Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kambale 2 Nazi kopo 1 Nyanya kopo 1 Vitunguu 2 Curry powder 1 kijiko cha chai Turmaric 1/2 kijiko cha chai Binzari nyembamba ya unga 1/2 kijiko cha chai Swaum/ tangawizi 1 kijiko cha chakula Giligilani kiasi Limao 1/2 Chumvi Olive oil
Matayarisho
Loweka samaki katika maji ya moto kwa muda wa muda wa nusu saa.Baada ya hapo Saga pamoja nyanya, vitunguu, swaum na tangawizi kisha vibandike jikoni na uvipike mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta. Pika mpaka nyanya zitengane na mafuta kisha tia spice zote.Zipike kwa muda mdogo kisha tia tui la nazi, maji kiasi, samaki, pilipili nzima, chumvi na kamulia limao. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na samaki pia wawe wameiva na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo ipua kisha tia giligilani iliyokatwa na mchuzi utakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuulia kwa chochote kile upendacho. Mi hupendaga kuulia na ugali mlaiiini au na wali pia.
Updated at: 2024-05-25 10:34:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO:
Unga wa Visheti
Unga 4 Vikombe vya chai
Siagi 1 Kikombe cha chai
Hiliki ½ Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
2. Changanya vizuri isiwe na madonge.
3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.
Shira:
Sukari 2 Vikombe vya chai
Maji 1 Kikombe cha chai
Vanilla ½ Kijiko cha chai
(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Mayai 5
Sukari 450gm (1 lb)
Unga wa Ngano 1 kg
Siagi 450gm (1 lb)
Baking powder ½ Kijiko cha chai
Unga wa Custard Vijiko 2 vya chakula
Karanga za kusaga 250gm
Jam ½ kikombe
MAANDALIZI
Chukua bakuli la kiasi, weka sukari na siagi. Changanya sukari na siagi kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cakemixer), mpaka sukari ichanganyike na siagi. Vunja yai moja moja na weka kiini chake kwenye mchanganyiko wa sukari na siagi, endelea kuchanganya mpaka ichanganyike vizuri. Hifadhi ute wa mayai ndani ya kibakuli. Mimina unga wa ngano ndani ya mchanganyiko wako huku ukichanganya Changanya unga wa custard na baking powder. Tengeneza viduara vidogo vidogo. Vichovye viduara ndani ya ute wa yai kisha zimwagie unga wa karanga na kuzipanga kwenye tray ya kuchomea. Weka dole gumba kati kati ya kila kiduara na uweke jam. Washa jiko (oven) 350F na uchome vileja vyako kwa dakika 20. Toa vileja vyako vipoe na uviweke ndani ya sahani tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Mchele wa pishori (basmati) - 4
Vitunguu katakata - 3
Nyanya (tungule) katakata vipande vikubwa - 3 -5
Pilipili boga la kijani (capsicum) katakata
Supu ya kitoweo au vidonge vya supu - 1
Bizari mchanganyiko Garama masala - 5-7
Pilipili mbichi ya kusaga - Kiasi
Zaafarani ya maji (flavor) - 1 kijiko cha chakula
Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe
Samaki wa kukaanga
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Roweka mchele kiasi nusu saa kisha chemsha mchele kwa supu uive nusu kiini. Mwaga maji chuja. Wakati mchele unapikika, weka mafuta katika sufuria kubwa ya kupikia wali, kaanga vitunguu mpaka vigeuke rangi ya hudhurungi. Tia nyanya na vitu vinginevyo vyote kaanga kidogo tu. Mwaga wali katika sufuria na nyunyizia zaafarani kisha changanya na masala vizuri. Funika upike katika oven (bake) au juu ya stovu moto mdogo mdogo kiasi dakika 15- 20. Epua ikiwa tayari, pakua kwenye sahani kisha tolea kwa samaki wa kukaanga.
Updated at: 2024-05-25 10:37:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Pilipili hoho (Red pepper 3) Cougette 1 Kitunguu (onion 1) Uyoga (mashroom 1 kikombe cha chai) Carrot 1 Nyanya (fresh tomato 1) Nyanya ya kopo iliyosagwa (tomato paste 3 vijiko vya chai) Giligilani (fresh coriander) Binzari manjano (Turmaric 1/2 ya kijiko cha chai) Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai Chumvi (salt) Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Kata hoho kati na utoe moyo wake kisha ziweke pembeni, Kisha katakata cougette, kitunguu, uyoga, carrot, nyanya katika vipande vidogo vidogo, Weka sufuria jikoni na uanze kupika uyoga kwa muda wa dakika 5, kisha weka curry powder, turmaric na chumvi na kaanga kidogo kisha weka vegetable zilizobakia pamoja na nyanya ya kusaga pamoja na giligilani. Zikaange kwa muda wa dakika 5 kisha zitie kwenye hoho na kisha uzibake kwa muda wa dakika 20 na hapo zitakuwa tayari kuseviwa na wali. Wali: angalia katika recipe zilizopita
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 3 Vikombe
Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
Siagi 250 gm
Mayai 3
Vanilla 2 Vijiko vya chai
Baking powder 1 Kijiko cha chai
JINSI YA KUPIKA
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini. Tia unga na baking powder changanya na mwiko. Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi. Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma. Pika (bake) katika oven moto wa 350°F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Jinsi ya kutengeneza Cookies Za Tende Na Tangawizi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe vikombe 4
Baking soda 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi 400 gms
Sukari ½ kikombe
Tende chambua ukatekate ifikie ¾ kikombe
Tangawizi ya unga vijiko 2 vya chai
Vanilla 1 kijiko cha chai
Yai 1
Maziwa mazito vijiko 2 vya kulia.
MAANDALIZI
Changanya siagi na sukari katika mashine usage mpaka iwe laini nyororo. Tia yai uchanganye vizuri Tia tende na vanilla, tangawizi uchanganye vizuri. changanya unga na baking soda kisha, mimina kidogo kidogo huku unachanganya kwa kijiko cha ubao (mwiko). Unga ukiwa mzito ongeza vijiko 2 vya maziwa. Fanya viduara upange katika treya uliyopakaza siagi kisha uchome (bake) katika over moto mdogo wa kiasi dakika 15 vigeuke rangi viwive. Epua vikiwa tayari
Updated at: 2024-05-25 10:37:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kupata takriban gilasi 6
Mabungo - 3
Maji - 6 au 7 Gilasi
Sukari - kiasi upendacho
Chumvi - kidogo sana
Namna Ya Kutayarisha:
Kata mabungo na toa nyama yake tia katika mashine ya kusagia. Tia maji, sukari na chumvi usage kidogo tu. Chuja kisha mimina katika jagi uweke katika friji. Mimina katika gilasi.
Jinsi ya kupika Biriani ya Nyama Ng'ombe Na Mtindi
Updated at: 2024-05-25 10:37:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa biriani - 5 gilasi
Nyama ya ngombe ya mifupa - 1 ½ kilo na nusu
Vitunguu - 2 kilo
Tangawizi mbichi - ¼ kikombe
Thomu (saumu/garlic) - 3 vijiko vya supu
Mtindi - 2 vikombe
Nyanya ilokatwakatwa (chopped) - 3
Nyanya kopo - 1 kikombe
Masala ya biriani - 2 vijiko vya supu
Hiliki ya unga - 2 vijiko vya chai
Pilipili mbichi ilosagwa - 3 kiasi
Kotmiri ilokatwakatwa - 1 msongo (bunch)
Rangi ya biriani ya manjano - ½ kijiko cha chai
Zaafarani au zaafarani flavour - 1 kijiko cha supu
Mafuta ya kukaangia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katakata vitunguu ukaangae katika mafuta mpaka vigeuke rangi ya brown ilokoza. Weka nyama iwe ilokatwakatwa katika treya au bakuli kubwa la oveni. Chaganya pamoja na tangawizi, thomu, nyanya, nyanya kopo, mtindi, masala ya biriani, chumvi, pilipili. Acha irowanike kwa muda wa masaa mawili takriban. Funika kwa karatasi ya jalbosi (foil paper) utie katika oveni upike muda wa dakika 45 takriban mpaka nyama iwive na huku unachanganya changanya sosi. Ikiwa ina maji ongezea nyanya kopo iwe nzito. Epua funua, kisha vuruga vitungu umwagie pamoja na kotmiri na umwagie mafuta ya moto kiasi. Ongezea kutia masala ya biriani na hiliki ya unga. Chemsha mchele nusu kiini, mwaga maji chuja, umwagie juu ya sosi ya nyama ukipenda kuchanganya au chemsha wali pekee. Nyunyizia rangi ya biriani pamoja na zaafarani flavour au zaafarani yenyewe ukipenda. Mimina mchele juu ya masala ya nyama, funika urudishe ndani ya oven upike muda wa kiasi ya dakika ishirini. Epua upake kwa kuchota wali kwanza kisha masala uwekee juu yake, kiwa tayari.