Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 2 Mugs
Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) - Mug
Tuna (samaki/jodari) - 2 kopo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu
Garam masala - 1 kijiko cha supu
Nyanya - 2
Kitungu maji - 1
Mdalasini nzima - 2 vijiti
Karafuu - 6 chembe
Pilipili mbichi - 1
Chumvi - kiasi
Viazi - 3
Maji - 2 ½ Mugs
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Maandalizi
Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20 Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga. Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive. Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu. Tia maji, yatakapochemka tia mchele. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:51 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 1 Magi (vikombe vya chai)
Sukari ya browni ½ Magi
Siagi iliyoyayushwa 125 g
Nazi iliyokunwa ½ Magi
Mjazo wa karameli (Caramel filling)
Syrup 1/3 kikombe cha chai
Siagi iliyoyayushwa 125 g
Maziwa matamu ya mgando 2 vikopo (condensed milk)
Mjazo wa chokoleti (Chocolate filling)
Chokoleti 185 g (dark chocolate)
Mafuta 3 Vijiko vya chai
Jinsi ya kuandaa na kupika
1. Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.
2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda.
3. Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni.
4. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu.
5. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane.
6. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi - 15 takriiban
Nayma ya ng’ombe - 1 kilo
Kitunguu maji - 1
Nyanya - 3
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi ilopondwa - 2
Jira/cummin/bizari ya pilau ilosagwa - 1 kijiko cha chai
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha nyama kwa ndimu, chumvi na tangawizi mbichi na kitunguu thomu. Menya ndizi na zikatekate vipande kiasi, weka katika sufuria. Katakata kitunguu na nyanya utie katika ndizi. Tia jira na chumvi. Nyama ikiwiva mimina pamoja na supu yake ufunike ndizi ziwive na kuwa tayari kuliwa. Ukipenda tia pilipili mbuzi zichemke pamoja na ndizi.
Updated at: 2024-05-25 10:37:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Mgagani mkono 1 Mafuta vijiko vikubwa 4 Karanga zilizosagwa kikombe ½ Maji kikombe 1 Kitunguu 1 Karoti 2 Maziwa kikombe 1 Chumvi kiasi
Hatua
• Chambua mgagani, oshana katakata. • Chemsha maji, weka chumvi kisha ongeza mgagani, funika zichemmke kwa • dakika 5-10. • Menye osha na katakata kitunguu. • Osha, menya na kwaruza karoti. • Kaanga karanga, ondoa maganda na saga. • Kaanga vitunguu na karoti mpaka zilainike ukikoroga. • Weka mgagani uliochemshwa koroga sawasa na funika kwa dakika 5 zilainike. • Changanya maziwa na karanga ongeza kwenye mgagani ukikoroga kasha punguza moto kwa dakika 5 ziive. • Onja chumvi na pakua kama kitoweo.
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama (kata vipande vidogodogo) - ½ kilo
Maharage - 3 vikombe
Mahindi - 2 vikombe
Kitunguu - 1
Nyanya - 2
Kabichi lililokatwa - 2 vikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Vidonge vya supu - 2
Chumvi - kiasi
Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula
Namna Yakutayarisha
Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi. Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi. Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi. Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi. Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive. Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano ( self risen flour) kikombe 1 na 1/2 Hamira (yeast) 1 kijiko cha chai Sukari (sugar) 1 kijiko cha chakula Chumvi (salt) 1/2 kijiko cha chai Siagi iliyoyeyushwa (melted butter) 1 kijiko cha chakula Maji ya uvuguvugu ( warm water) kiasi
Matayarisho
Changanya vitu vyote katika bakuli kubwa kisha aanza kukanda mpaka upate donge laini.Baada ya hapo liweke hilo donge kwenye bakuli la plastic na weke katika sehemu yenye joto ili unga uumuke. Hakikisha unga unaumuka zaidi (yani unaji double size) unaweza kuchukua kama saa 1 na nusu hivi. Baada ya hapo ukande tena na uache uumuke tena kwa mara ya pili, Ukisha umuka pakaza butter katika baking tin (chombo cha kuokea) na upakaze mkate butter kwa juu,kisha uoke katika oven kwa muda wa dakika 30 (katika moto wa 200C) (hakikisha juu na chini unakuwa wa brown Na hapo mkate wako utakuwa tayari
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga ngano vikombc 3 Unga mbegu za mchicha kikombe 1 Baking powder vijiko vidogo Maziwa kikombe 1 Sukari kikombe 1 Blue band kikombe ½ Mayai 10-12
Hatua
• Chagua, osha, kausha mbegu za mchicha mweupe, kisha saga zilainike. • Chekecha unga wa ngano, unga wa mbegu za mchicha na baking powder Kwenye bakuli kubwa. • Ongeza sukari na changanya. • Ongeza mayai kidogo, kidogo ukikoroga na mwiko kwenda njia moja mpaka ilainike. • Kama rojo ni zito ongeza mayai, au maziwa ili iwe laini, ongeza vanilla na koroga. • Paka mafuta kwenye chombo cha kuoka au sufuria na chekechea unga kidogo. • Mimina rojo ya keki na oka kwenye oveni au kama ni sufuria funika, weka moto mwingi juu, chini weka moto kidogo. • Ukinusia harufu nzuri ya vanilla, funua, choma kisu katikati ya keki, kama ni kavu epua, pozesha na pakua kama kitafunio.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Tende zilizotolewa kokwa - 1 Kilo
Cornflakes - 1 ½ kikombe
Lozi Zilokatwa katwa - 1 kikombe
Siagi - ¼ kilo
MANDALIZI
Mimina tende na siagi kwenye sufuria bandika motoni moto mdogo mdogo mpaka zilainike. Kwa muda wa dakika 10. Isonge kidogo kwa mwiko au kuikoroga ichanganyike vizuri. Changanya Cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyika vizuri. Pakaza treya au sinia mafuta au siagi kidogo. Mimina mchanganyiko wa tende, zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda. Zikiwa tayari kuliwa kwa kahawa.
Chemsha nyama na chumvi na nusu ya limao mpaka iive kisha weka pembeni. Baada ya hapo andaa vitu vya pilau kwa kuloweka mchele kwenye maji kwa muda wa dakika 10.Menya na kukatakata vitunguu na viazi kisha weka pembeni na pia chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Baada ya hapo weka sufuri jikoni na tia mafuta kiasi . Yakisha pata moto tia vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya rangi ya kahawia na kisha uitie nyama na ikaange mpaka ipate rangi ya bown pia. Baada ya hapo tia kitunguu swaum na tangawizi na uikoroge vizuri kisha iache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia spice ambazo ni Binzari nyembamba ya unga, hiliki,karafuu, amdalasini na pilipili mtama na viazi. Baada ya hapo unatakiwa ugeuze geuze mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia mchele na ugeuzege mpaka uchanganyike na viungo. Baada ya hapo tia chumvi na maji ya kutosha na ukoroge vizuri kisha funika na uache uchemke katika moto wa wastani. Maji yakikaribia kukauka tia binzari nyembamba nzima na ufunike uache mpaka maji yakauke kabisa. maji yakisha kauka ugeuze na ufunike tena na uuache mpaka uive. Baada ya hapo andaa kachumbali kwa kukatakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili, hoho na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuliwa.