Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.
Nini husababisha.
Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.
2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k
3. Msongo wa mawazo na hasira.
4. Kula haraka haraka na kula unaongea.
5. Uvutaji wa Sigara
6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.
Jinsi ya kujitibu.
Β· Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.
Β· Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.
Β· Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula
Β· Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.
Β· Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.
Β· kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.
Β· Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.
Β· Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.
Β· Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.
Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.
Related Posts
Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao y...
Read More
Kulingana na baadhi ya chunguzi zilizofanywa na wanasayansi asilimia 60 β 70 ya wanaume hupotez...
Read More
Leo nimekuletea matumizi ya mbegu ya parachichi yenyewe yaani ile inayokuwa katikati ya tunda la ...
Read More
Nichukue wasaa huu kukuarika rasmi ewe mpenzi na mfuatiliaji wa blog hii ya Muungwana blog, naomba n...
Read More
Faida kuu za ukwaju ni kama ifuatavyo:
Huondoa sumu Mwilini
Chanzo kizuri cha viua ...
Read More
Masaji uongeza kinga ya mwili
Masaji kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambuki...
Read More
- Mafuta ya zeituni
- Mafuta ya nazi
- Samaki
- Binzari
- Mayai
Read More
Dengue ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na kuambatana na maumivu makali. Kwa sasa hakuna ...
Read More
Unahitaji vitu vifuatavyo:
a)Binzari ya unga
b)Maziwa fresh
c)Asali
d)Baku...
Read More
Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kwamba watu wazima wasiovuta sigara lakini walipokuw...
Read More
Ukwaju ni tunda maarufu sana ambalo hupatikana katika maeneo yenye uoto wa kitropiki. Kwa kingere...
Read More
Kuna wakati mwanaume huweza kupata maumivu ya korodani, ambapo inawezekana ikawa ni maumivu kwa k...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!