Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu matarajio ya baadaye na ndoto za kibinafsi ni muhimu katika kujeng... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kuheshimu matakwa ya kiroho na imani ya mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kuheshimu matakwa ya kiroho na imani ya mpenzi wako

  1. Tambua Imani Yake Ni muhimu kujua imani ya mpenzi wako ili uelewe matakwa yake ya kiroh... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya elimu na mafunzo

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya elimu na mafunzo

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya elimu na mafunzo inaweza kuwa ngumu sana. Lakini hak... Read More

Jinsi ya Kuwa Mfano wa Uvumilivu na Uwazi katika Familia: Kujenga Uhusiano Thabiti

Jinsi ya Kuwa Mfano wa Uvumilivu na Uwazi katika Familia: Kujenga Uhusiano Thabiti

Karibu katika makala hii ya jinsi ya kuwa mfano wa uvumilivu na uwazi katika familia, ili kujenga... Read More

Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kimapenzi kabla hajakwambia

Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kimapenzi kabla hajakwambia

Kujua kama mwanamke anakupenda kabla hajakwambia angalia dalili zifuatazo

Anafanya mambo ... Read More

Njia za Kuweka Kipaumbele cha Mawasiliano ya Wazi na Uaminifu katika Familia

Njia za Kuweka Kipaumbele cha Mawasiliano ya Wazi na Uaminifu katika Familia

Kuweka kipaumbele cha mawasiliano ya wazi na uaminifu katika familia ni muhimu sana kwa ustawi wa... Read More

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya kimyakimya au ngono/kufanya mapenzi ya kelele?

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya kimyakimya au ngono/kufanya mapenzi ya kelele?

Je, watu wanapendelea ngono/kufanya mapenzi ya kimyakimya au ngono/kufanya mapenzi ya kelele? Hii... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki wa kifamilia

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki wa kifamilia

Karibu katika makala hii ambapo tutajadili kuhusu jinsi ya kusaidiana na mpenzi wako katika kujen... Read More

Jinsi ya Kuwa Mfano Bora katika Familia: Kuwa Mtu wa Kuigwa

Jinsi ya Kuwa Mfano Bora katika Familia: Kuwa Mtu wa Kuigwa

Karibu kwenye makala hii ya jinsi ya kuwa mfano bora katika familia yako. Kuwa mtu wa kuigwa ni m... Read More

Jinsi ya Kuonyesha upendo na heshima kwa mpenzi wako

Jinsi ya Kuonyesha upendo na heshima kwa mpenzi wako

Kuonyesha upendo na heshima kwa mpenzi wako ni muhimu katika kudumisha uhusiano mzuri na wa afya. Ha... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kimawazo na maadili na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kimawazo na maadili na mpenzi wako

Katika uhusiano, tofauti za kimawazo na maadili ni jambo ambalo linaweza kusababisha migogoro kat... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiuchumi na kifedha na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiuchumi na kifedha na mpenzi wako

Kwenye uhusiano, tofauti za kiuchumi na kifedha ni mojawapo ya masuala ambayo yanaweza kuwa na at... Read More