Bizari ya unga (cummin powder) - 1 Kijiko cha chai
Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Safisha daal kwa kutoa mawe ikiwa yapo, kisha osha na roweka dakika 15 hivi. Kisha chemsha kwa kutia maji, bizari ya manjano, chumvi, pili pili ya unga na maji ya ndimu hadi iive na kuvurujika. Halafu chukua kisufuria na kaanga kitungu, kisha thomu na mwisho tia bizari ya pilau. Kisha mimina mchanganyiko wa kitunguu kwenye sufuria ya daal (iliyokwisha iiva)na uchanganye na iwache motoni kidogo itokote. Ukipenda mimina mchanganyiko kwenye blenda na usage mpaka iwe laini. Tia kwenye bakuli na itakuwa tayari kuliwa na wali na samaki ukipenda
Updated at: 2024-05-25 10:34:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO:
Unga wa Visheti
Unga 4 Vikombe vya chai
Siagi 1 Kikombe cha chai
Hiliki ½ Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
2. Changanya vizuri isiwe na madonge.
3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.
Shira:
Sukari 2 Vikombe vya chai
Maji 1 Kikombe cha chai
Vanilla ½ Kijiko cha chai
(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Tambi (spaghetti 1/2 ya packet) Mafuta (vegetable oil) Sukari (sugar 1/2 kikombe cha chai) Hiliki (cardamon 1/2 kijiko cha chai) Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai) Tui la nazi (coconut oil 1 kikombe cha chai) Maji kiasi
Matayarisho
Tia mafuta kiasi kwenye sufuria kisha ibandike jikoni (katika moto wa wastani) yakisha pata moto kiasi tia tambi na uanze kuzikaanga kwa kuzigeuzageuza kila mara mpaka zitakapokuwa za yangi ya light brown. baada ya hapo ipua na umwage mafuta ya kwenye tambi (bakiza kidogo sana kwani usipofanya hivyo tambi zitakuwa na mafuta sana) Baada ya hapo zirudishe jikoni na kisha utie hiliki, chumvi, sukari, tui la nazi na maji kiasi. Zifunike kisha ziache zichemke mpaka maji yakauke. Baada ya hapo zigeuze na uzipike mpaka ziive. Nahapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mackerel 2 Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2 Limao (lemon) 1/2 Chumvi (salt) kiasi Curry powder 1/2 kijiko cha chai Coriander powder 1/2 kijiko cha chai Mafuta 1 kijiko cha chai
Matayarisho
Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Ngogwe ½ kg Kitunguu 2 Bamia ¼ kg Karoti 2 Mafuta vijiko vikubwa 8 Maji vikombe 3 Mayai 2 Nyanya 2 Chumvi
Hatua
• Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu. • Osha, menya na kata karoti virefu virefu. • Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata vipande viwili. • Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili. • Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike. • Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka zionekane kukolea rojo. • Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au mpaka ziive. Punguza moto. • Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia kwa dakika 5. • Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa Basmati /Pishori - 4 vikombe
Kuku
Vitunguu - 3
Nyanya/Tungule - 2
Tangawizi mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi nzima - 3
Ndimu - 2
Garama Masala/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu
Haldi/tumeric/bizari manjano - 1 kijiko cha chai
Pilipilu ya unga nyekundu - 1 kijiko cha chai
Mtindi /yoghurt - 3 vijiko vya supu
Mafuta ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele, roweka. Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli. Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu. Punguza mchanganyiko kidogo weka kando. Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi. Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive. Epua, weka kando. Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando. Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali. Tia kuku uchaganye vizuri. Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja. Punguza masala nusu yake weka kando. Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali. Funika upike katika oveni hadi uive. Changanya unapopakua katika sahani.
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Ndizi mbichi - 10
Nyama - kilo 1
Nazi ya kopo - 1
Chumvi - 1 Kijiko cha chakula
Ndimu - 1
Bizari ya manjano - 1 Kijiko cha chai
Pili pili mbichi - 3
Nyanya (tomatoes) - 2
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chakula
Namna ya Kutayarisha Na Kupika
Kata nyama vipande vipande na uisafishe. Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive. Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria. Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo. Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda. Weka pembeni zipoe. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Maziwa ya unga - 2 vikombe
Sukari - 3 vikombe
Maji - 3 vikombe
Unga wa ngano - ½ kikombe
Mafuta - ½ kikombe
Iliki - kiasi
MAPISHI
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.