Updated at: 2024-05-25 17:13:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) Mtoto…Mama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasa…..
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
"Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana."
Padri, "Endelea…"
Updated at: 2023-04-29 22:53:14 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani peke yake. Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama {confess} "Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana." Padri, "Endelea…"
"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa kufungwa. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?"
Padri: "Utasamehewa." "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona kilichotokea akasema anapiga polisi simu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?" Padri: "Utasamehewa."
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?" Padri:"Utasamehewa."
"Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua? Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?"
Kimyaa…. "Padri yesu atanisamehe?" kimya….
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, "Sasa baba mbona umekimbia?" Padri kwa taabu akajibu, "Nilitazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu……."
jamaa akagoma kwenda kazini 😬😬 mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwa nimemdhibiti ndo mana hatoki🚷 jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwa ulidhani rafiki yako kumbe adui yako🤔🤔 jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwa ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu