Updated at: 2024-05-25 16:23:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hata kama utafanya kila kitu usibakwe bado inaweza ikatokea.
Ubakaji na unyanyasaji wa ujinsia unaweza kutokea kwa kila mtu.
Hata hivyo kuna baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kupunguza
hatari ya kubakwa.
Jizuie usiwe peke yako kwenye giza, kutembea peke yako
katika misitu au sehemu ambazo zina watu wachache, kuchota
maji sehemu ya mbali. Hakikisha kuwa kuna watu karibuni wa
kukusaidia iwapo kuna hatari. Pia jihadhari na watu walevi na
sehemu ya kunywea pombe maana watu walevi wanaweza wakawa
hatari. Iwapo umelazimika kufanya kazi katika mazingira
ya hatari, jaribu kujadili tatizo hili na wazazi wako au mtu
unayemwamini na muulize huyu mwanamume au mwanamke
azungumze na wazazi wako.
Usikubali zawadi au upendeleo, kama unafikiri unapewa wewe
kwa kubadilishana na ngono. Kama unajisikia unatishwa jaribu
kukimbia na piga kelele kwa kutafuta msaada mara moja.
Utafiti umeonyesha kuwa wasichana au wanawake ambao kwa
ushupavu wanasema hapana na ambao wanathubutu kupiga
kelele na kuvutia hisia za wengine wakati wanaposhambuliwa
wana hatari kidogo ya kubakwa. Unapokuwa unajitetea kwa
uhakika unapoanza unachopenda na usichopenda, ni sehemu
muhimu ya kujilinda.
Je, ni kweli kwamba uvutaji wa bangi hukufanya uwe na nguvu?
Updated at: 2024-05-25 16:22:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Si kweli kabisa! Baada ya kuvuta bangi mtu hujiona kama jasiri sana na mwenye nguvu. Lakini madhara ya bangi ni kinyume na matarajio ya mtumiaji kwani mishipa husinyaa na ubongo hushindwa kufanya kazi zake vyema na kutoa uamuzi usio sahihi wa utendaji sahihi wa kazi za mwili.
Kwa nini wanaume wengi hupenda kufanya mapenzi baada ya kulewa; na wasichana wengi hupatwa na vishawishi?
Updated at: 2024-05-25 16:24:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Pombe ina tabia ya kufanya ubongo kushindwa kufikiri, na kushindwa kujizuia na vishawishi vya kufanya mapenzi. Pombe huwafanya watu kustarehe, kuwa wazembe na kushindwa kutoa maamuzi ya busara kutokana na kutojali. Ndiyo maana kuna uhusiano sana kati ya maambukizo ya VVU na ulevi wa kupindukia.
Msichana wako ni kama jua linalotia nuru maisha yako kila siku. Hapa ni vidokezo kadhaa vya kuonyesha shukrani yako kwa yule mrembo uliyonaye kando yako.
Updated at: 2024-05-25 16:21:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hivi karibuni, wanaume wengi wamekuwa wakikosa jinsi ya kuonyesha shukrani kwa msichana wao. Hata hivyo, ni muhimu kwa wanaume kuelewa kwamba ni muhimu kuonyesha shukrani kwa mpenzi wao, na hata kama inaonekana ndogo, inaweza kuwa na athari kubwa kwa uhusiano wako. Kwa hivyo, hapa kuna vidokezo vyenye mapenzi vya kuonyesha shukrani kwa msichana wako.
Mpe zawadi ya kimapenzi: Jinsi bora ya kuonyesha shukrani kwa mpenzi wako ni kumpa zawadi ya kimapenzi. Hii inaweza kuwa kitu kidogo kama maua au kitu kikubwa kama chokoleti au pete ya ndoa. Kumbuka, sio kuhusu thamani ya zawadi hiyo lakini ni kuhusu kuthamini uhusiano wako.
Andika barua ya upendo: Hii ni njia nzuri ya kuonyesha shukrani kwa msichana wako. Andika barua ya upendo kwa mkono wako mwenyewe na kumwambia jinsi anavyothaminiwa na jinsi anavyofanya maisha yako kuwa bora.
Mpikie chakula chake kipendwa: Anapenda chakula gani? Mpikie chakula chake kipendwa na kumwambia jinsi unavyopenda kwa nini yeye ni mtu muhimu katika maisha yako.
Tumia muda pamoja: Kuna kitu cha kimapenzi kuhusu kutumia muda pamoja. Jitahidi kupanga siku ya kupendeza kwa ajili yake, kama kwenda kutembelea maeneo mapya kwenye jiji au kutazama sinema.
Mwambia jinsi anavyokuwa mzuri: Ni muhimu kwa mwanamke kusikia jinsi anavyofanya maisha yako kuwa bora. Mwambie jinsi anavyokuwa mzuri, jinsi anavyoonyesha upendo wake na jinsi anavyokutia moyo.
Onyesha maombi ya kimapenzi: Kuna kitu cha kimapenzi kuhusu kumuomba msichana wako kwa njia ya mapenzi. Sema kitu kama "Nimekuwa nikifikiria juu ya wewe siku zote, na ninapenda kuwa wewe uwe sehemu ya maisha yangu kwa muda mrefu."
Kwa ujumla, kuna njia nyingi za kuonyesha shukrani kwa msichana wako. Muhimu zaidi, ni kwamba kuonyesha shukrani kunaboresha uhusiano wako na kuweka upendo wenu hai. Jaribu njia hizi na utaona jinsi zitakavyofanya maisha yako na uhusiano wako kuwa bora zaidi.
Je, nini kitatokea iwapo mwanamke atatumia dawa za kulevya wakati wa ujauzito?
Updated at: 2024-05-25 16:22:34 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kama mama mjamzito atatumia dawa za kulevya basi humuathiri mtoto moja kwa moja. Mtoto aliye tumboni hulishwa kupitia damu ya mama yake. Kwa hiyo mama mjamzito anapotumia dawa hizo za kulevya, dawa huingia mwilini mwa mtoto anayekua. Matumizi ya dawa za kulevya pia huongeza uwezekano wa mimba kuharibika.
Kwa nini Albino wanatengwa katika masuala ya mapenzi na wale watu ambao siyo Albino?
Updated at: 2024-05-25 16:24:14 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu huogopa kujaribu vitu au mambo ambayo hawajayazoea au yale ambayo yapo tofauti. Jinsi unavyozidi kujua ukweli kuhusu sababu za ualbino ndipo unavyoweza kujenga mtazamo chanya ikiwemo kuwapenda. Wapo pia watu wengi katika jamii yetu ambao wana mahusiano ya kimapenzi na Albino na ambao wapo katika ndoa. Watu wengine katika jamii wanapoona mifano hiyo inasaidia katika kuondoa wasiwasi na kuondoa imani potofu.
Updated at: 2024-05-25 16:23:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na muliwaze maana amepata jambo la kutisha. Na iwapo mtu amejeruhiwa sana mpeleke katika kituo cha huduma za afya kilicho karibu mara moja. Vinginevyo ongozana na rafiki yako kwenda kituo cha Polisi na kutoa taarifa kuhusu jambo lililotokea. Polisi watampa fomu ambayo ataipeleka kwa mtoa huduma. Ni muhimu usijioshe kwa maji kabla hujachunguzwa na mtaalamu wa afya kwani kufanya hivyo kutaondoa ushahidi wa kubakwa. Kwa kuwa kupitia utaratibu huu inakuwa vigumu mwathiriwa anahitaji msaada wa karibu na uangalizi. Mzazi au rafiki anahitajiwa aongozane naye na kumsaidia, kwa mfano kuhakikisha kuwa katika kituo cha polisi msichana ahojiwe na polisi wa kike. Mtu aliyebakwa anahitaji kusaidiwa kihisia ili aweze kusahau mawazo na jambo liliomtokea. Kwa mwathirika, ni muhimu apewe ushauri nasaha ili aendelee kujihisi kwamba yeye bado yupo kama mtu wa kawaida. Ni muhimu pia kuzishughulikia habari za mwathiriwa kwa siri. Usimweleze kila mtu kilichotokea. Waeleze wale tu ambao unafikiri wanaweza kusaidia kama daktari, mwalimu au mzazi. Usiulize maswali ya kwa nini maana inaweza ikaonekana ni kosa la mwathiriwa. Badala yake zungumza na huyo mtu kwa utaratibu, polepole, peke yake na mpe uangalifu wa kutosha. Hakikisha kwamba hutoi lawama yoyote kwa mwathiriwa. Kubakwa kamwe siyo kosa la mwathiriwa.
Kufahamu tabia ya rafiki yako wa kike/kiume kabla ya kuoana hata kama anaishi mbali
Updated at: 2024-05-25 16:22:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Unaweza kufanya uchunguzi wa kutosha kuhusu tabia, muono na imani ya rafiki yako hata kama mnaishi mbalimbali. Unaweza kumuuliza maswali kuhusu mahali anapoishi na familia yake kwa ujumla. Jaribu kufanya mawasiliano ya karibu zaidi ili uweze kumdadisi, na yeye aweze kujieleza mwenyewe kwa undani zaidi kuhusu yeye mwenyewe.
Njia nyingine ni kutumia watu wengine walio karibu naye. Unapomchunguza mtu ambaye unafikiri anaweza kuwa mchumba wako inakubidi uwe na vigezo ulivyojiwekea ambavyo ungependa awe navyo.
Uchunguzi wa namna hiyo unaweza kukusaidia kujua tabia ya rafiki yako. Hata hivyo kufanya uchunguzi hakuna maana kwamba huhitaji kuwa naye kabisa. Bado unahitaji muda zaidi wa kuwa naye ili kumjua na kujenga uhusiano.
Jambo la kukumbuka ni kwamba tabia, siyo rahisi kufahamika na kuelezeka waziwazi, na hasa kama watu wako kwenye mapenzi. Mara nyingi katika mazingira haya siyo rahisi kuona kasoro. Vilevile tabia ya mtu huenda ikabadilika kulingana na umri.
Je, watu wanaoishi na hali ya ualbino wanaweza kuzaa watoto wangapi?
Updated at: 2024-05-25 16:24:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kwa vile Albino hana tofauti na watu wengine inopokuja kwenye suala la idadi ya watoto wa kuzaa jambo la msingi ni yeye mwanamke au mwanaume Albino kuzaa idadi aliyojipangia mwenyewe. Akitia maanani uwezo alio nao wa kuwatunza na kuwapa mahitaji muhimu.
Kwa nini wasichana wakiingia utu uzima damu zinaanza kutoka kwenye uke?
Updated at: 2024-05-25 16:22:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kutoka damu (hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo na hii ni dalili ya mtoto wa kike kuingia utu uzima,0 yaani kuwa mwanamke. Wasichana wanavunja ungo kati ya umri wa miaka 8 na umri wa miaka 18. Lakini, kuvunja ungo haina maana kwamba unahitaji kuanza kujamii ana. Kwa sababu ukijamii ana kuna hatari ya kupata mimba!
Mwanzoni siku za hedhi zinaweza kuwa na mabadiliko sana. Ni baada ya muda ndipo msichana anaanza kwenda mwezini mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo, wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo. Idadi ya siku katika mzunguko wa hedhi ni siku 21 hadi 35.Ukitaka kuelewa kabisa maana ya kutoka damu za mwezi, lazima nieleze kuhusu mzunguko wa hedhi. Siku ya kwanza ya damu huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa.
Na vilevile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mirija ya kupitishia mayai hadi kwenye mfuko wa uzazi. Mwanamke anapata mimba kama yai likirutubishwa na mbegu ya kiume ndani ya mirija ya kupitisha mayai, i ina maana, kwamba atakuwa amejamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka. Kama yai halikurutubishwa, basi hufa na hutangulia kutoka kama ute, pia utando kwenye mfuko wa uzazi na kuta za uzazi hubomoka na kutoka kama damu. Hii ndiyo hedhi yenyewe.
Endapo msichana amejamiiana na mvulana na yai likarutubushwa, hataona hedhi na aelewe kwamba kuna uwezekano kwamba mimba imetungwa.
Mzunguko wa hedhi kwa baadhi ya wasichana hauna mpangilio mwanzoni, hivyo endapo hupati hedhi inayolingana kila mwezi usijali.
Katika hali ya kawaida usipopata hedhi na hukujamiiana na mvulana, basi inawezekana ni mabadiliko tu ya mwili. Hali hii ikiendelea au ukiwa na wasiwasi unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya