Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna nyama za aina mbili, nazo ni nyama nyeupe na nyama nyekundu.
Nyama nyeupe
Hizi ni nyama zitokanazo na samaki, kuku, ndege wa aina zote, bata, wadudu
Nyama nyekundu
Hutokana na ng’ombe, mbuzi, kondoo,nguruwe na wanyama wa porini.
Nyama ina virutubishi vingi muhimu kwa afya ya binadamu kama protini, vitamini na madini. Madini ya chuma yanayopatikana kwenye nyama ni rahisi sana kusharabiwa (kufyonzwa) mwilini na ni muhimu kwa kuongeza wekundu wa damu. Uwezo wa miili ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuyeyusha chakula na kusharabu (kufyonza) virutubishi hupungua. Utumiaji wa nyama nyekundu kwa wingi unaweza kuwaletea matatizo hasa katika uyeyushwaji tumboni kwani nyama nyekundu si rahisi kuyeyushwa ukilinganisha na nyama nyeupe.
Hata hivyo katika nchi yetu watu walio wengi wanatumia nyama kwa kiasi kidogo sana na mara chache. Si vyema watu hawa waache kabisa nyama nyekundu. Jambo la muhimu ni kutumia njia mbalimbali ili kuifanya nyama hii iyeyushwe kwa urahisi tumboni.
Namna ya kusaidia uyeyushwaji ni pamoja n a : -
• Kutafuna vizuri au kutumia nyama ya kusaga (kwa wanaoipata). • Kupika nyama na viungo vinavyosaidia kulainisha kama vile papai bichi, limao, vitunguu saumu n.k. • Kula nyama pamoja na papai
Kwa hiyo, kwa anayepata nyama nyekundu kwa wingi, kupunguza kiasi cha nyama hiyo na kuongeza kiasi cha nyama nyeupe. Na kwa yule asiyepata nyama nyeupe, apatapo nyama nyekundu asiache kutumia kwani ina umuhimu mwilini mwake.
Updated at: 2024-05-25 10:37:57 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga wa ngano vikombe vikubwa 3 Boga lililopondwa kikombe 1 Baking powder vijiko vidogo Sukari kikombe kikubwa 1 Blue band kikombe ½ Vanilla kijiko kidogo 1 Mayai 2 Maji kiasi/ maziwa (kama nilazima)
Hatua
• Osha boga, Kata, ondoa mbegu, kisha kata vipande vikubwa, chemsha na maji mpaka vilainike. • Kwangua boga la ndani ukiacha maganda na ponda sawasawa. • Chekecha unga (kila kikombe 1, vijiko vidogo 2 vya baking powder) kwenye bakuli kubwa. • Ongeza blue band na changanya sawasawa na vidole. • Ongeza sukari na changanya. • Ongeza mayai na koroga na mwiko. • Ongeza boga lililopondwa na koroga njia moja mpaka ilainike. • (Kama haikulainika ongeza yai /mayai au maziwa/ maji kidogo). • Ongeza vanilla na koroga. • Paka mafuta chombo cha kuokea au sufuria kisha chekecha unga kidogo wa ngano. • Mimina rojo la keki kwenye sufuria au chombo cha kuokea. • Oka kwenye oven au tumia sufuria na weka mkaa wa moto juu na chini moto kidogo mpaka iive. • Jaribu kuchoma kisu katikati, kama ni kavu keki imeiva, epua, pozesha kata tayari kwa kula, kama kitafunio.
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa Basmati /Pishori - 4 vikombe
Kuku
Vitunguu - 3
Nyanya/Tungule - 2
Tangawizi mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi nzima - 3
Ndimu - 2
Garama Masala/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu
Haldi/tumeric/bizari manjano - 1 kijiko cha chai
Pilipilu ya unga nyekundu - 1 kijiko cha chai
Mtindi /yoghurt - 3 vijiko vya supu
Mafuta ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele, roweka. Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli. Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu. Punguza mchanganyiko kidogo weka kando. Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi. Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive. Epua, weka kando. Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando. Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali. Tia kuku uchaganye vizuri. Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja. Punguza masala nusu yake weka kando. Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali. Funika upike katika oveni hadi uive. Changanya unapopakua katika sahani.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).
Mahitaji
Kuku mzima Nyanya kubwa 3 Karoti mbili Pilipili hoho Kotmiri Tangawizi Kitunguu maji Kitunguu saumu kidogo Ndimu Mafuta ya kupikia Chumvi (pilipili ukipenda)
Matayarisho
1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja. 2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu). 3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni. 4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni. 5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni. 6. Andaa kikaango na jiko.
Mapishi
1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui). 2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi. 3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana. 4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako. 5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu. Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.
Jinsi ya kupika Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe 2 ¼
Siagi 250g
Sukari kukaribia kikombe ½ (au takriban vijiko 10 vya kulia)
Baking powder ½ kijiko cha chai
Ute wa yai 1
Vanilla 1 kijiko cha chai
Sukari Ya Kunyunyizia na rangi mbali mbali.
MATAYARISHO
Kagawa sukari katika vibakuli utie rangi mbali mbali uweke kando. Changanya siagi na sukari katika mashine ya kusagia keki upige mpaka ilainike iwe nyororo. Tia ute wa yai vanilla uhanganye vizuri. Tia unga na baking powder kidogo kidogo uchanganye upate donge. Sukuma donge ukate kwa kibati cha shepu ya kopa. Pakaza siagi katika treya ya kupikia kwenye oveni upange biskuti Nyunyizia sukari za rangi rangi kisha pika katika oven moto mdogo wa baina 180 – 190 deg F kwa takriban robo saa. Epua zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 2 Vikombe
Cocoa ya unga - 1 Kijiko cha supu
Sukari ya hudhurungi - 1 Kikombe
Siagi - ¾ Kikombe
Yai - 1
Molasses - ¼ Kikombe
Baking soda - 2 vijiko vya chai
Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu
Karafuu ya unga - ½ kijiko cha chai
Chumvi ½ kijiko cha chai
Vanilla ½ kijiko cha chai
MAANDALIZI
Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando. Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti. Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili. Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri. Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike. Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri. Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.) Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka
Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.
Oka katika oven 350ºF kwa muda wa dakika 15.
Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi. Panga kwenye sahani tayari kuliwa.
Karibu kwenye makala yetu ya "Vidokezo 10 vya Vitafunio visivyo na Karanga"! 🥳🍿🍓🥕 Je, wewe ni mpenzi wa vitafunio bora na lishe? Ikiwa ndivyo, basi hii ni kwa ajili yako! Tumekusanya mapishi yenye ladha kubwa na mbadala wa karanga 😋🥜 Unachotakiwa kufanya ni kubonyeza na kusoma zaidi! Maskio yako yanasikia raha? 🎉 Usikose fursa hii kubwa ya kuburudika kwa lishe ya afya. Tembelea sasa ili kugundua vitafunio vipya na vya kushangaza! 💪🌽🥑🍌 Soma, jaribu, na furahiya! 📚🤩
Updated at: 2024-05-25 10:22:24 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vidokezo 10 vya Vitafunio visivyo na Karanga 🥜🚫
Kama unapenda kufurahia vitafunio na unakabiliwa na mzio wa karanga, basi hii ni makala sahihi kwako! Leo, kama AckySHINE, ningependa kushiriki nawe vidokezo 10 vya vitafunio visivyo na karanga ambavyo utaweza kufurahia bila wasiwasi wowote. Tuko pamoja kwenye safari hii ya kufurahia vitafunio bila kujali msongamano wa mzio. Hebu tuanze! 💪😄
🍓 Matunda yaliyokaushwa: Matunda yakiwa yamekaushwa ni chaguo bora la vitafunio vya afya. Unaweza kuchagua matunda kama tini, zabibu, na apple zilizokaushwa. Ni vitafunio vya asili na vyenye ladha tamu na bora.
🥕 Mboga mboga za chumvi: Badala ya vitafunio vyenye mafuta mengi, jaribu mboga mboga za chumvi kama vile karoti, matango, na pilipili mboga. Ni vitafunio vya chini katika kalori na vyenye virutubisho vingi muhimu kwa afya yako.
🍿 Popcorn: Ni vitafunio maarufu sana na vinapatikana kwa urahisi. Unaweza kununua popcorn zilizopikwa tayari au kutengeneza mwenyewe nyumbani. Kumbuka kutumia mafuta ya kupikia ya afya kama vile mafuta ya mzeituni au ya alizeti.
🍌 Ndizi: Ndizi ni vitafunio vyenye ladha tamu na vinafaida nyingi za kiafya. Unaweza kuchukua ndizi kama vitafunio vyako vya asubuhi au jioni. Pia, unaweza kujaribu kuongeza chaguzi zingine kama ndizi iliyochomwa au ndizi iliyokatwa na kuongeza juisi ya limao juu yake.
🥚 Mayai: Mayai ni chaguo bora la vitafunio visivyo na karanga. Unaweza kuwapika kukawa mayai ya kuchemsha au kukaanga. Pia, unaweza kuchanganya mayai na mboga mboga kama vitafunio vya kuchoma kwa afya.
🥨 Mikate ya kusaga: Mikate ya kusaga ni chaguo bora la vitafunio vinavyotumika kila wakati. Unaweza kupaka jibini ya cheddar au mchuzi wa nyanya juu yake. Ni vitafunio vyenye ladha tamu na rahisi kubeba popote uendapo.
🥦 Korosho: Korosho ni vitafunio vingine vyenye ladha nzuri na vinafaida nyingi za kiafya. Unaweza kuchagua korosho zisizosindikwa au zilizopikwa kwa mafuta kidogo. Ni chaguo nzuri la vitafunio vya kati na vyenye chumvi kidogo.
🍎 Kabeji za kukaanga: Kabeji za kukaanga ni chaguo bora la vitafunio vya afya. Unaweza kukata kabeji vipande vidogo na kuzikaanga kwenye mafuta kidogo. Kabeji ina kiwango kidogo cha kalori na ina virutubisho vingi muhimu kwa afya yako.
🍇 Embe: Tunda hili tamu linapatikana kwa urahisi na ni chaguo nzuri la vitafunio visivyo na karanga. Unaweza kula embe kama vitafunio vyako pekee au kuchanganya na matunda mengine katika smoothie ya asubuhi.
🍪 Biskuti visivyo na karanga: Soko limejaa biskuti zilizotengenezwa kwa ajili ya watu wenye mzio wa karanga. Unaweza kujaribu biskuti zilizotengenezwa kwa kutumia mafuta ya alizeti au mafuta ya kokoa badala ya mafuta ya karanga. Ni vitafunio vya afya na vyenye ladha nzuri.
Kwa hiyo, kama AckySHINE, napenda kukuhimiza kufurahia vitafunio bila wasiwasi wa mzio wa karanga. Kuna chaguzi nyingi nzuri huko nje ambazo utaweza kufurahia bila wasiwasi wowote. Kumbuka daima kusoma maelezo ya viungo kabla ya kununua vitafunio ili kuhakikisha hakuna karanga yoyote iliyomo.
Je, wewe ni mpenzi wa vitafunio? Ni vitafunio gani visivyo na karanga unapenda? 😊
Updated at: 2024-05-25 10:23:06 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - Vikombe 2
Samli au shortening ya mboga - 2 Vijiko vya supu
Maziwa ¾ Kikombe
Iliki - Kiasi
Mafuta ya kukarangia Kiasi
VIAMBAUPISHI :SHIRA
Sukari - 1 Kikombe
Maji ¾ Kikombe
Vanila ½ Kijiko cha chai
Zafarani (ukipenda) - Kiasi
JINSI YA KUPIKA
Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya. Tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo lake. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.
Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ng’ombe
Updated at: 2024-05-25 10:37:39 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - Kisia
Nyama ng’ombe - ½ kilo
Pilipili ya kusaga - 1 kijiko cha chai
Tangawizi ya kusaga - 2 vijiko vya supu
Thomu (garlic/saumu) - 1 kijiko cha supu
Bizari mchuzi - 1 kijiko cha chai
Nazi ya unga (ukipenda kuongezea) - 2 vijiko cha supu
Chumvi - Kiasi
Ndimu - 1 kamua
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Weka nyama ng’ombe katika sufuria, tia tangawizi, thomu, pilipili mbichi, bizari, chumvi. Roweka kidogo ukipenda kisha ikaushe yenyewe kwa maji yake Ongezea maji ya kiasi yasizidi mno, kisha funika na chemsha. Menya ndizi, ukatekate. Nyama ikikaribia kuiva, weka ndizi uendelee kupika mpaka viive vyote. Tia nazi ya unga kidogo tu ukipenda. Koleza kwa bizari mchuzi, pilipili, na ndimu Epua mimina katika chombo cha kupakulia zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:05 (11 months ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mayai yaliochemshwa 4 Nyama ya kusaga robo kilo Kitunguu swaum Tangawizi Limao Chumvi Pilipili Breadcrambs Carry powder Binzari nyembamba ya unga Yai moja bichi Mafuta
Matayarisho
Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa