Binti:Β Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.
Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.
Updated at: 2024-05-25 16:58:28 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jumapili baada ya kutoka KANISANI, Pastor akaona simu yangu niliyonunua LAKI 5,akaniuliza hiyo simu umenunua Bei gani?
Kwakuwa natoaga sadaka kidogo,na ZAKA ndo sijawahi kutoa,Nikamjibu nimenunua JANA,ELFU 50, akanipa LAKI MOJA,nikanunue mbili,yake na ya mke wake. Sa najaribu kumuuliza Mungu,kwanini kaamua kuniadhibu mbele ya mchungaji bila hata kunionya!
Updated at: 2024-05-25 17:46:22 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtalii: Do you have vegetables here. Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa. Waiter: Vijimeza vidogo hatuna. Mtafsiri: No sir, they don't have. Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs. Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto. Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa. Mtafsiri: They don't cook here Mtalii: What type of snacks do you have here. Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa, Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao. Mtafsiri: They don't cook any type of snacks here, maybe you can go back and eat at home. Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice. Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo. Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena sasa hivi kabla sijakasirika. Mtafsiri: Lets get out of here ππππππ Usicheke pekeyako
Je, hii ni kweli kwa wale wasichana wasiojibu meseji WhatsApp!!!?
Updated at: 2024-05-25 16:56:10 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukiona hivyo ujue ndio hivi
Mwanaume mwenzangu ukiona unamtext msg msichana WhatsApp kaisoma hajajibu, umetuma ya pili kasoma hajajibu, ukatuma ya tatu hajajibu mmmmmhπ¨π¨ hapo ujue mwenzio kaangalia kwenye profile yako, kakagua picha weee mwishoni akajisemea tuΒ "Huyu.mkaka hapana kwa kweli"π€£π€£π€£π€£π€£π€£
Updated at: 2024-05-25 17:10:24 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
01.π Wale wanafunzi walioongoza Mashuleni, wanaenda kwenye Engineering na Medical school.
02.π Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.π Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia Siasa na kuwaongoza wote hapo juu. Yaani wa kwanza na wa pili.
04.π Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu wote hawana raha.
05.π Wale waliopata Zero na waliokataa shule wanakuwa waganga wa kienyeji, wote hapo juu watamtafuta huyu, pale mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake. ππππππππππΏππΏπππππ
Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
Updated at: 2024-05-25 18:08:10 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa. RAFIKI: Nini tena?
JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje? JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, βHuyo nguruwe umeshamuondoa?β Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja
Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?β¦.Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka β¦majimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
Updated at: 2024-05-25 18:05:01 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?β¦.Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka β¦majimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo