SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye
Updated at: 2024-05-25 15:36:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
Updated at: 2024-05-25 15:36:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Katika maisha nimejifunza mambo mengi ikiwemo,. Kupendwa, kupenda, kusamehe, kuvumilia, lakini nimeshindwa kujifunza kukusahau wewe kwa sababu umekuwa ukinikumbuka sana.. nakutakia ASUBUHI NJEMA
SMS ya kumshukuru mpenzi wako na kumwambia kuwa unampenda
Updated at: 2024-05-25 15:26:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
nakupenda sana mpenzi wangu ,we ndo wa pekee mwenye kujua furaha ya moyo wangu nikiwa na majonzi huwa upo karibu nami,nikiwa na furaha huja kushea nami,ahsante wangu tabibu ,we ndo wangu wa manani.