Updated at: 2024-05-25 16:53:24 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
HAHAHAHAHAAAAAA DUH TAMAA MBAYA
Muokota makopo katika uokotaji wake wa makopo akaona chupa ambayo ndani kuna ki2, alipoifungua likatoka jitu la ajabu. Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vi2 viwili sasa hivi. Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari. Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka. Akaambiwa ombi la pili,akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada Hapohapo akageuzwa akawa chipsi yai.!!😂🤣🤣🤣
Updated at: 2024-05-25 18:09:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:
Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania. Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa: Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!
Updated at: 2024-05-25 18:10:15 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli. Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye…… Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji. "Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!" Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
"CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5"
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji. "BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI"
#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……
Updated at: 2024-05-25 17:10:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Boss;- kwa nini umechelewa kazini Juma;- kuna mtu njiani alidondosha elfu1 Boss;- ohhoh kwa hiyo ulikuwaunamsaidia kuitafuta Juma;- hapana nilikuwa nimeikanyaga