Updated at: 2024-05-25 18:10:22 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama mdaku alishangaa kila siku mchungaji anaingia nyumba ya jirani yake ambaye hana mume, akawa anajiuliza anakwenda kufanya nini? Uzalendo ukamshinda akamuuliza "Mwenzangu, mbona kila siku mchungaji anakuja kwako, vipi anakuja kukuombea?" Akajibiwa "Nyoo, umbea tu! Mbona kwako kila siku anakuja mwanajeshi kuna vita! chefuuuu π³π³π³π³π³
Updated at: 2024-05-25 17:59:16 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Huwa naenjoy sana kusoma yaliyoandikwa nyuma ya daladala hasa ninapokuwa kwenye foleni. Misemo maarufu ya kwenye daladala.
1.Yatima hadeki 2.Utamu wa chips mimba 3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni 4. Usiyempenda kaja 5. Kobe hapimwi joto 6. Acha kazi uone kaz kupata kaz 7. Ukichezea koki utalowa 8. Heshima pesa kipara kovu tu! 9. Mtumbwi hauna saitmira. 9. Silaha pesa bastola mzigo 10. Hata uoge mjini huendi 11. Chezea mshahara usichezee kazi. 12. Ukiona manyoya ujue kishaliwa 13. Ikisimama Panda 14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwebwe 15. Njia ya chooni haioti nyasi 16. Likizo ya maskini ugonjwa 17. When i grow up i want to be a scania 18. Hata bibi alikuwa binti 19. Kisigino hakikai mbele 20. Kama mapenz pesa kaolewe na benki 21. Hata barabara ina matuta lakin huwez panda viazi 22. Mavi hayana miba lakin ukikanyaga lazma uchechemee 23. Paka haishi kwa msela 24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa 25. NIPO NIPO KWANZA 26. Mchana nzi ucku mbu 27. Ucmshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake 28. Kama umelipenda(gari) bonyeza nyota liwe lako 29. Supermarket hawauzi mkaa 30. We nisubiri mi nakungoja. 31. Zetu dagaa kuku tamaa 32. Hata uwe na heshima vipi huwezi kumpokea askari bunduki H ππππππππππ
Updated at: 2024-05-25 17:07:17 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jana usiku kuna Jirani yangu..kanitumia text "mambo vipi?"β¦halafu tunakaa nae mtaa mmoja nikaona nikimjibu ni uharibifu wa hela nikaenda kumgongea mlango saa 7 usiku. Alipofungua nikamjibu "shwari"halafu nikarudi nyumbani kulala zangu..
Updated at: 2024-05-25 17:57:23 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake
anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke,
mkewe akakataa, akamwambia baba yake
akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa
babaake, mwisho babaake akamwambia basi
ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi
hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!
Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha
kikao cha ndugu wote pande 2,
Mzee akaanza kueleza jaman kijana wetu
anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital
zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga
wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa
atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye
ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu
alipoolewa ndo kijana wetu atapona!
Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii
kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote!
Je kina mama nani ataandaa? Walitoka nje
wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake
mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana,
mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia
wanaume peke yao! Mzee akamwambia
mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo?
Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani
umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
SOMA TENA KISHA MTUMIE NA MWENZIO.