Jamaa kaingia Bar; Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Updated at: 2023-04-29 22:53:32 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Jamaa kaingia Bar; Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi. Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapoβ¦β¦.
Angalia alichokifanya huyu mtu baada ya kuokota wallet ya thamani
Updated at: 2024-05-25 17:15:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station "naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu" Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao "U SAVED ME" umfikie popote alipo!!
Updated at: 2024-05-25 17:46:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtalii: Do you have vegetables here. Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa. Waiter: Vijimeza vidogo hatuna. Mtafsiri: No sir, they don't have. Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs. Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto. Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa. Mtafsiri: They don't cook here Mtalii: What type of snacks do you have here. Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa, Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao. Mtafsiri: They don't cook any type of snacks here, maybe you can go back and eat at home. Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice. Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo. Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena sasa hivi kabla sijakasirika. Mtafsiri: Lets get out of here ππππππ Usicheke pekeyako
Updated at: 2024-05-25 17:17:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa alikuwa kwenye daladala pembeni kuna dada mrembo kakaa. Kamlia timing kwa muda kisha halafu akamuuliza "Samahani dada unaitwa Google?". Dada: "hapana, kwanini umedhani naitwa hivyo?". Jamaa: "Una kila kitu nnachokitafuta "π πππππππππ