Mapishi ya Wali Wa Tambi Na Kuku Wa Sosi Ya Mtindi
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo Vya Wali
Mchele - 3 vikombe
Tambi - 2 vikombe
Mafuta - ¼ kikombe
Chumvi
Vipimo Vya Kuku
Kuku kidari (boneless) aliyekatwa katwa vipande - 1 Kilo
Kitunguu maji kilichokatwa katwa - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Paprika - 1 kijiko cha supu
Masala ya kuku (tanduri au yoyote) - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 2 vijiko vya supu
Mtindi (yoghurt) au malai (cream) - 1 kikombe
Mafuta - ¼ kikombe
Majani ya kotmiri (coriander) - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali:
Osha Mchele, uroweke. Tia mafuta katika sufuria, kaanga tambi zilizokatwakatwa hadi zigeuke rangi kuwa nyekundu. Tia mchele endelea kukaanga kidogo. Tia maji kiasi cha wali kupikika kama unavyopika pilau. Kiasi cha maji kinategemea aina ya mchele Funika katika moto mdogo mdogo hadi uive ukiwa tayari.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku
Katika bakuli, changanya vitu vyote isipokuwa mtindi na kitunguu. Tia mafuta katika karai, kisha tia kitunguu ukaange muda mdogo tu, usikiache kugeuka rangi. Tia kuku na masala yake, endelea kukaanga, kisha tia mtindi au malai ufunike apikike na kuiva vizuri. Nyunyuzia kotmiri iliyokatwakatwa ikiwa tayari kuliwa na wali wa tambi.
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Mchele basmati, pishori - 3 vikombe
Vitunguu katakata - 2
Nyanya/tungule katakata - 5 takriban
Viazi/mbatata menya katakata - 3 kiasi
Thomu (saumu/garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha kulia
Hiliki ya unga - ½ kijiko cha chai
Kidonge cha supu - 2
Chumvi - kisia
Mafuta - ½ kikombe
Maji ya moto au supu - 5 takriban
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha na roweka mchele Katika sufuria weka mafuta yashike moto, tia viazi, vitunguu ukaange. Vikianza tu kugeuka rangi tia thomu na bizari, hiliki, endelea kukaanga kidogo. Tia nyanya kaanga lakini usiache zikavurugika sana. Tia mchele ukaange chini ya dakika moja. Tia maji ya moto, na kidonge cha supu au supu yoyote kiasi cha kufunika mchele yazidi kidogo. Koroga vichanganyike vitu, kisha funika upike kama pilau. Pakua ikiwa tayari, tolea kwa samaki wa kukaanga au kitoweo chochote kile
Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana na nimlo uliokamilika.
Mahitaji
Tambi ½ paketi
Vitunguu maji 2 vikubwa
Karoti 1
Hoho 1
Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
Carry powder kijiko 1 cha chai
Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
Mafuta kwa kiasi upendacho
Mayai 2
Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu 2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni 3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva. 4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya . 5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula
Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.
Mapishi ya Pilau Ya Nyama ya Kusaga, Adesi Za Brauni Na Zabibu
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa Par boiled au basmati - 5 vikombe
Nyama kondoo/mbuzi ya kusaga - 1 kikombe
Kitunguu - 2
Kitunguu saumu (thomu/galic) - 7 chembe
Adesi za brauni (brown lentils) - 1 kikombe
Zabibu - 1 kikombe
Baharaat/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu
Chumvi - kiasi
Pilipilii manga - ½ kijiko
Jiyra/bizari pilau/cummin - 1 kijiko cha chai
Supu ya nyama ng’ombe - Kiasi cha kufunikia mchele
Mafuta - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha
Osha, roweka masaa 2 au zaidi.
Katakata (chopped)
Menya, saga, chuna
Osha, roweka, kisha chemsha ziive nusu kiini.
Osha, chuja maji
Namna Ya Kupika:
Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka vyekundu. Tia kitunguu thomu, kaanga, tia baharati/bizari zote kaanga. Tia nyama uchanganye vizuri, ukaange iwive.. Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu, koroga kidogo, funika uivie mchele. Karibu na kuiva, tia adesi, zabibu, changanya, funika uendelee kuiva kama unavyopika pilau. Epua pakua katika chombo, ongezea zabibu kupambia ukipenda
Mapishi ya Biriani Ya Samaki Nguru, Njegere Na Snuwbar (UAE)
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa basmati - 4 cups
Samaki nguru (king fish) - 7 vipande au zaidi
Kitunguu - 5
Nyanya/tungule - 3
Njegere - 1 kikombe
Snuwbar (njugu za pine) - 1 kikombe
Viazi - 2 kata kata mapande makubwa
Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu
Kitunguu saumu - 1 kijiko cha supu
Pilipili nyekundu - 1 kijiko cha chai
Bizari ya biriani/garama masala - 1 kijiko cha supu
Namna Ya Kupika:
Kaanga samaki mbali kwa viungo upendavyo umkoleze vizuri. Au choma (bake/grill) katika oveni ukipenda. Weka mafuta katika sufuria, tia vitunguu kaanga hadi vigeuka rangi. Gawa sehemu mbili. Sehemu moja bakisha katika sufuria kisha tia tangawizi mbichi na kitunguu thomu ukaange. Tia nyanya kaanga kisha tia bizari zote endelea kukaanga, tia njegere, njugu za snuwbar na ndimu kavu. Tia viazi ulivyokwishakaanga, na vitunguu vilobakia. Tia mapande ya samaki, changanya na masala bila ya kumvuruga samaki. Chemsha wali kisha mwagia juu yake, funika upike ndani ya oveni au mkaa hadi wali uive kama unavyopika kawaida ya biriani. Epua pakua huku ukichanganya na masala ya samaki.
Mapishi ya Wali maharage,mchuzi wa samaki na spinach
Updated at: 2024-05-25 10:37:46 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele (rice 1/2 kilo) Maharage yaliyochemshwa (boiled red kidney beans 1 kikombe cha chai) Samaki waliokaangwa ( 2 fried fish) Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 ya tin) Vitunguu vilivyokatwa (onion 2) Kitunguu swaum (garlic 3 cloves) Tangawizi (ginger kiasi) Limao (lemon 1/2) Chumvi (salt) Pilipili (scotch bonnet pepper 2) Mafuta (vegetable oil) Spinach Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai)
Matayarisho
Saga nyanya, kitunguu, tangawizi na kitunguu swaum pamoja. Tia kwenye sufuria na upike mpaka maji yakauke kisha tia curry powder, mafuta na chumvi na upike tena mpaka mchanganyiko uive kisha tia samaki na limao na maji kiasi na uache uchemke kiasi. Na hapo mchizi utakuwa tayari. Osha na uzikate spinach kisha kaanga kitunguu na mafuta kiasi (hakikisha visiwe vya brown kisha tia spinach na chumvi. zipike kwa muda wa dakika 3-4 na hapo zitakuwa tayari zimeshaiva. Wali: Chemsha maji kiasi kisha tia, chumvi, pilipili nzima(isikatwe) mafuta na tui la nazi. Baada ya hapo koroga na utie mchele na maharage na ufunike uache uchemke mpaka maji yakauke. Kisha geuza na ufunike tena na uuache mpaka uive. Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuseviwa.
Updated at: 2024-05-25 09:52:20 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa) Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa) Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai) Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai) Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa) Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula) Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)
Matayarisho
Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu.
Jinsi ya kupika
Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua vyote vilivyobaki.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Choroko kikombe 1 na nusu Nazi kopo 1 Kitunguu kikubwa 1 Nyanya 1/2 kopo Swaum 1 kijiko cha chai Curry powder 1 kijiko cha chai Chumvi kiasi Olive oil Pilipili nzima
Matayarisho
Loweka choroko usiku mzima kisha zichemshe mpaka ziive na ziweke pembeni. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, na swaum kisha vipike mpaka maji yote, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko,tui la nazi, maji nusu kikombe,pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Mi huwa napenda kuila na wali ila hata na ugali au chapati inaenda pia.