Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Kujenga Mazingira ya Upendo na Kujali katika Familia Yako

Kujenga Mazingira ya Upendo na Kujali katika Familia Yako

Familia ni moja ya mazingira muhimu kuliko yote katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunakulia, t... Read More

Jinsi ya Kusaidia Watoto kujenga Uhusiano wa Karibu na Wazee: Kuheshimu na Kujali

Jinsi ya Kusaidia Watoto kujenga Uhusiano wa Karibu na Wazee: Kuheshimu na Kujali

Leo hii tutaangazia jinsi ya kusaidia watoto kujenga uhusiano wa karibu na wazee. Kwa kawaida, wa... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiutamaduni na maadili katika mahusiano na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiutamaduni na maadili katika mahusiano na mpenzi wako

Mahusiano ni jambo la muhimu sana katika maisha yetu na wengi wetu tunataka kuwa na uhusiano mzur... Read More

Njia za Kuboresha Uhusiano wa Kufanya Mapenzi: Ushirikiano na Mazungumzo

Njia za Kuboresha Uhusiano wa Kufanya Mapenzi: Ushirikiano na Mazungumzo

Njia za Kuboresha Uhusiano wa Kufanya Mapenzi: Ushirikiano na Mazungumzo

Kufanya mapenzi k... Read More

Jinsi ya Kujenga na kudumisha urafiki na mpenzi wako

Jinsi ya Kujenga na kudumisha urafiki na mpenzi wako

Kujenga na kudumisha urafiki mzuri na mpenzi wako ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wenu. Hapa ku... Read More
Je, ni muhimu kuzungumzia kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi kabla ya kuingia katika uhusiano?

Je, ni muhimu kuzungumzia kuhusu upendeleo wako wa ngono/kufanya mapenzi kabla ya kuingia katika uhusiano?

Je, ni muhimu kuzungumzia upendeleo wako wa ngono kabla ya kuingia katika uhusiano? Jibu ni ndio!... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Mawasiliano na Kuwa na Mipasuko katika Familia Yako

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Mawasiliano na Kuwa na Mipasuko katika Familia Yako

Karibu katika makala yetu inayojadili njia za kupunguza mazoea ya kukosa mawasiliano na kuwa na m... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kuwa na wazazi na familia na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kuwa na wazazi na familia na mpenzi wako

Kuwa na wazazi na familia na mpenzi wako ni jambo zuri sana. Hata hivyo, mara nyingine hutokea ch... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kuishi kwa sasa na kuthamini maisha ya pamoja

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kuishi kwa sasa na kuthamini maisha ya pamoja

Kusaidiana na mpenzi wako katika kuishi kwa sasa na kuthamini maisha ya pamoja ni njia nzuri ya kuim... Read More
Kuwa na Wazi kuhusu Matumizi ya Dawa katika Kufanya Mapenzi: Mwongozo na Mjadala wa Kimahusiano

Kuwa na Wazi kuhusu Matumizi ya Dawa katika Kufanya Mapenzi: Mwongozo na Mjadala wa Kimahusiano

Kuwa na Wazi kuhusu Matumizi ya Dawa katika Kufanya Mapenzi: Mwongozo na Mjadala wa KimahusianoRead More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Kuimarisha ushirikiano wa kijamii na familia ni muhimu sana katika kuendeleza mahusiano yenye fur... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kufurahia Kila Siku katika Familia Yako

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kufurahia Kila Siku katika Familia Yako

Kuwa na familia yenye ushirikiano na furaha ni jambo muhimu sana katika maisha. Kwa kufanya hivyo... Read More