SALA YA IMANI
Mungu wangu, nasadiki maneno yote linalosadiki na linalofundisha kanisa katoliki la Roma; Kwani ndiwe uliyefundisha hayo, wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina
Mungu wangu, nasadiki maneno yote linalosadiki na linalofundisha kanisa katoliki la Roma; Kwani ndiwe uliyefundisha hayo, wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina
Ee Yesu Mfungwa wa Upendo wa Mungu,/ ninapofikiri Upendo wako na jinsi ulivyojitolea kwa ajili yangu,/ nashindwa kuelewa./ Unaficha Ukuu wako usiofahamika/ na kujidhihirisha kwa ajili yangu mimi mnyonge./ Ee Mfalme wa utukufu,/ unaficha uzuri wako,/ lakini jicho la moyo wangu/ linapenya pazia na kuona Majeshi ya Malaika/ wakikuimbia kwa heshima bila kukoma/ na nguvu zote mbinguni zikikusifu bila mwisho zikisema:/ “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu..”/
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya cho chote, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina
Tumia Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria iliyo na mafungu 7 yaani mateso 7 yenye Salamu Maria saba kwa kila teso.
TESO LA KWANZA
Mzee Simeoni aliagua kuwa Moyo wa Mama Maria utachomwa kwa upanga.
Tuombe neema ya kuvumilia mateso.
Mama wa mateso utuombee.
Kwa njia ya Maji haya ya Baraka, na kwa njia ya Damu yako azizi, na kwa maombezi ya Moyo Safi wa Maria, unioshe na uovu wangu wote na uwasaidie roho zinazoteseka toharani. Amina.
Roho ya Kristo unitakase
Mwili wa Kristo uniokoe
Damu ya Kristo unifurahishe
Maji ya ubavu wake Kristo yanioshe
Mateso ya Kristo nguvu yanizidishie
Ee Yesu mwema unisikilize
Atukuzwe Baba
na Mwana
na Roho Mtakatifu
Kama mwanzo
na sasa,
na siku zote,
na milele.
Amina.
Rozari ya Malaika Mkuu Mikaeli ni sala nzuri sana ya kumheshimu huyu Malaika Mkuu pamoja na makundi yote tisa ya Malaika. Kuendana na jinsi tunavyofunuliwa katika Maandiko Matakatifu, makundi haya tofauti tofauti ya Malaika hujipanga kuanzia karibu sana na Kiti cha Enzi alipo Mwenyezi Mungu, kwenda chini tulipo sisi wanadamu
Enyi Yesu na Maria na Yosefu,nawatolea Moyo, na roho, na uzima wangu. Enyi Yesu na Maria na Yosefu, mnipokee saa ya kufa kwangu. Enyi Yesu na Maria na Yosefu, mnijalie nife mikoni mwenu.