Huyu mwanamke ni noma cheki alichomwambia mme wake baada ya kumnunulia nguo za ndani
Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazeni moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia. Mpenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka. MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili,
Updated at: 2024-05-25 18:13:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazeni moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia. Mpenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka. MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili,
Jamaa alifura akawa kama mbogo na hapo ndipo zogo kuu lilipoanza
Updated at: 2024-05-25 17:17:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ni noma!
Baada ya Talaka mke kamtumia mume meseji:- "Nasikitika kukujulisha kuwa binti uliyemlea kwa miaka 20 sio mtoto wako" Mume akamjibu:- "Duh! Nashukuru Mungu kwani nilikuwa nikiumia rohoni kila siku kwamba nazini na binti yangu" 😂😂😂😂😂😂😂😂😂 🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃
Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata
Updated at: 2024-05-25 17:49:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kubeba nauli kamili nayo ni shida Yani nimepanda daladala Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!
Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa
Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondoka…
Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka.
Updated at: 2024-05-25 18:13:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondoka…
Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: "kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.
Wanaume ni noma, Angalia wanachokifanyaga wakimwona mwanamke
Updated at: 2024-05-25 16:59:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wanaume ni viumbe WASTAARABU sana..Mdada anapokua kavaa BIKINI na BRA tu, 98% ya mwili wake unakuwa wazi…Sisi kwa USTAARABU huwa tunaangalia pale PALIPOFUNIKWA..Hatutaki Dhambi za Kijinga kabisa Sisi…
Huyu bwana leo kapatikana, Jamani nyodo nyingine mbaya
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja.
Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka.
Updated at: 2023-04-29 22:52:17 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja. Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka. Wakati mdada alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yupo busy na kuongea na simu ya umuhimu. Wakati anaongea na simu akisikika akisema No, No, No….. Absolutely No. Wajuulishe hao lay person wa New York kua siwezi kushuhulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million. Mimi ni profesional lawyer and im crossing the border to sarve international community.
Aka pose kidogo na akanywa maji kisha akaendelea….. Naweza kuanza kukusanya primary evidence next weak but tell them watume kwanza ten million kwa kuanza… Hahahahaha you dont know my Account Mr Roger. Ok waambie watume kwenye Account ileile walionitumia million 100 last month…
Aka pose tena akameza fundo la maji na kurekebisha tai yake kisha akaendelea… Ok usisahau kumueleza muendesha mashtaka mkuu wa marekani kua nitakuja New York mwezi ujao maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu mholanzi kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza.
Wakati anaongea hayo yote yule mdada alikua ametulia na anamuangalia Bwana Rwegashora anavyojizunguusha kwenye kiti chake huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu ya TTCL. Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia mdada mrembo.
Samahan sana kwa kukupotezea muda wako unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana ninapokea simu sana mpaka nimechoka na simu nyingi ni za wateja wa njee ya nchi.
Anyway nikusaidie nn? Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopita…!!!