Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Nimwambie nini mtu anayejaribu kunishawishi nijihusishe na makundi ya watu wanaokunywa pombe na wavutaji sigara?

Featured Image

Kama umeamua kutovuta sigara wala kunywa pombe ni uamuzi
mzuri sana na wa kiafya. Ni haki yako binafsi kuchukua uamuzi
huu, kama vile watu wengine pia wanavyoruhusiwa kufanya
maamuzi kuhusu maisha yao wenyewe.

Mara nyingine ni vigumu sana, lakini kama umeamua hutaki
kujiunga na kundi la watu wavutao sigara au kunywa pombe ni
muhimu kusema hivyo. Jaribu kuwa wazi na kusema HAPANA.
Jaribu kueleza kwamba unataka kuishi maisha yenye afya bila
kutumia pombe na sigara na uwaeleze rafiki zako ni kwa nini.
Waambie kuwa unajua unachokifanya na kwamba umeridhika
kuwa uvutaji sigara na unywaji pombe unahatarisha afya yako,
unagharimu fedha nyingi na kukuzuia kufikia malengo yako.
Kama umeridhika na kuwathibitishia watu hao, hawatakusumbua
tena. Na kama unatafuta rafiki usisahau: Rafiki ni mtu anayejali,
kulinda na kuthamini maisha ya mwenzake! Kwa hivyo, ni kwa
vipi mtu ambaye anayekushawishi ufanye kitu cha kudhuru
afya yako kwa kusudi na haheshimu maamuzi yako awe rafiki
wa kweli?

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Vidonge vya Kuzuia Mimba

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Vidonge vya Kuzuia Mimba

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Vidonge vya Kuzuia Mimba 😊

Karibu... Read More

Kwa nini ngozi ya Albino inafanana ya watu weupe?

Kwa nini ngozi ya Albino inafanana ya watu weupe?

Ngozi ya Albino ina ukosefu wa rangi. Inaonekana kama ya watu
weupe ambao wana kiasi cha pig... Read More

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu dini na imani za mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu dini na imani za mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu dini na imani za mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenz... Read More

Njia za Kujenga Ukaribu wa Kiroho na Msichana katika Uhusiano

Njia za Kujenga Ukaribu wa Kiroho na Msichana katika Uhusiano

Kujenga ukaribu wa kiroho na msichana katika uhusiano ni jambo muhimu sana. Uhusiano wa kimapenzi... Read More

Kuna athari gani za mimba za utotoni hasa kwa kijana Albino?

Kuna athari gani za mimba za utotoni hasa kwa kijana Albino?

Katika masuala ya athari za mimba katika umri mdogo ni
kwamba vijana Albino hawana tofauti n... Read More

Je, Ni Sahihi Kuanza Kujihusisha na Ngono nikiwa na Mpenzi Wangu?

Je, Ni Sahihi Kuanza Kujihusisha na Ngono nikiwa na Mpenzi Wangu?

Je, Ni Sahihi Kuanza Kujihusisha na Ngono nikiwa na Mpenzi Wangu? πŸ€”

Jambo zuri kujiuliz... Read More

Dawa za kulevya ni nini?

Dawa za kulevya ni nini?

Tunaposema dawa za kulevya ina maana ni matumizi mabaya ya dawa na hasa pale yatumikapo kinyume c... Read More

Je , vipimo vya Virusi vya UKIMWI vinasema ukweli?

Je , vipimo vya Virusi vya UKIMWI vinasema ukweli?

Uwezekano wa kupata majibu ya uwongo ni mdogo sana, isipokuwa tu kama vipimo vitafanyika kipindi ... Read More

Kuna fikra kuwa Albino ni watu wa kawaida je, kisayansi hii ni kweli?

Kuna fikra kuwa Albino ni watu wa kawaida je, kisayansi hii ni kweli?

Hii ni kweli kabisa. Watu wanaoishi na ualbino ni watu wa
kawaida kama binadamu wengine wote... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Mapenzi kwa Msichana Wako

Jinsi ya Kuonyesha Mapenzi kwa Msichana Wako

Leo tutazungumzia juu ya jinsi ya kuonyesha mapenzi kwa msichana wako. Ingawa kuna njia nyingi to... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Uaminifu katika Uhusiano wako na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uaminifu katika Uhusiano wako na Msichana

Uaminifu ni tabia muhimu sana katika uhusiano wako na msichana. Kama unataka uhusiano wako ufanye... Read More

Dalili za kwanza za msichana au mwanamke kuwa na mimba ni zipi?

Dalili za kwanza za msichana au mwanamke kuwa na mimba ni zipi?

Dalili moja i iliyo wazi zaidi ni kukosa hedhi. Mwanamke akijamii ana na mwanaume bila kutumia kinga... Read More