Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS💌💕
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Featured Image

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.


Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.


Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.


Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: “Sasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.”


Akajibu: “Mimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.”
.
.
.


FUNZO:


Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.


Meno huung’ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.


1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.


2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.


3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.


Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.


Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.


*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.


Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!






Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke





Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.





[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kujenga Heshima na Uthamani katika Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kujenga Heshima na Uthamani katika Ndoa na mke wako

Kujenga heshima na uthamani katika ndoa na mke wako ni muhimu sana kwa ustawi wa uhusiano wenu. Hapa... Read More

Mbinu za Kujenga Upendo na Shukrani Ndani ya Familia: Mwongozo wa Mtaalamu

```html

Njia za Kujenga Utamaduni wa Upendo na Shukrani Ndani ya Familia: Msingi wa Furaha na Ms... Read More

Dalili za mahusiano feki, mahusiano ya kichina

Dalili za mahusiano feki, mahusiano ya kichina

Ukitaka kujua Simu ya Kichina utajua tu jinsi ilivyo na makelele mengiiiii sana wakati wa kuita... Read More

Je, watu wana amini nini katika kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wana amini nini katika kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi?

Je, umewahi kujiuliza watu wana amini nini katika kutumia vifaa vya ngono/kufanya mapenzi? Kuna m... Read More

Jinsi Kuaminiana na Kuwa Wazi katika Mahusiano yako na mke wako

Jinsi Kuaminiana na Kuwa Wazi katika Mahusiano yako na mke wako

Kuaminiana na kuwa wazi ni msingi muhimu wa mahusiano imara na yenye furaha na mke wako. Hapa kuna n... Read More
Jinsi ya Kuelewa na kuheshimu mipaka ya kifamilia na urafiki na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kuheshimu mipaka ya kifamilia na urafiki na mpenzi wako

Kuelewa na kuheshimu mipaka ya kifamilia na urafiki ni muhimu katika kudumisha uhusiano mzuri na mpe... Read More
Jinsi ya Kuonyesha upendo na heshima kwa mpenzi wako

Jinsi ya Kuonyesha upendo na heshima kwa mpenzi wako

Kuonyesha upendo na heshima kwa mpenzi wako ni muhimu katika kudumisha uhusiano mzuri na wa afya. Ha... Read More
Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Uwazi katika Familia: Kuweka Nafasi ya Mazungumzo na Ufahamu

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Uwazi katika Familia: Kuweka Nafasi ya Mazungumzo na Ufahamu

  1. Familia ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu na inaweza kuathiri sana maendeleo yet... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Kuimarisha ushirikiano wa kijamii na familia ni muhimu sana katika kuendeleza mahusiano yenye fur... Read More

Jinsi ya Kuimarisha Nguvu ya Ushawishi na Utamu wa Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuimarisha Nguvu ya Ushawishi na Utamu wa Ndoa na mke wako

Kuimarisha nguvu ya ushawishi na utamu wa ndoa na mke wako ni muhimu katika kuendeleza uhusiano imar... Read More
Jinsi ya Kuwa na Mipango ya Baadaye katika Familia: Kuweka Maono ya Pamoja

Jinsi ya Kuwa na Mipango ya Baadaye katika Familia: Kuweka Maono ya Pamoja

  1. Kuanzisha mawasiliano ya wazi: Ili kuweza kufikia malengo ya pamoja kama familia, ni mu... Read More

Jinsi ya Kuishi kwa Amani na Ndugu: Kuepuka Migogoro na Kutunza Uhusiano

Jinsi ya Kuishi kwa Amani na Ndugu: Kuepuka Migogoro na Kutunza Uhusiano

  1. Jifunze kuwasiliana: Mawasiliano ni ufunguo wa uhusiano mzuri. Hakikisha unawasiliana k... Read More