Updated at: 2024-05-25 17:59:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.
Updated at: 2024-05-25 17:06:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.
Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza 🙆♂
Utajuaje kama unachoangalia ni filamu ya kibongo!!!!
Updated at: 2024-05-25 17:59:35 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Angalia hivi
-Mlinzi wa Getini lazima awe chizi -Mtu yupo kijijini, maisha magumu ana Wave kichwani. -Kama bosi atakuwa na kampuni basi ni lazima itakuwa ya Clearing and Forwading au ya uuzaji Magari. -Lazima waende Kununua nguo. -Jambazi lazima avae koti lefu jeusi na Miwani. -Mtu akichapwa kofi huangukia kwenye kochi ama kitandani. -Actress huwa hawapiki hata chai. -Kwa mdada akiishi maisha ya kitajiri lazima avae nguo inayoishia mapajani. -Actress even after 5 yeas utakuta staili ya nywele na rangi za kucha ni zile zile. -Anaweka Sumu alafu anaonja kama imekolea. -Movie zote wapenzi huitana Baby.. -Main actor wote ni wafanya biashara na lazima wataongelea mizigo kutoka bandarini. -Wakinywa Soda basi lazima wabakishe.
Updated at: 2024-05-25 17:11:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa. Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba. Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- "Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3." SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE
Updated at: 2023-04-29 22:52:30 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
STORY ZA WASICHANA KTK SIM
Mary… Hallow mpenzii Lily…. Niambie my dear Mary..Pouwaa za siku jamani Lily…Nzuri rafiki Yangu wa damu Mary…Jioni nakuja kwako tule Na kunywa japo wine wanguu Lily…Nakusubiri kwa hamuu mpenziiii
BAADA YA KUKATA SIMU…KILA MMOJA ANAWAZA
Lily…Huyu mchawi wa kike Leo anataka kuja kwangu wala hanikuti. Mary..Hahahahaaaa Uwiiiiiiiiii huyu kahaba eti nakusubir Kwa hamuu nani aende!!!
STORY ZA WAVULANA KATIKA SIMU
John…Niaje we mbwaa Sam…Pouwa kichaa wanguu John..Upo wap mpumbavu wewe Sam…Niko hom, we fala Uko wap? John..Baadae nakuibukia jambaz langu tukale bata Sawa… Pouwaa we ms**nge nakusubiri
BAADA YA KUKATA SIMU…KILA MMOJA ANAWAZA
John…Dah baadae nikakae na mwanangu Sam sijamuona long time Sam…John bwana akiwa Na pesa lazima anitafute mwanaeee.
FUNZO..
Baadhi ya Wasichana hujifanya wanapendana Kwa maneno lkn ni Kwa nje tu!! lkn WANACHUKIANA WAVULANA unaweza Kudhani hawapendani Kwa Maneno lkn WANAPENDANA..
Mpe TANO mchizi wako kudumisha upendo wetu wavulana… High 👊👊👊👊👊 boys
Soma huyu mtoto anachosema sasa, Ndoto za watoto bwana! Kazi ipo!
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
Updated at: 2023-04-29 22:53:28 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae. MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani? JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo. MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga. MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi. MWAL: Na wewe Nehemiah ?? Nehemiah : mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……" Akameza mate kisha akaendelea…. "Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali." MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani?? JENNY: Nataka kuwa mke wa Nehemiah .!!
Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu
Updated at: 2024-05-25 17:15:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem'bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika "NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU" 😂😂😂 Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapo *Sipendagi Ujinga mimi* 🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽
Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station
"Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…"
Updated at: 2024-05-25 18:04:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station
"Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…"
Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?
John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura "MAJANGA" umfikie popote pale alipo…!!!