Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) 100g Sukari (sugar) 100g Siagi isiyokuwa na chumvi (unsalted butter) 100g Mayai (eggs) 2 Vanila 1 kijiko cha chai Chumvi pinch Warm water 3 vijiko vya chakula
Matayarisho
Kwanza washa oven moto wa 200 C. Baada ya hapo saga butter na sukari mpaka viwe laini kisha tia mayai na uendelee kusaga mpaka vichanganyike vizuri kisha tia unga, vanila, chumvi na na maji na usage mpaka upate uji usiokuwa mzito sana au mwepesi sana. Baada ya hapo utie kwenye baking tin na u bake kwa muda wa dakika 25 na mpaka cake yako iive yani juu na chini iwe ya brown na ukidumbukiza kijiti katikati kinatoka kikiwa clean. Baada ya hapo itoe kwenye tin na uiache ipoe. Ikisha poa itakuwa tayari kwa kuliwa.
Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan
Updated at: 2024-05-25 10:23:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama ya mbuzi au ng’ombe ya mafupa - 2 LB
Mchanganyiko wa dengu (hadesi, mchele, chooko, ngano, dengu n.k au nunua ya tayari iliyokwisha changanywa - 2 Vikombe
Kitungu maji (vikate vidogo) - 1
Mafuta - ¼ Kikombe
Nyana kata ndogo ndogo - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawazi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu
Bizari ya haliym - 2 vijiko vya supu
Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha nyama na chumvi ½ kijiko mpaka iive, toa mafupa. Chemsha mchanganyiko wa dengu mpaka ziive. Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu vilainike, tia thomu na tangawizi, bizari ya haliym, nyanya ya kopo. Kaanga mpaka iwive. Tia nyama iliyowiva na supu yake kidogo. Tia mchanganyiko wa dengu tia kwenye mashine ya kusaga (blender), saga na ile supu ya nyama isagike vizuri Mimina kwenye sufuria changanya, tia ndimu kidogo, acha moto mdogo mdogo kwa muda wa dakika 15. Tia katika bakuli, pambia kwa vitunguu vilivyokaangwa vya rangi ya hudhurungi vikavu, pilipili mbichi (ukipenda) na kotmiri, ikiwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote.. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau. Tia bizari zote isipokuwa hiliki. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.