Updated at: 2024-05-25 16:24:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Haki za binadamu ni haki zinazohusiana na mambo ya msingi na
asili ya uhuru na heshima ya ubinadamu ambapo watu wote wamepewa
haki ya kupata heshima kama
binadamu. Mara mtu azaliwapo
mume au mke hupata
haki hizi. Haki hizi
zinatambuliwa kimataifa
na zina usawa kwa watu
wote. Nchi mbalimbali
zimetia saini na kuidhinisha
haki hizi za kimataifa
na kufanya ni sehemu
ya sheria zao
pamoja na kuweka sera
zinazolinda haki hizi.
Haki za uzazi zina misingi yake katika haki za binadamu na pia
zinahusiana na haki za mtu mmojammoja.
Kupata habari juu ya ujinsia na mada zinazohusu afya
ya uzazi.
Mwanamke au mwanaume kuamua kwa uhuru na
kuwajibika, kama unataka kujamiaana lini na nani.
Uhuru wa maamuzi.
Kuamua kwa hiari na kuwajibika juu ya idadi na muda wa
kupishana katika kupata watoto.
Kupata huduma za afya ya uzazi kwa urahisi.
Haki za kufanya maamuzi kuhusu afya ya uzazi, kwa
uhuru, bila kunyanyaswa, kulazimishwa, bila kutumia
nguvu pamoja na maamuzi nani wa kufunga naye ndoa.
Kujilinda kutokana na mila zenye madhara kama vile
ukeketaji wa wanawake.
Haki hizi zimerekebishwa tangu mkutano uliofanyika Cairo mwaka
19941.
Je, nifanye nini ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?
Updated at: 2024-05-25 16:22:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hakuna chanjo dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, Lakini kuna mienendo ya tabia ambayo i itaweza kukusaidia kujikinga na maambukizi ya UKIMWI na UKIMWI. Kutokufanya ngono kabisa ni njia mojawapo ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI na UKIMWI. Kuwa mwaminifu na kuwa na mpenzi i ambaye hajaambukizwa ni njia nyingine ya kujikinga. Lakini hii i ii inahitaji wote muwe katika afya nzuri ( bila maambukizi) wakati mnaanza uhusiano wa kujamii ana kwa mara ya kwanza. Pia i inashauriwa hima kutafuta matibabu ya magonjwa ya ngono mara pale yatakapojitokeza. Vidonda vinavyosababishwa na magonjwa ya ngono vinasababisha mwingiliano wa maji maji ya ukeni, maji maji ya uumeni na damu wakati wa kujamii ana na kuwezesha Virusi vya UKIMWI kupita kwa urahisi. Kufuata kanuni za ngono salama ni njia nyingine ya kujikinga ili usiambukizwe na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ngono salama kwa upande mwingine ni kitendo cha kukaribiana ambacho hakitahusisha uume kuingia ukeni au njia ya haja kubwa. Pia utumiaji wa kondomu kila wakati ngono i itahusisha kuingizwa kwa umme, ukeni au njia ya haja kubwa ni njia nyingine ya kujikinga
Je, kuna umuhimu wa kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?
Je, unajua umuhimu wa kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi? Hapana? Usijali, ninakufungulia macho katika nakala hii!
Updated at: 2024-05-25 16:17:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kila siku, tunaishi katika jamii ambayo ina maadili na kanuni za kufuata katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi. Haki na usawa ni suala muhimu katika uhusiano huu. Je, kuna umuhimu wa kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi? Jibu ni ndio. Katika makala hii, tutajadili umuhimu wa kujadili haki na usawa katika uhusiano huu.
Kuongeza ufahamu wa haki na usawa: Kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kuongeza ufahamu wa watu kuhusu haki na usawa. Hii inaweza kuwawezesha kufanya uamuzi sahihi katika uhusiano huu.
Kuzuia unyanyasaji wa kijinsia: Kujadili haki na usawa kunaweza kusaidia kuzuia unyanyasaji wa kijinsia katika uhusiano huu. Wote wanapaswa kuheshimiana na kufuatilia kanuni zinazosimamia uhusiano huu.
Kuzuia magonjwa ya zinaa: Kujadili haki na usawa kunaweza kusaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Mtu anapaswa kuvaa kondomu kujilinda na magonjwa ya zinaa.
Kujenga uhusiano wa kudumu: Kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi kunaweza kusaidia kujenga uhusiano wa kudumu. Uhusiano wa kudumu huboresha ubora wa maisha na kuongeza furaha.
Kusaidia kupunguza dhuluma za kijinsia: Kujadili haki na usawa kunaweza kusaidia kupunguza dhuluma za kijinsia katika uhusiano huu. Haki na usawa ni mambo muhimu katika kuzuia dhuluma za kijinsia.
Kujenga uaminifu: Kujadili haki na usawa kunaweza kusaidia kujenga uaminifu katika uhusiano huu. Uaminifu ni muhimu sana katika uhusiano wa kimapenzi.
Kuzuia mimba zisizotarajiwa: Kujadili haki na usawa kunaweza kusaidia kuzuia mimba zisizotarajiwa katika uhusiano huu. Kila mmoja anapaswa kufanya uamuzi sahihi kuhusu uzazi wa mpango.
Kupunguza kiwango cha talaka: Kujadili haki na usawa kunaweza kusaidia kupunguza kiwango cha talaka katika uhusiano huu. Talaka ni moja ya mambo yanayoweza kuharibu uhusiano wa kimapenzi.
Kuwezesha mawasiliano: Kujadili haki na usawa kunaweza kuwezesha mawasiliano katika uhusiano huu. Mawasiliano ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa uhusiano unaendelea vizuri.
Kujenga upendo: Kujadili haki na usawa kunaweza kusaidia kujenga upendo katika uhusiano huu. Upendo ni muhimu sana katika uhusiano wa kimapenzi.
Kwa hiyo, kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi ni muhimu sana. Haki na usawa ni mambo muhimu katika kukuza uhusiano wa kimapenzi. Kuongeza ufahamu wa haki na usawa, kuzuia unyanyasaji wa kijinsia, kuzuia magonjwa ya zinaa na kujenga uhusiano wa kudumu ni baadhi ya faida ya kujadili haki na usawa. Kwa hiyo, ni muhimu sana kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi. Je, wewe umejadili haki na usawa katika uhusiano wako wa kimapenzi? Je, unafikiri ni muhimu kujadili haki na usawa katika uhusiano huu? Napenda kusikia kutoka kwako.
Kwa nini mara nyingine mimba inatungwa kwenye mrija wa kupitisha mayai badala ya kwenye tumbo la uzazi?
Updated at: 2024-05-25 16:22:17 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mara nyingi utunguaji mimba nje ya mfuko wa uzazi hutokea kwa sababu ya maradhi kwenye via vya uzazi. Maradhi hayo huharibu mirija ya kupitisha mayai. Uharibifu huo hufanya yai lisiweze kufika kwenye mfuko wa mimba na mara nyingi unasababishwa na magonjwa ya zinaa. Kama mwanamke alikuwa na magonjwa ya zinaa uwezekano wa kutunga mimba kwenye mrija wa kupitia mayai unaongezeka. Ikiwa unafikiri una mimba au iwapo una maumivu chini ya tumbo, unashauriwa uende kliniki kwa ajili ya uchunguzi. Yai lililorutubishwa linapokaa kwenye mrija wa kupitisha mayai tunasema mimba i imetungwa nje ya mji wa mimba”ectopic pregnancy”. Kwa maana hiyo basi,, ukuta mwembamba wa mrija utashindwa kutanuka kikamilifu i ili kubeba mimba i inayokua. Mrija hupasuka na damu kutoka. Ikitokea hali hii , lazima mwanamke aende hospitali kwa ajili ya kupasuliwa na pengine kuongezwa damu.
Updated at: 2024-05-25 16:22:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Zipo aina mbili za mapacha, wale wanaofanana na wale wasiofanana. Karibu robo ya mapacha wote hufanana. Hii ina maana kwamba wametokana na yai moja lililotungwa mimba ambalo hujigawa katika makundi mawili tofauti ya chembechembe, kila mojawapo hubadilika kuwa kiumbe pekee. Hadi sasa, wataalamu hawaelewi vizuri sababu za yai kujigawa. Mapacha wa aina hii , kwa vile wametokana na yai moja, mara zote huwa na jinsia moja na hufanana sana kimaumbile.
Mapacha wasiofanana hutokea wakati wa yai kupevuka, kokwa za mwanamke hutokea zikawa mayai mawili badala ya moja tu. Mayai yote mawili hurutubishwa na hutungishwa mimba kwa mbegu mbili tofauti za mwanaume. Viumbe viwili hukua wakati mmoja katika mfuko wa uzazi. Mbali ya kukua katika mfuko mmoja wa uzazi na kuwa na umri uleule, mapacha hawa ni sawa sawa na watoto wengine wawili wa wazazi haohao. Wanaweza kuwa wa jinsia na maumbile tofauti kabisa.
Updated at: 2024-05-25 16:24:06 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Afya ya uzazi inahusiana na mfumo wa uzazi wa mtu, na via
vya uzazi kwa watu. Kwa hali hiyo basi inahusiana na mambo
yote yanayojumuisha uzazi na ujinsia. Ina maana kuwa watu
wana uwezo wa kukidhi mapenzi na usalama katika maisha
yao, kwamba watu wana uwezo wa kuwa na watoto na pia wana
uhuru wa kuamua, kama lini na kwa muda gani wapate watoto.
Yaliyomo humu yanampa haki mwanamume na mwanamke kupewa
habari au kuelekezwa na kufikiwa na njia za uzazi wa mpango
ambazo ni salama, zinazofanya kazi, anazomudu kulipia na njia
zinazokubalika za uzazi wa mpango alizochagua na haki ya kuwa
na huduma za afya zinazofaa ambazo zitawawezesha wanawake
kuwa salama wakati wa ujazito na kujifungua.
Updated at: 2024-05-25 16:22:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Neno VVU ni i virusi au vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI. Neno hili kwa lugha ya Kii ngereza ni HIV yaani “Human Immunodeficiency Virus”. UKIMWI ni kifupi cha maneno matatu ambayo ni Upungufu wa Kinga Mwilini. Kwa Kii ngereza jina la UKIMWI AIDS ambacho kirefu chake ni “Acquired Immune Deficiency Syndrome”. Neno UKIMWI tayari linaonyesha tayari aina ya ugonjwa, i ikii manisha kuwa mwili umepungua uwezo wake wa kinga kwa maradhi mbalimbali mwilini. Dalili za upungufu huu ukianza kujitokeza basi maradhi haya huitwa UKIMWI.
Tofauti kati ya VVU na UKIMWI ni kuwa mtu aliyeambukizwa VVU bado anaweza kuonekana mzima wa afya. Pamoja na kuwa virusi hivyo vitaonenekana katika damu yake, ni kwamba virusi hivyo vitakuwa havijaanza bado kushambulia chembechembe nyeupe za damu. Kwa upande mwingine kinga ya mwili ya mtu anayeumwa UKIMWI i itakuwa tayari i i imepungua. Mwili wake utaanza kuugua magonjwa nyemelezi. Magonjwa nyemelezi hupata nafasi ya kushambulia mwili huu ambao tayari kinga imepungua. Watu wnaoumwa UKIMWI wanaweza kupungua uzito wa mwili, kuharisha au kupata matatizo ya ngozi. Hata hivyo maradhi haya siyo lazima yatokane na kuwa na VVU. Ili kuwa na uhakika, onana na mtaalamu yaani dakatari wako.
Kwa nini watu wasio na ualbino wanaogopa kuoa Albino kwa imani kuwa watawazalia watoto Albino?
Updated at: 2024-05-25 16:24:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ualbino ni hali ya kurithi, hii inamaanisha kuwa unapata ualbino kutoka kwa wazazi wako. Watu wawili weusi wanaweza kupata Albino endapo kila mmoja wao atakuwa na kinasaba cha ualbino. Hali hii huwezi kuiona au kuijua. Unaweza tu kuitambua baada ya kujifungua. Takribani mtu mmoja katika watu 70 ana kinasaba cha ualbino lakini si rahisi kujua ni nani anacho. Endapo Albino ataoa mwanamke mweusi, uwezekano wa kuzaa Albino ni mdogo sana. Albino wengi waliooa au kuolewa na watu weusi wamepata watoto ambao ni weusi.
Kwa upande mwingine, wanandoa ambao wamekwisha pata mtoto Albino kuna uwezekano wa kupata mtoto mwingine Albino katika uzazi wa pili. Kuzaliwa Albino ni lazima mtoto huyo arithi vinasaba vya ualbino kutoka kwa wazazi wote wawili, yaani mama na baba.
Je, ni kweli matumizi ya dawa za kulevya ni mojawapo ya sababu zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU)
Updated at: 2024-05-25 16:22:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dawa za kulevya zenyewe hazisababishi UKIMWI na magonjwa ya zinaa. Lakini utumiaji wa dawa za kulevya hurahisisha kupata na kuenea kwa magonjwa haya. Dawa hizi hudhoofisha mwili na kinga ya mwili. Hivyo basi hurahisisha virusi vya magonjwa kuingia mwilini mwa mtumiaji kiurahisi.
Matumizi ya dawa za kulevya huwafanya watumiaji kusahau hatari za kuwa na wapenzi wengi pamoja na kufanya ngono na watu usiofahamu hali za afya zao. Hujisahau kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu. Vilevile husahau majukumu yao kama vile mke, watoto na familia nzima kwa ujumla. Dawa za kulevya zinazoingia mwilini kwa njia ya sindano husababisha uwezekano mkubwa wa kuenea kwa virusi vya UKIMWI (VVU) kwa watumiaji pindi wanapochangia sindano kujidungia dawa hizo mwilini. Pia dawa za kulevya huchangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI kwa kuwa watumiaji hujii ngiza katika biashara ya ngono i ili kuweza kujipatia fedha za kununulia dawa hizo.
Updated at: 2024-05-25 16:24:28 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watoto hawatakiwi kunywa pombe wala kuvuta sigara!
Watoto hasa ndio wapo katika hatari zaidi ya kupata madhara yatokanayo na uvutaji sigara na unywaji pombe, kwa sababu bado wanaendelea kukua. Wanaweza wakaathiri miili yao na ubongo kwa maisha yao yote. Wana hatari zaidi ya kuathirika katika maendeleo yao ya kijamii na kisaikolojia. Matumizi mabaya ya pombe na sigara yanaweza yakaleta madhara katika makuzi ya mtoto.