Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Featured Image

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.


Mambo hayo ni kama ifuatavyo;


Kupewa nafasi na kipaumbele.


Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.


 

Kuheshimiwa


Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.


Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa


Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.


 

Nafasi ya kuongea na kujieleza


Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.


 

Kusaidiwa katika shida na matatizo yao


Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.


Kubembelezwa


Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.






Mfahamu zaidi Mwanamke kwa Kupitia Kitabu hiki kizuri cha SIRI ZA MWANAMKE




[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kukuza Utatuzi wa Mizozo na Ushirikiano katika Familia Yako

Jinsi ya Kukuza Utatuzi wa Mizozo na Ushirikiano katika Familia Yako

Familia ni kitu muhimu sana katika maisha yetu. Hata hivyo, tofauti za kifikra, tabia, na mengine... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uaminifu katika Familia: Kuhamasisha Uaminifu na Urejesho

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uaminifu katika Familia: Kuhamasisha Uaminifu na Urejesho

Katika maisha yetu ya kila siku, tunakabiliana na changamoto mbalimbali katika familia zetu. Moja... Read More

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi? Hili ni swali ambalo linaweza kuwa na maji... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Mawasiliano ya Upendo katika Mahusiano yako

Kuweka Kipaumbele cha Mawasiliano ya Upendo katika Mahusiano yako

Mahusiano ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Kila mtu anataka kuwa na mtu wa kumpenda na kuwa na uh... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Kuweka Kipaumbele cha Ubora wa Mahusiano: Jinsi ya Kutunza Ushirikiano wako

Mahusiano ni s... Read More

Jinsi ya Kufanya Familia Yako Kuwa ya Kipekee na Bora Zaidi

Jinsi ya Kufanya Familia Yako Kuwa ya Kipekee na Bora Zaidi

Kila familia inahitaji kuwa na uhusiano thabiti na wa upendo ili iweze kukua na kuwa bora. Ni muh... Read More

Kuhamasisha Kujitambua na Kujielewa katika Mahusiano

Kuhamasisha Kujitambua na Kujielewa katika Mahusiano

  1. Kujitambua na Kujielewa ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Kujitambua kunamaanisha ... Read More

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ushawishi na Msichana katika Uhusiano

Leo tutazungumzia njia za kujenga ushawishi na msichana katika uhusiano. Kujenga ushawishi kunama... Read More

Upendo na Kufanya Mapenzi: Tofauti na Uhusiano wao

Upendo na Kufanya Mapenzi: Tofauti na Uhusiano wao

  1. Upendo na kufanya mapenzi ni vitu viwili tofauti katika uhusiano. Upendo ni hisia za ki... Read More

Jinsi ya Kuanzisha Mawasiliano ya Kwanza na Msichana

Jinsi ya Kuanzisha Mawasiliano ya Kwanza na Msichana

Leo, tutazungumzia jinsi ya kuanzisha mawasiliano ya kwanza na msichana. Ni muhimu sana kwa kila ... Read More

Jinsi ya Kuimarisha maisha ya ngono na intimiteti katika uhusiano na mpenzi wako

Jinsi ya Kuimarisha maisha ya ngono na intimiteti katika uhusiano na mpenzi wako

Kuimarisha maisha ya ngono na intimiteti katika uhusiano wako ni muhimu kwa afya na furaha ya wote. ... Read More
Je, kuna mambo mazuri na mabaya kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo mazuri na mabaya kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo mazuri na mabaya kuhusu ngono/kufanya mapenzi? Ndio, kuna mambo mengi sana ambayo ... Read More