Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Tende zilizotolewa kokwa - 1 Kilo
Cornflakes - 1 ½ kikombe
Lozi Zilokatwa katwa - 1 kikombe
Siagi - ¼ kilo
MANDALIZI
Mimina tende na siagi kwenye sufuria bandika motoni moto mdogo mdogo mpaka zilainike. Kwa muda wa dakika 10. Isonge kidogo kwa mwiko au kuikoroga ichanganyike vizuri. Changanya Cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyika vizuri. Pakaza treya au sinia mafuta au siagi kidogo. Mimina mchanganyiko wa tende, zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda. Zikiwa tayari kuliwa kwa kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:43 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mshale 10 Utumbo wa ng'ombe 1/2 kilo Nazi ya kopo 1 Nyanya 1 Kitunguu kikubwa 1 Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chakula Olive oil kiasi Limao 1 Chumvi Curry powder 1 kijiko cha chai Turmaric 1/2 kijiko cha chai Coriander ya powder 1/2 kijiko cha chai Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai Pilipili kali nzima (usiipasue)
Matayarisho
Safisha utumbo kisha uweke ktk pressure cooker pamoja na chumvi kiasi, limao, tangawizi, swaum na maji kiasi kisha uchemshe kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo menya ndizi kisha zikate vipande vidogo kiasi ili ziwahi kuiva, kisha ktk sufuria ya kupikia tia vitunguu na nyanya kisha ndizi kwa juu yake na supu ya utumbo kiasi chumvi kidogo na mafuta kiasi kisha bandika jikoni na uchemshe mpaka ndizi zikaribie kuiva. Zikisha karibia kuiva tia utumbo na spice zote, pilipili nzima na tui la nazi kisha changanya vizuri na uache vichemke mpaka ndizi na tui la nazi vitakapoiva na rojo ibaki kiasi. Baada ya hapo Ndizi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:47 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Biriani ni miongoni mwa vyakula ambavyo ni nadra sana kupikwa katika familia nyingi tofauti na vyakula vingine. Inawezekana ni kutokana na watu wengi kutoelewa namna ya kuoika chakula hiki kutokana na kuhitaji viungo vingi ambavyo huwapa usumbufu wapishi. Kuna aina mbalimbali za upishi wa biriani ambapo mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika upishi. Biriani la mbogamboga ni miongoni mwa aina hizo za upishi. Chakula hiki kinaweza kuliwa na kila mtu hususan wale wasiotumia nyama wala samaki.
Mahitaji:
½ kg mchele wa basmati Kitunguu maji kikubwa 1 Nyanya 1 kubwa Karoti 1 kubwa Njegere robo kikombe Kiazi ulaya 1 kikubwa Tangawizi za kusaga kijiko 1 Kitunguu swaumu cha kusaga kijiko 1 Karafuu kijiko 1 Majani ya kotimili fungu 1 Maziwa ya mtingi ¼ kikombe Chumvi na pilipili kiasi Unga wa dhani kijiko 1 cha mezani Juisi ya limao kijiko 1 cha mezani Mafua ¼ lita
Maandalizi:
Chemsha mchele na kisha weka pembeni Osha mbogamboga zote isipokuwa vitunguu na nyanya Changanya mtindi na tangawizi pamoja na kitunguu swaumu viache vikae kwa muda wa saa moja Chukua sufuria weka mafuta na kisha kaanga vitunguu maji, weka nyanya, chumvi, kotimili na limao halafu weka karafuu na kanga hadi vichanganyike vizuri Miminia mchanganyiko wa mtindi na baadaye weka pilipili na baadaye weka unga wa dhania Chukua mchele uliochemshwa changanya na mchanganyiko huo Palia moto juu ya chakula chako na acha kwa muda wa dakika 30 Baada ya hapo chakula chako cha biriani kitakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:35 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa basmati - 3 vikombe
Kuku - ½
Viazi - 4
Vitunguu - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Binzari ya pilau nzima - 1 Kijiko cha chakula
Binzari ya pilau - ½ kijiko cha chai
Pilipili manga nzima - ½ kijiko cha chai
Karafuu nzima - 8
Iliki nzima - 6
Mdalasini nzima - 5 vijiti
Pilipili mbichi iliyosagwa - 2
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele. Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi. Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia thomu na tangawizi na binzari zote kaanga kidogo Kisha tia viazi kanga kidogo kisha tia kisha tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia. Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza) Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele Kisamvu kilichotwangwa Samaki Mbaazi Nyanya chungu Vitunguu Nyanya ya kopo Tangawizi Kitunguu swaum Vegetable oil Curry powder Tui la nazi (kopo 2) Chumvi Pilipili Limao
Matayarisho
Safisha samaki kisha wamarineti na kitunguu swaum, tangawizi, pilipili, chumvi na limao kwa muda wa masaa 3.Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana na uwaweke pembeni kwa ajili ya kuungwa.Katakata vitunguu maji, saga tangawizi na kitunguu swaum. Baada ya hapo injika sufuria ya mchuzi jikoni na mafuta kiasi ya kupikia, mafuta yakisha pata moto, tia vitunguu maji na vikaange mpaka viwe vya rangi ya brown. kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.kaanga kidogo kisha tia nyanya ya kopo moja na ufunike. acha mpaka nyanya ziive. Kisha tia chumvi na curry powder na uache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia samaki na nyanya chungu nakisha kamulia nusu ya limao. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi kopo moja na uache ichemke mpaka mchuzi uive.
Baada ya hapo chemsha kisamvu pamoja na mbaazi Kikisha iva, kaanga kitu na nyanya pembeni mpaka ziive kisha tia kisamvu. geuza mchanganyiko mpaka uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi na chumvi na aacha ichemke mpaka tui liive kisha ipua.malizia kwa kupika wali ambapo utachemsha maji kisha tia mafuta,chumvi na mchele na uupike mpaka uive kisha sevu na mboga ulizopika na mlo wako utakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kambale 2 Nazi kopo 1 Nyanya kopo 1 Vitunguu 2 Curry powder 1 kijiko cha chai Turmaric 1/2 kijiko cha chai Binzari nyembamba ya unga 1/2 kijiko cha chai Swaum/ tangawizi 1 kijiko cha chakula Giligilani kiasi Limao 1/2 Chumvi Olive oil
Matayarisho
Loweka samaki katika maji ya moto kwa muda wa muda wa nusu saa.Baada ya hapo Saga pamoja nyanya, vitunguu, swaum na tangawizi kisha vibandike jikoni na uvipike mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta. Pika mpaka nyanya zitengane na mafuta kisha tia spice zote.Zipike kwa muda mdogo kisha tia tui la nazi, maji kiasi, samaki, pilipili nzima, chumvi na kamulia limao. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na samaki pia wawe wameiva na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo ipua kisha tia giligilani iliyokatwa na mchuzi utakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuulia kwa chochote kile upendacho. Mi hupendaga kuulia na ugali mlaiiini au na wali pia.
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - ½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote.. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau. Tia bizari zote isipokuwa hiliki. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.
Jinsi ya kutengeneza Cookies Za Tende Na Tangawizi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe vikombe 4
Baking soda 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi 400 gms
Sukari ½ kikombe
Tende chambua ukatekate ifikie ¾ kikombe
Tangawizi ya unga vijiko 2 vya chai
Vanilla 1 kijiko cha chai
Yai 1
Maziwa mazito vijiko 2 vya kulia.
MAANDALIZI
Changanya siagi na sukari katika mashine usage mpaka iwe laini nyororo. Tia yai uchanganye vizuri Tia tende na vanilla, tangawizi uchanganye vizuri. changanya unga na baking soda kisha, mimina kidogo kidogo huku unachanganya kwa kijiko cha ubao (mwiko). Unga ukiwa mzito ongeza vijiko 2 vya maziwa. Fanya viduara upange katika treya uliyopakaza siagi kisha uchome (bake) katika over moto mdogo wa kiasi dakika 15 vigeuke rangi viwive. Epua vikiwa tayari