Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Je, kwa nini unasema kwamba wasichana vijana hawapo tayari kubeba mimba?

Featured Image

Ni kweli kwamba kupata hedhi ni dalili ya mwili wa msichana kuwa tayari kwa kubeba mimba, lakini kupata hedhi hakuna maana kwamba msichana yupo tayari kwa kuanza kujamii ana au kubeba mimba. Uke wa mwanamke ambaye ni mtu mzima ni madhubuti na unavutika, lakini uke wa msichana ni mwembamba na hauwezi kutanuka sana. Hivyo uke wa msichana unaweza kuchanika vibaya wakati wa kujifungua. Vilevile nyonga ya msichana huwa bado nyembamba sana kuweza kumpitisha mtoto wakati wa kujifungua.
Kwa kuongezea, kupata mtoto siyo suala tu la mwili kuwa tayari kubeba mimba na kujifungua. Inamaanisha pia kuwa tayari kuwa na mwenzio wa kushirikiana naye katika malezi ya mtoto, kuwa na kipato cha kutosha cha kutunza familia na kuwa na nyumba ya kuishi. Kwa vyovyote vile kubeba mimba mapema kunamkosesha msichana kuendelea na masomo na hivyo kumyima nafasi nyingi nzuri za mafanikio.
Hivyo kupata hedhi kila mwezi ni dalili tu ya kuelekea kwenye utu uzima. Haimaanishi kwamba mwili wake umekua vya kutosha kuweza kujifungua mtoto na haimaanishi kwamba amepanga maisha yake kikamilifu kuwa mzazi.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kukosa Ujasiri kuhusu Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kukosa Ujasiri kuhusu Ngono?

Nifanyeje Kukabiliana na Hisia za Kukosa Ujasiri kuhusu Ngono? 😊

Karibu kwenye makala h... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Kila siku, tunaishi katika jamii ambayo ina maadili na kanuni za kufuata katika uhusiano wa ngono... Read More

Je, Ni Vipi Kuepuka Shinikizo la Kufanya Ngono Katika Mahusiano?

Je, Ni Vipi Kuepuka Shinikizo la Kufanya Ngono Katika Mahusiano?

Je, Ni Vipi Kuepuka Shinikizo la Kufanya Ngono Katika Mahusiano? 😊

Kuwa na nguvu ya kue... Read More

Je, kama mwanamke na mwanaume wanapata watoto wa jinsia moja tu, ni kosa la nani?

Je, kama mwanamke na mwanaume wanapata watoto wa jinsia moja tu, ni kosa la nani?

Hakuna mwenye kosa, kwa sababu jinsia ya mtoto i inategemea na bahati na hamna uwezekano wa kupan... Read More

Je, baada ya kutumia vidonge au sindano kwa muda mrefu, mwamamke akiacha kuzitumia hizo njia ataweza kupata mimba tena?

Je, baada ya kutumia vidonge au sindano kwa muda mrefu, mwamamke akiacha kuzitumia hizo njia ataweza kupata mimba tena?

Vidonge na sindano zinazuia mimba kwa kuzuia yai lisipevuke. Akitumia njia hizi za kuzuia mimba, ... Read More

Je, unaweza kufa ukitumia dawa za kulevya?

Je, unaweza kufa ukitumia dawa za kulevya?

Ndiyo, unaweza. Kifo kinaweza kuwa cha ghafla au
kutokana na madhara ya muda mrefu katika vi... Read More

Je, kuna tofauti za kimwili katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kimwili katika ngono/kufanya mapenzi?

Mapenzi ni sehemu muhimu katika maisha ya binadamu na inaweza kuwa njia ya kujifunza, kufurahia, ... Read More

Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI vinaambukiza kwa kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni?

Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI vinaambukiza kwa kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni?

Ndiyo, kuna hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI wakati wa kujamii ana kwa nji... Read More

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu dini na imani za mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu dini na imani za mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuelewa na kuheshimu dini na imani za mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenz... Read More

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?

Ni katika umri gani vijana wana haki ya kutumia huduma za afya ya uzazi na njia za uzazi wa mpango?

Hakuna kiwango cha umri kwa kutumia huduma za afya ya uzazi
na njia za uzazi wa mpango. Unat... Read More

Kwa nini Albino wanatengwa katika masuala ya mapenzi na wale watu ambao siyo Albino?

Kwa nini Albino wanatengwa katika masuala ya mapenzi na wale watu ambao siyo Albino?

Watu huogopa kujaribu vitu au mambo ambayo hawajayazoea
au yale ambayo yapo tofauti. Jinsi u... Read More

Je, nini imani ya watu katika kufanya mazoezi ya kujenga ujasiri wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, nini imani ya watu katika kufanya mazoezi ya kujenga ujasiri wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Leo tutazungumzia jambo la muhimu sana, ambalo ni kujenga ujasiri wakati wa ngono. Hivi karibuni,... Read More