Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna umuhimu wa kufanya ngono/kufanya mapenzi kwa mara kwa mara katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kufanya ngono/kufanya mapenzi kwa mara kwa mara katika uhusiano?

Je, kuna umuhimu wa kufanya ngono/kufanya mapenzi kwa mara kwa mara katika uhusiano? Hili ndilo s... Read More

Njia za Kupata Msichana Mzuri wa Kuwa Naye Maisha Yote

Njia za Kupata Msichana Mzuri wa Kuwa Naye Maisha Yote

Njia za Kupata Msichana Mzuri wa Kuwa Naye Maisha Yote

Kila mwanamume anataka kupata msich... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Mahusiano ni s... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu ndoto na malengo ya kazi

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu ndoto na malengo ya kazi

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu ndoto na malengo yako ya kazi ni muhimu katika kujenga uelewa na u... Read More
Jinsi ya Kusaidia Watoto kujenga Ujuzi wa Kujitunza na Kuwa na Heshima

Jinsi ya Kusaidia Watoto kujenga Ujuzi wa Kujitunza na Kuwa na Heshima

Karibu kwenye makala hii! Leo, tutajadili jinsi ya kusaidia watoto kujenga ujuzi wa kujitunza na ... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kuheshimu na Kuelewa Tofauti katika Mahusiano

Kuweka Kipaumbele cha Kuheshimu na Kuelewa Tofauti katika Mahusiano

Mahusiano ni muhimu sana katika maisha yetu. Tunapowasiliana na watu wengine, tunapata nguvu na f... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya mazingira na utunzaji wa asili

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya mazingira na utunzaji wa asili

Katika dunia hii ya leo, utunzaji wa mazingira umekuwa suala muhimu sana kwa kila mtu. Tunahitaji... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipango ya muda mrefu

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipango ya muda mrefu

Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipango ya muda mrefu ni muhimu katika kuweka ... Read More
Jinsi ya Kukabiliana na Mazoea Mabaya katika Familia: Mabadiliko na Ukuaji

Jinsi ya Kukabiliana na Mazoea Mabaya katika Familia: Mabadiliko na Ukuaji

Karibu katika makala hii inayozungumzia jinsi ya kukabiliana na mazoea mabaya katika familia. Kam... Read More

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

Kuweka Mazingira ya Kufurahisha na Amani katika Familia Yako

Kuishi katika familia yenye amani na furaha ni jambo la muhimu sana kwa afya na ustawi wa kila mm... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano ya Mbali

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano ya Mbali

Mahusiano ya mbali ni changamoto kubwa sana kwa watu wengi, haswa katika ulimwengu wa leo ambapo ... Read More

Jinsi ya Kuanzisha Mazungumzo ya Wazi kuhusu Kufanya Mapenzi na Mapenzi

Jinsi ya Kuanzisha Mazungumzo ya Wazi kuhusu Kufanya Mapenzi na Mapenzi

Kufanya mapenzi ni kitu ambacho wengi wetu tunakifurahia. Hata hivyo, ni muhimu kujadili kwa wazi... Read More