Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima na Uadilifu katika Familia: Kuunda Tabia ya Uaminifu

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima na Uadilifu katika Familia: Kuunda Tabia ya Uaminifu

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima na Uadilifu katika Familia: Kuunda Tabia ya Uaminifu

... Read More
Jinsi ya kueleza hisia zako kwa mke wako

Jinsi ya kueleza hisia zako kwa mke wako

Kueleza hisia zako kwa mke wako ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wenu na kujenga ufahamu wa kina... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kuwa na wazazi na familia na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kuwa na wazazi na familia na mpenzi wako

Kuwa na wazazi na familia na mpenzi wako ni jambo zuri sana. Hata hivyo, mara nyingine hutokea ch... Read More

Jinsi ya Kuelewa Mahitaji, Matakwa, na Maslahi ya Mke wako

Jinsi ya Kuelewa Mahitaji, Matakwa, na Maslahi ya Mke wako

Kuelewa mahitaji, matakwa, na maslahi ya mke wako ni muhimu sana katika kudumisha uhusiano wa afya n... Read More
Kuhamasisha Heshima na Uwiano katika Mahusiano ya Familia

Kuhamasisha Heshima na Uwiano katika Mahusiano ya Familia

Mahusiano ya familia ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Kuwa na heshima na uwiano ka... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Furaha na Ustawi wa Kila Mwanafamilia katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Furaha na Ustawi wa Kila Mwanafamilia katika Familia Yako

Karibu katika makala hii kuhusu kuweka kipaumbele cha furaha na ustawi wa kila mwanafamilia katik... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuwa na Urafiki katika Familia Yako

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Kuwa na Urafiki katika Familia Yako

Kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kuwa na urafiki katika familia yako ni muhimu sana kwa afya ... Read More

Kufanya Mapenzi ya Kufurahisha na Mazoezi ya Kujiboresha: Jinsi ya Kufurahia Vyote

Kufanya Mapenzi ya Kufurahisha na Mazoezi ya Kujiboresha: Jinsi ya Kufurahia Vyote

  1. Kufanya mapenzi ni jambo muhimu katika uhusiano, lakini ni muhimu pia kujiboresha kiafy... Read More

Jinsi ya Kuweka mipaka na kuheshimu mipaka ya mpenzi wako

Jinsi ya Kuweka mipaka na kuheshimu mipaka ya mpenzi wako

Kuweka mipaka na kuheshimu mipaka ya mpenzi wako ni muhimu katika kujenga uhusiano mzuri na kuhakiki... Read More
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za binadamu na usawa

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za binadamu na usawa

Hivi unajua kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuzungumzia masuala ya haki za binadamu na usawa kwa mp... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kukuza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kukuza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha ushirikiano wa kielimu na kukuza maarifa katika familia ni muhimu sana katika kuhakik... Read More

Jinsi ya Kuendelea Kujifunza na Kukua katika Ndoa

Jinsi ya Kuendelea Kujifunza na Kukua katika Ndoa

Kuendelea kujifunza na kukua katika ndoa ni muhimu sana kwa ustawi wa uhusiano wenu na kujenga ndoa ... Read More