Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi
Mchele wa basmati - 3 vikombe
Kuku - ½
Bilingani - 2 ya kiasi
Viazi - 4
Vitunguu - 2
Kitunguu (thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 2
Chumvi - kiasi
Garama masala (mchanganyiko wa bizari) - 1 kijiko cha chai
Hiliki ya unga - ¼ kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia wali - ¼ kikombe
Mafuta ya kukaangia viazi na bilingani - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele. Kata kuku vipande upendavyo safisha Kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu, na bizari mchanganyiko (garama masala). Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria. Menya na kata viazi kaanga weka kando. Kata kata bilingani slesi nene kaanga, chuja mafuta weka kando. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia vipande vya kuku, ukaange kidogo. Tia supu ya kuku, mchele, tia hiliki, ufunike hadi karibu na kuwiva kabisa. Tia viazi na bilingani uchanganye kidogo, kisha tia katika oven imalizike kupikika pilau humo au unaweza kuendelea kufunika juu ya jiko hadi pilau iwive. Pakua katika sahani ikiwa tayari kuliwa kwa saladi ya mtindi.
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 2 Mugs
Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) - Mug
Tuna (samaki/jodari) - 2 kopo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu
Garam masala - 1 kijiko cha supu
Nyanya - 2
Kitungu maji - 1
Mdalasini nzima - 2 vijiti
Karafuu - 6 chembe
Pilipili mbichi - 1
Chumvi - kiasi
Viazi - 3
Maji - 2 ½ Mugs
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Maandalizi
Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20 Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga. Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive. Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu. Tia maji, yatakapochemka tia mchele. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi (potato) 1/2 kilo Mafuta ya kukaangia (veg oil) Chumvi
Matayarisho
Menya viazi kisha vioshe na vikaushe maji yote kwa kutumia kitchen towel.Baada ya hapo katakata katika shape ya chips uzipendazo either nyembamba au nene kisha zikaushe tena maji na uzitie chumvi. Baada ya kuzitia chumvi tu zitie kwenye mafuta ya kukaangia straightaway (hakikisha mafuta yasiwe ya moto sana kwani utazibabua) Zipike upande mmoja ukiiva geuza upande wa pili. Baada ya hapo endelea kuzipika uku ukiwa unazigeuzageuza mpaka kwa nje ziwe light brown na crisps.Baada ya hapo zitoe na uziweke kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:05 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mayai yaliochemshwa 4 Nyama ya kusaga robo kilo Kitunguu swaum Tangawizi Limao Chumvi Pilipili Breadcrambs Carry powder Binzari nyembamba ya unga Yai moja bichi Mafuta
Matayarisho
Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) 100g Sukari (sugar) 100g Siagi isiyokuwa na chumvi (unsalted butter) 100g Mayai (eggs) 2 Vanila 1 kijiko cha chai Chumvi pinch Warm water 3 vijiko vya chakula
Matayarisho
Kwanza washa oven moto wa 200 C. Baada ya hapo saga butter na sukari mpaka viwe laini kisha tia mayai na uendelee kusaga mpaka vichanganyike vizuri kisha tia unga, vanila, chumvi na na maji na usage mpaka upate uji usiokuwa mzito sana au mwepesi sana. Baada ya hapo utie kwenye baking tin na u bake kwa muda wa dakika 25 na mpaka cake yako iive yani juu na chini iwe ya brown na ukidumbukiza kijiti katikati kinatoka kikiwa clean. Baada ya hapo itoe kwenye tin na uiache ipoe. Ikisha poa itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa Basmati /Pishori - 4 vikombe
Kuku
Vitunguu - 3
Nyanya/Tungule - 2
Tangawizi mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi nzima - 3
Ndimu - 2
Garama Masala/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu
Haldi/tumeric/bizari manjano - 1 kijiko cha chai
Pilipilu ya unga nyekundu - 1 kijiko cha chai
Mtindi /yoghurt - 3 vijiko vya supu
Mafuta ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele, roweka. Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli. Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu. Punguza mchanganyiko kidogo weka kando. Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi. Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive. Epua, weka kando. Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando. Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali. Tia kuku uchaganye vizuri. Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja. Punguza masala nusu yake weka kando. Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali. Funika upike katika oveni hadi uive. Changanya unapopakua katika sahani.
Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga
Updated at: 2024-05-25 10:23:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama isiyokuwa na mifupa - 1 ½ Lb(ratili) Mchele wa Basmati (rowanisha) - 3 Magi Vitunguu maji - 2 Mchanganyiko wa mboga za barafu - 1 Magi (karoti, mahindi, njegere) Pilipili Mbichi - 3 Pilipili mboga kijani na nyekundu - 1 Pilipili manga - ½ kijiko cha chai Chumvi - Kiasi Sosi ya soya (soy sauce) - 5 Vijiko vya supu Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu Mchanganyiko wa bizari (garam masala) - 1 Kijiko cha supu Kotmiri iliyokatwa - ½ Kikombe Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kutaarisha
Ndani ya sufuria, tia mafuta yakipata moto kaanga vitunguu mpaka ziwe rangi ya hudhurungi. Kisha tia nyama iliyokatwa vipande vidogo vidogo pamoja na maji ya kiasi na viungo vyote isipokuwa mchele, mboga zote na kotmiri. chemsha mpaka nyama iwive na maji yakauke. Halafu changanya na mboga na iwache kwa muda wa dakika kumi kisha tia kotmiri na umimine kwenye bakuli au treya ya oveni na uweke kando. Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja, kisha umwagie juu ya ile treya ya nyama. Nyunyizia mafuta na sosi ya soya na ipike katika oveni moto wa 350° kwa muda wa dakika 20 hivi. Ukishawiva, uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:23:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga wa mchele - 500g
Samli - 250g
Sukari - 250g
Hiliki iliyosagwa - 1/2 kijiko cha chai
Arki (rose flavour) - 1/2 kijiko cha chai
Baking powder - 1 kijiko cha chai
Mayai - 4
Maji ya baridi - 1/2 kikombe cha chai
MAANDALIZI
Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa.