa, โฆmume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweliโฆ!_
Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaaโฆ!
Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaaโฆ! Akaniandikia message nyingineโฆ.
*โฆNakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupeโฆ Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuriโฆ!*
Nami nikamjibuโฆ
_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipoโฆ!_
Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdaiโฆ!
Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaaโฆ. Kama sio mie!