Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kwa nini jamii inatuchukia sisi Albino?

Featured Image

Siyo watu wote katika jamii wanawachukia au kuwatenga Albino.
Wazazi, ndugu zenu, rafiki zenu wanawapenda na kuwajali. Ni
jambo la kawaida kwa watu wa aina fulani kuwakataa au kuwakwepa
wale ambao wanaonekana tofauti na wao. Kwa mfano, katika jamii
ya watu weupe ni kawaida kuwakwepa au kuwakataa wale wenye
rangi nyeusi na hivyo ndivyo ilivyo pia kwa jamii ya watu weusi
kuwakataa au kuwakwepa watu weupe.
Jamii ya watu weusi huwaogopa, na hivyo huwakwepa Albino
kwa kuwa hawajui kilichotokea mpaka wakawa hivyo. Hali hiyo
inaimarishwa na uvumi potofu unaosambazwa kuwa ukimgusa
Albino unaweza ukageuka rangi ukawa mweupe au ukiwa na mimba
na ukamcheka au ukakutana na Albino, utazaa Albino. Ukweli ni
kwamba uvumi huu ni potofu na ni upuuzi mtupu. Ualbino ni hali
inayorithiwa na si ya kuambukizwa. Hakuna sababu ya kumuogopa
Albino. Mtazamo hasi wa jamii unaweza kubadilishwa endapo watu
watakuwa na ufahamu zaidi kuhusu ualbino na wanapowafahamu
watu wa aina hii vizuri zaidi kwamba ni watu wakarimu na wenye
urafiki. Na wewe unaweza ukachangia katika kuendeleza uelewa
huu kama utashiriki na watu kwa urafiki na kwa uwazi.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Msaada juu ya ukeketaji

Msaada juu ya ukeketaji

Unaweza ukajaribu kuzungumza na wazazi wako kwamba
ukeketaji ni desturi mbaya, na pia unawez... Read More

Je, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga shahawa bila shida, inawezekana kwamba ni mgumba?

Je, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga shahawa bila shida, inawezekana kwamba ni mgumba?

Ndiyo, mwanaume ambaye ana uwezo wa kumwaga mbegu bila shida anaweza kuwa mgumba. Kutokuwa mgumba... Read More

Je, mvulana afanye nini ili kuzuia ndoto nyevu?

Je, mvulana afanye nini ili kuzuia ndoto nyevu?

Ndoto nyevu ni kitu kinachowatokea vijana wakiwa usingizini. Haiwezekani kuzuiwa kwa sababu uko usin... Read More
Je, ngono/kufanya mapenzi ni jambo la faragha au unajisikia huru kuzungumzia kuhusu hilo?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni jambo la faragha au unajisikia huru kuzungumzia kuhusu hilo?

Jambo la faragha kabisa ni ngono au kufanya mapenzi. Kila mtu ana hisia tofauti kuhusu suala hili... Read More

Je, kwa nini watu waanzao kutumia dawa za kulevya hupenda kuendelea kuzitumia?

Je, kwa nini watu waanzao kutumia dawa za kulevya hupenda kuendelea kuzitumia?

Hii ndio hasa sababu kwa nini dawa za kulevya ni hatari! Mara unapozizoea unakuwa na ugumu wa kue... Read More

Je, kuna tofauti za umri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za umri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za umri katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio, kuna tofauti nyingi sana! Hiyo ndiyo... Read More

Kwa nini watu wanakunywa pombe?

Kwa nini watu wanakunywa pombe?

Unywaji wa pombe ni sehemu ya utamaduni wa Tanzania na nchi
nyinginezo duniani.

Watu h... Read More

Njia za Kupunguza Mvutano katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kupunguza Mvutano katika Uhusiano wako na Msichana

Katika uhusiano wowote, mvutano ni jambo ambalo huwezi kuliepuka. Hata kama mna furaha nyingi pam... Read More

Mambo usiyoyajua kuhusu mimba na wasichana

Mambo usiyoyajua kuhusu mimba na wasichana

Je, mimba hupatikanaje?

Ukitaka kuelewa jinsi mimba i inavyopatikana, lazima uelewe mzung... Read More

Inawezekana msichana akapata mimba kabla ya kuvunja ungo?

Inawezekana msichana akapata mimba kabla ya kuvunja ungo?

Msichana anaweza kupata mimba kabla ya kuvunja ungo, yaani kabla ya kuona hedhi kwa mara ya kwanz... Read More

Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hukufanya uwe na nguvu?

Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hukufanya uwe na nguvu?

Si kweli kabisa! Baada ya kuvuta bangi mtu hujiona kama jasiri sana na mwenye nguvu. Lakini madha... Read More

Je , vipimo vya Virusi vya UKIMWI vinasema ukweli?

Je , vipimo vya Virusi vya UKIMWI vinasema ukweli?

Uwezekano wa kupata majibu ya uwongo ni mdogo sana, isipokuwa tu kama vipimo vitafanyika kipindi ... Read More